Utetezi wangu wa wazi wa William Ngeleja - The use of Emergency Powers Act 1986

Utetezi wangu wa wazi wa William Ngeleja - The use of Emergency Powers Act 1986

SG project ilikuwapo muda mrefu, matayarisho ya mwanzoni yalishafanywa, sote tunajua huu mradi is being pushed aside for selfishness!!! Ngereja hawezi kuepuka hili mkuu MKJJ!!!

Kwa ufupi the whole CCM group will never come clean on this!!! The truth is, SG is the only solution to this problem!!!
 
Na ukweli wa mambo ni kwamba hakuna mtu anayejua jinsi ya kulitatua hili tatizo kwani kama angekuwepo ama wangekuwepo basi lingekuwa limeshatatuliwa. Nani anabisha? Kama yupo anayebisha na ani prove wrong basi kwa kulitatua na kulifanya liwe historia. Simple as that!!
 
Nyani Ngabu, mimi naona kama kweli JK anataka kujisafisha na kuonekana ni shupavu, huu ndiyo wakati wa kutuonyesha yeye ni kiongozi kufuta hili tatizo!!! MKJJ ametoa a light on hoe he can!! Maana mawaziri wabo vu ni zigo lake, he should clean his own mess!!!

Siyo hii strategy yake ya kutafuta wabunge wachache kushambuliana beungeni, anaongeza mazingaombwe tu, ili wakulima kama mimi tuhadaike naye!!! Aache ulegelege afanye maamuzi sasa...
 
mkuu hapo kwenye red bold. Mkjj anamaanisha rais atangaze "hali ya hatari" ili apate madaraka ya kutatua hili tatizo yeye kama yeye; maana akitanga hilo, any other laws seizures!!
nimesoma nimemuelewa mmj mkuu hayo yote yanatokana hii kitu "emergency power back up"-hapa ndipo ambapo waweza wakaamua kupingisha sheria ili wanunue mitambo hewa na zamu hii tutegemee zaidi ya richmomd . Tutaenda tutazunguka lakini ukweli ni kwamba watawajibishana mpaka raisi wao lakini .strategically wamejipangaje kuhusu kumaliza hili suala la mgao ?. Infinite solution ni serikali iliyopo istep down tupate vichwa vingine vireform hii nchi
mitambo mipya hiyo ya 100mw iliyoletwa mpaka installation ikamilike ni desemba ambapo mvua sitaanza kunyesha baadae kwa kuwa mipango yetu ni mibovu itakuwa redundancy halafu tutakuwa tunalipa gharama za uendeshaji kizembe tu...
 
Na ukweli wa mambo ni kwamba hakuna mtu anayejua jinsi ya kulitatua hili tatizo kwani kama angekuwepo ama wangekuwepo basi lingekuwa limeshatatuliwa. Nani anabisha? Kama yupo anayebisha na ani prove wrong basi kwa kulitatua na kulifanya liwe historia. Simple as that!!
Kutokuwepo au kuwepo mtu wa kulitatua tatizo its assumptions ambazo nadhani sio vema to deal with assumptions...
Jambo la muhimu ni kwamba when you step up to do a job, you are required to do the job.., ukishindwa then you step down.., hapa tukianza kuwapa watu leeway ya kushindwa kazi eti kazi ni ngumu na hakuna mtu wa kuifanya then we are heading for disaster...,

kama hakuna mtu wa kuweza kufanya kazi basi ni bora hio kazi ifutwe au wapewe watu zaidi ya mmoja kufanya hiyo kazi na sio kulimpa mtu pesa wakati he is doing nothing at all
 
Sasa hivi hata tanesca wanapitia humo humo!!

Kinachisikitisha serikali imekaa kimya, so neither me nor you hatujui lini tutaanza kuona solution!!!
 
Tutaenda tutazunguka lakini ukweli ni kwamba watawajibishana mpaka raisi wao lakini .strategically wamejipangaje kuhusu kumaliza hili suala la mgao ?. Infinite solution ni serikali iliyopo istep down tupate vichwa vingine vireform hii nchi


Mganga wa kweli, hii pointi yako ni ya msingi sana. Mimi maoni yangu ni kwamba kwa ujumla mfumo wa CCM kifalsafa na kiutekelezaji haiendani kabisa na fikra za watanzania zama hizi; na labda hiyo ni matokeo ya mapungufu ya katiba ya sasa hivyo tunahitaji kutengeneza mfumo wa kikatiba utakaotupatia viongozi wenye akili na ubunifu. Kwenye taifa lenye katiba makini Ngeleja, Hawa Ghasia, Kikwete, etc. wasingepata kuwa viongozi muhimu wa serikali.
 
Tatizo kubwa tunalojitumbukiza watanzania kwa sasa ni kupambana na watu binafsi, individuals, badala ya mfumo uliopo. MM umeelezea kwa kina na ufasaha, nakubaliana nawe!

Tuuondoshe mfumo huu wa sasa unaokumbatiwa na serikali ya ccm ili tuanze upya kuijenga nchi yetu. Hiyo ndiyo rai yangu kwa watanzania. Tunaweza kuufanya mgao wa umeme histioria kwa kuamua kutenda bila woga, kwa moyo wa dhati INAWEZEKANA.

"Uwezo tunao, rasilimali tunazo, tuamue sasa"
 
Kutokuwepo au kuwepo mtu wa kulitatua tatizo its assumptions ambazo nadhani sio vema to deal with assumptions...
Jambo la muhimu ni kwamba when you step up to do a job, you are required to do the job.., ukishindwa then you step down.., hapa tukianza kuwapa watu leeway ya kushindwa kazi eti kazi ni ngumu na hakuna mtu wa kuifanya then we are heading for disaster...,

kama hakuna mtu wa kuweza kufanya kazi basi ni bora hio kazi ifutwe au wapewe watu zaidi ya mmoja kufanya hiyo kazi na sio kulimpa mtu pesa wakati he is doing nothing at all

I still maintain that there is no one, absolutely no one that knows what to do. If there is one out there, then he or she should prove me wrong.
 
mie naunga mkono hoja, ila nashauri tutumie njia hiyo hiyo ya kutangaza kuwa nchi ipo ktk hali ya hatari na sio kwa umeme tu, bali kwa ukali wa maisha kwa ujumla wake na tutumie njia ya dharura hiyo hiyo kuiondoa serikali iliyopo madarakani kabla ya 2015
 
Ni kweli kuwa tatizo la umeme ni la siku nyingi na ni la kimfumo zaidi kwa hiyo haliwezi kutatulika katika mfumo ule ule. Nisichokubaliana ni hoja ya namna ya kulitatua hili tatizo.

Sheria katika nchi hii hazijawahi kuwa tatizo la kuwazuia watendaji walio willing na nia njema kufanya mambo makubwa kwa ajili ya taifa hili. Sheria zinawalinda na kuwaunga mkono. Tatizo ni nia wanazokuwa nazo watendaji. Sheria ya manunuzi ya umma si tatizo na kuisimamisha kwake hakuwezi kuwa solution kwa matatizo ya umeme hata kwa muda mfupi. Ukitaka kujua hilo angalia Richmond!!!! Kwani hapa sheria ya manunuzi ya umma ilikuwa tatizo?

Tatizo letu ni watu wabovu waliokwishajazana kila mahali. Pengine ndugu Mwanakijiji umeelezea vizuri matatizo makubwa ya kisera yaliyoletwa na Azimio la Zanzibar. Hapa ndipo treni yetu ilipo-derail. Sababu kubwa ni kuwa viongozi walioruhusiwa kuwa wafanyabiashara vile vile wasingeweza kufanya uongozi na biashara kwa wakati mmoja bila kimoja kuingilia kingine. Wakati viongozi wanapofikiria kufanya maamuzi ya kitaifa, maslahi ya kibiashara ya mtu mmoja mmoja huingilia na HAPA NDIPO tatizo kubwa lilipo. Kama viongozi wangekuwa wakifanya maamuzi kwa kuangalia maslahi ya kitaasisi na kitaifa, tusingekuwa hapa tulipo!

Kwa hiyo, suluhisho la kwanza ni kukubali kuwa Azimio la Zanzibar ndiyo tatizo na kulifutilia mbali mara moja. Haitakuwa na maana ikiwa tutalifutilia mbali na kurejesha Azimio la Arusha; kwani mazingira ya sasa hayaruhusu Azimio la Arusha kurudi kama lilivyo. Lakini inabidibi tufanye maamuzi makubwa sana yatakayowalazimisha viongozi walioko madarakani kutumia asilimia mia moja ya muda wao wa kazi kufanya kazi zao za umma. Leo viongozi wengi wanatumia ofisi zao kama vijiwe tu vya kufanyia mambo yao binafsi huku kazi za umma zikipewa muda mdogo mno! Katika hali kama hiyo hatuwezi kufika kokote!

Suala ni kuwa katika "superstructure" iliyopo; Aina ya viongozi waliopo na mifumo iliyopo, hayo yanawezekana? Sipendi kuwa mtu wa kukata tamaa mapema lakini kusema ukweli inahitaji "fresh mind". Viongozi waliopo na mifumo iliyopo na mazonge zonge yake yote haviwezi kututoa hapa; tutaendela kulia hadi hapo wananchi watakapokuwa tayari kufanya uamzi mkubwa. Uamzi wa kuing'oa CCM na serikali yake na kuipumzisha. Watakaoingia watakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi tofauti na kuyasimamia.

Kansa iliyopo ni kuwa sasa hivi hakuna uamzi wa kutumia fedha nyingi utafanyika bila maslahi ya watu binafsi watakaohusika kuwa mbele kwanza. Hili ndo linatatiza miradi mingi; iwe ni ya umeme, vitambulsho vya utaifa, kupanua bandari, n.k. Siku zote tutakuwa kwenye matatizo tu kwa sababu mfumo umeshafikia kwenye "ground zero". Kila mtu anajua kuwa katika mradi ule, fulani na fulani walinufaika hivi; kwa nini na yeye asinufaike? Matokeo yake ni kuwa miradi yetu yote ama inasimama kabisa; au inatoa robo tu ya matokeo yaliyotarajiwa. Kwa kifupi "we are in a shit and there is little hope" kwa sababu watanzania hawana uwezo wa kuliona tatizo hili na kulifanyia kazi! Watanzania wana uwezo wa kushabikia tu!!
 
Mwanakijiji unataka kubariki utawala wa kiimla kisheria! Wameshindwa kulitatua tatizo kidemokrasia ndio wataweza kidikteta? Kwa mujibu wa hii Katiba kuukuu isiyo na uhalali wa wananchi unayoitetea humu Rais tayari ana madaraka makubwa na ya kutosha kulitatua hilo tatizo bila kutangaza hali ya hatari.
 
Mwanakijiji unataka kubariki utawala wa kiimla kisheria! Wameshindwa kulitatua tatizo kidemokrasia ndio wataweza kidikteta? Kwa mujibu wa hii Katiba kuukuu isiyo na uhalali wa wananchi unayoitetea humu Rais tayari ana madaraka makubwa na ya kutosha kulitatua hilo tatizo bila kutangaza hali ya hatari.

Huu ndo ukweli mtupu! Rais halitatui tatizo kwa sababu; Hana uwezo wa kimkakati wa kuona ufumbuzi wa hilo tatizo au haoni kuwa kuna tatizo kubwa linalohitaji kufanyiwa kazi. Si kwa sababu kuna vikwazo vya kisheria au kimfumo; rais wa Tanzania kwa katiba iliyopo hakuna uamzi ambao unaweza kumshinda. Wala halazimiki kutumia HALI YA HATARI, never!!
 
Hakuna wakati hata mmoja kuanzia ukoloni mpaka sasa, Tanganyika na sasa Tanzania ilipojitosheleza kwa umeme.

Kwa sasa na jinsi matumizi yanavyokuwa kwa kasi, na wengi kuhamia mijini na kuona raha ya umeme. Matumizi ya hapo ulipo umeme yameoingezeka maradufu.

Si siri, hakuna awamu iliowekeza katika umeme kuanzia kabla ya Uhuru na mpaka hii leo, zaidi ya awamui hii ya Kikwete. Miradi zaidi ya 20 ya kuzalisha umeme, miradi zaidi ya 50 ya usambazaji wa umeme. Jitihada za makusudi kabisa za kubadili sheria za ufuaji na usambazaji wa umeme, kututoa kutoka mfumo wa kuitegemea Tanesco pekee, umeb uniwa na kutendeka awamu hii.

Kina Mwanakijiji mna yenu mnayoyatafuta lakini ukweli unabaki kuwa ukweli na fumbo hufumbiwa mjinga.
 
umeme! umeme! umeme! Hiki ni kilio cha tangu nenda miaka rudi. Hapo ni asilimia 10 ya wenye uwezo wa kuupata kwa watanzania wote mil. 40. Ngeleja go 2 hell, ccm dig ur grave, magamba burry ur self. U gat non power to control this conciouslic growing nation of poor but naughty teenagers and needy bt tired elders.
 
Ilihitaji Tafakari na uchambuzi wa Kina kufikia hapa. Naunga mkono hoja
 
Nyinyi kubalini tu kuwa hatuwezi kulitatua hili tatizo. Kama tunaweza tungekuwa tushalitatua. Sasa kama mpo ambao mnadhani mnaweza kulitatua hebu litatueni basi mniumbue mimi wenu mtukutu.....

Narudia tena, hakuna mwenye ubavu wala werevu wa kulitatua hili tatizo.
 
Mimi naona hata hawa jamaa nao wanakuwa wavivu sana katika kusoma maana kwa hali kama hii na maelezo haya basi ingekuwa rahisi sana katika kusoma hata waziri kuona waziri na maneno yasiyokwisha na watu, wanataaluma na wasomi na wanasiasa kama vile wamelala hakuna jipya na zaidi ya kusema. Hongera mzee na babu yangu mwanakijiji
 
Awali ya yote nikupongeze kwa uchunguzi mzuri wa kiini, mizizi ana uendelevu wa matatizo ya umeme nchini.
Kwanza, watanzania wote wanafahamu kwamba huyu waziri wa juzijuzi hawezi kuwa chanzo cha tatitzo mfumo wa takribani miaka ishirini, hilo halina ubishi. Penye ubshi, ni kwamba, je katika muda wake aliokaa ofisi hiyo, kimkakati kuondoa au kupunguza tatizo hili amefanya nini cha kuonekana angalau katika makaratasi!
La utetezi wa Ngeleja kwamba si mwanzilishi sawa, lakini yeye ndiyo mwenye dhamana, amefanya nini? Amepewa mayai via awapikiwe watanzania, akakubali, akayapika, akadai yanalika huku watanzania wakilia, ah via via, ebo wasing'ake!
 
Back
Top Bottom