UTEUZI: Camilius Wambura ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI)

UTEUZI: Camilius Wambura ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI)

Haya ni mapungufu makubwa yanayojirudia mara ya pili, ingekuwa ni mimi ningefagia hicho kitengo cha upekuzi chote waingie wapya ambao wapo makini na wenye uadilifu, wanaharibu legacy ya SSH na ataonekana hana umakini.

Ninashauri awe na timu nyingine ndogo kabisa isiyo rasmi itakayopitia majina ya wateule ambao tayari wameshafanyiwa upekuzi ili kuhakiki zaidi. Uhakiki huu wa kuwahakiki wahakiki ufanywe kabla ya majina kutangazwa rasmi na siyo uhakiki wa wahakiki unafanyika baada ya tukio.

Pia SSH awe na wasifu wa kila mteule wa page moja au nusu page ambayo anaweza kuipitia kwa haraka sana bila kuathiri majukumu yake mengine.
Aanze na Msigwa maana ndiyo mpotoshai namba 1
 
Mama anakurupuka sana. Na pale Ikulu bado hawajakaa sawa. Yaani mama anateua RAS mtu mwenye darasa la 12 kweli!!? Wanaomchomekea vimemo ndio wanampotosha mama. Inapaswa afanye individual vetting kabla ya kufanya uteuzi..
Mbona baba yako Magu alipokuwa anateua makada wa chama kuwa ma das na maras hukulalamika?
Mwacheni mama,msimpangie,kama ambavyo hamkumpangia Magu.
 
Dr Ulimboka hatamsahau maisha yake yote!

Hawa watu wanapokuwa kwenye nafasi wanajisahau na kusahau utu, kwamba kuna kesho na kesho kutwa! Siyo ajabu siku moja Ulimboka akamnunulia soda!
Sio kumnunulia soda tu mkuu itapendeza akimkuta Ulimboka kama daktari wa zamu siku akienda kupasua busha lake lile.
 
Barua ipo incomplete hatujaelezwa DCI aliyekuwepo amekwenda wp!!??

Kabisa taarifa hii kwa umma haijakamilika. Kufanya mabadiliko ngazi ya DCI huku hakuna maelezo kigogo aliyekuwepo hatuambiwi kama kastaafu au kupangiwa majukumu mengine inazua masualu mengi sana katika duru za usalama na intelejensia ya polisi.

Kutoka maktaba: Taarifa kwa umma tarehe 20 December 2017:



Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI CP Robert Boaz akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mwenendo wa makosa ya jinai leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Nsato Marijani Nzassa na Kamishna wa Rasilimali Watu Fedha na Logistic, Albert Nyamuhanga, na Mkuu wa Kitengo cha Makosa dhidi ya Maadili ya Jamii, Hussein Laissery
Source : MAELEZO TV

Kutoka maktaba :

 
Mpumbavu wewe, kwaiyo wewe una taarifa zaidi za watumishi kuliko Rais???mbona magufuli alikuwa anatengeua na kuteua kila uchao hamkusema?? Majungu gani ayo ambayo Rais kayapokea? au Kuna bwanaako kakosa ulaji ndio yanakutoka ayo dada
Mkuu nikutoe wasiwasi, humu nishawaambi, matusi kwangu ni maji ya kunywa, kuhusu ulaji mimi hata utawale wewe maisha yangu hayabadiliki. Unadhani kama vetting ipo vizuri hata wiki haija isha unabadili, kuwa rais unaeza kuwa na taarifa nyingi lakini zikawa Wrong, sababu kila mtu anainterest zake.
Unakumbuka ya TPDC hata masaa 12 hatakufika.
Punguza hasira mkuu kama uliumia pole.
Lakini lazima tuwe na wasiwasi kwa nini baadhi ya teuzi mpya zina tenguliwa mda mfupi sana hata madhaifu na ubora wao kwenye nafasi hizo hawajaonesha.
 
Huwa hawafanyi bahati mbaya, ni makusudi ili kukomoa. Hata mimi ningepewa hayo mamlaka ya kuteua na kutengua ningemteua bashite kuwa katibu mkuu kiongozi then masaa machache kabla ya kuapishwa namtengua nachagua mwingine. Kwani sh. Ngapi bana?
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji125][emoji125][emoji125]
 
kwahiyo majambazi ya dsm hapo nani atayashughulikia kama jamaa anaondoka dsm?
 
Lakini ni Bora kutengua immediately kuliko kuacha MTU ambaye ni incompetent Kwa kuogopa tuu negative reaction ya watu wachache.
"Incompetence" ni pamoja na kutokuwa makini kwenye uteuzi unaoishia kwenye "kutengua", au unaonaje mkuu 'kabulala'!
 
Umeeleweka mkuu, kazi inaendelea kuweka mpangilio mpya.
Hehe unachekesha huo mpangilio mpya kwani hao wanatoka sayari ya mars ,si ni hao hao wa kila siku, ni sawa tu na kubadili chapati kutoka upandewakwanza kwenda upande mwingine ukiona upande uliotangulia unaungua.
 
Sio kumnunulia soda tuu hata kumtibia ndugu yake au yeye mwenyewe kumbuka ULIMBOKA,NI DAKTARI
Sidhani kama atakubali kutibiwa na Dr Ulimboka, labda awe amepoteza fahamu, na ndugu zake wasimjue daktari!
 
Mkuu nikutoe wasiwasi, humu nishawaambi, matusi kwangu ni maji ya kunywa, kuhusu ulaji mimi hata utawale wewe maisha yangu hayabadiliki. Unadhani kama vetting ipo vizuri hata wiki haija isha unabadili, kuwa rais unaeza kuwa na taarifa nyingi lakini zikawa Wrong, sababu kila mtu anainterest zake.
Unakumbuka ya TPDC hata masaa 12 hatakufika.
Punguza hasira mkuu kama uliumia pole.
Lakini lazima tuwe na wasiwasi kwa nini baadhi ya teuzi mpya zina tenguliwa mda mfupi sana hata madhaifu na ubora wao kwenye nafasi hizo hawajaonesha.
Hii sura kama naipata vile...
 
Hii sura kama naipata vile...

Anaonekana alikuwa mbunge makini 2015-2020 kupitia viti maalum CCM
4 May 2017
Dodoma,Tanzania

Mbunge Azza alia na Mkoa wa Shinyanga kukosa X-Ray, Madaktari Bingwa, fedha kulingana na bajeti


Mbunge wa Viti maalum Azza Hilal Hamad amesema mkoa wa Shinyanga una X Ray Mashine moja tu na iliyopo imeharibika na kwamba kampuni ya Phillips haina mpango wa kuikarabati

Source : mwananchi digital


Azza ataka muswada sheria ya mfuko wa wanawake na vijana


10 Nov 2016
Mbunge wa viti maalum Azza Hilal Hamad amesikitishwa na kitendo cha Halmashauri kutopeleka asilimia kumi (10%) ya mapato yake katika mfuko wa wanawake na vijana
 
Tatizo SSH ameruhusu vimemo, baadhi ya majina yanapenyezwa ikija kufanyika proper vetting unakuta mtu hafai hiyo nafasi. SSH anahitaji kuwa mkali akiendelea kulegezea wapiga deal itakula kwake, haiwezekani kila siku kunakuwa na makosa kwenye uteuzi.
Na kwa nini proper vetting isifanyike kabla ya kutoa majina !!!??
 
Back
Top Bottom