Uteuzi: January Makamba ateuliwa kuwa Waziri wa Nishati. Ndugulile, Kalemani, Chamuriho na AG Kilangi watenguliwa, Feleshi ateuliwa

Kagoma kuachia hiyo Wizara huyo gaidi.
Wizara zote nyeti wamepewa wanawake, afya ,ulinzi,tamisemi, elimu,[emoji18][emoji18]mwigulu namshauri aachie wizara ya fedha mapema[emoji33][emoji33]
 
Wachaga tulio tanesko tutapumua kidogo. Loh ilikua Kama mchaga unaongoza kitengo Fulani Basi tulikua tunajua anytime 't' naweza zushiwa jambo
 
Mbarawa ndani ya Nyumba nilisikitika Sana mwendazake kumwacha huyu maana ni mchapakazi Sana Magufuli kusema kweli hakuipenda ZANZIBAR na alikuwa na UKABILA SANAA
 
Ndio hivyo tulivyoambiwa usiku huu , kwamba kuna wateule na watenguliwa wapya wako njiani kuja tena baada ya hawa wa leo kuapishwa .

Tunaambiwa hii ni mbinu mpya ya kubadili viongozi .

Tuendelee kusubiri tuone wateule wapya wanaokuja .
 
Tukianza tena umeme wa mgao lazima kuna atakayewajibu watanzania nini kinaendelea
 
Mkuu tunajadili bila kutukana, Kama hauni tunavyoyumba fumba macho kidg, halafu fumbua utaelewa... Yaan unaona sa iv kila siku teuzi teuzi hakuna la maana sa makamba nae wazir jamani hii nchi inavituko vikuu
Makamba ni mara yake ya kwanza hii kuwa Waziri?
 
Weekend njema wapendwa.
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri wa Tanzania.
Hii ndio Tanzania, au sio ndugu zangu!!!!
 
General, ulimwengu alisema Kuna uwezekano Yale ya guinea yanafika EA, ukwel mama anaupinga mwingiiiiiiiiii...
 
Kalemani amepambana sana umeme vijijini
Kuna Uzi upo humu ulitabir haya makamba atachukua nafasi kipindi ile ya mifumo ya luku kusimama
Aliyepambana sana na umeme wa vijijini ni Muhongo!! Usema ovyo wa Muhongo ulisaidia sana, kwa sababu wakati hili zoezi linaanza watu walishaanza habari za kulipwa sehemu zitakopita nguzo! Muhongo kama kawaida yake, akasema "halipwi mtu", na tukiona kijiji kinaleta mambo ya kutaka kulipwa, tunawaruka, tunaenda kule wanakohitaji umeme. Hili Muhongo sitamsahau hata chembe kwa sababu nakumbuka Bush kwetu tulitaka kuwekewa umeme mwaka 1995, lakini ikashindikana baada ya kijiji cha kabla yetu watu wake kugoma kukatwa miti yao (wanafanya sana kilimo cha miti) hadi walipwe! Zoezi likaishia hapo, tukaja kupata 2015.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…