Uteuzi: January Makamba ateuliwa kuwa Waziri wa Nishati. Ndugulile, Kalemani, Chamuriho na AG Kilangi watenguliwa, Feleshi ateuliwa

Uteuzi: January Makamba ateuliwa kuwa Waziri wa Nishati. Ndugulile, Kalemani, Chamuriho na AG Kilangi watenguliwa, Feleshi ateuliwa

Ndungulile nini tena kimetokea tukidhani angefaa kuwa Waziri wa Afya kuliko wale waliopo
 
Hivi Kibajaji hawamuoni miaka 20 bungeni hajawahi hata kuwa naibu,wapinzani waliohamia ndani ya miezi kadhaa wakapewa uwaziri
Kuna tofauti kubwa kati ya kupiga porojo kwenye kijiwe cha kahawa na kufungua na kupitia mafaili na ma documents kibao tena ya kimombo [emoji12][emoji12][emoji12]
 
Yani nishati ilikuwa na shida kuliko wizara ya Tozo?

Basi ngoja tusubiri aseeee
 
Haiwezekani wateja kulipia 27 elfu kuunganishwa ? mbona hata bure inawezekana ? Ukizingatia mita na nguzo ni mali yao na kuunganishwa watu wanapata faida zaidi ya watumiaji unadhani baada ya Bwawa la Nyerere kumwaga hizo megawatt tutazipeleka wapi ?
Iyo miundombinu ya umeme ni Mali ya Mteja kupelekea isiwezekane?
Tumia akili kidogo
 
Ushuzi kwakua nimesema Jk alikuwa mwizi pia?

Kama utatumia hata robo ya akili zako ndogo ulizonazo, hauwezi kuupima utofauti wa JK na JPM katika sekta ya wizi.Watofautishe kwa mengine ila kwenye swala la wizi hawana utofauti, tena bora hata JPM aliiba kijanja.
Ni kweli kabisa hata ule uwanja wa ndege kule kijijini kwao aliujenga kijanja [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Pongezi kwa wateule wote,

mara baada ya kiapo wanapaswa wachape kazi kwa speed na weledi.

Watanzania wengi tunapenda kuona Watendaji wanafuatilia miradi ya serikali kwa karibu.

hatupendi kuona viongozi wanakaa ofisini tu.

Mfano, Prof: Mbarawa ni mfuatiliaji mzuri ila sio mkali hivyo ili afanikiwe ni lazima awe mkali pale inapo bidi.

Makamba ni mfuatiliaji mzuri ila apunguze ushikaji kazini apige kazi, nishati ni nguzo ya uchumi wa Taifa.

Kijaji ni mpambanaji mzuri sana pia ni mkali hapendi masihara awapo kazini.

Mama Tax ni mweledi tunategemea maboresho mazuri zaidi.
 
Hata mimi imenishangaza hii mkuu! Hadi mtu anamaliza kipindi chake huko nje, anarudi tu anabandikwa ubunge na uwaziri hapo hapo baada ya kuapa ubunge!!!! CCM wajitafakari! Kundi lote hilo hakuna mbadala wa Marehemu Kwandikwa?
Ndiyo maana watu wanadai katiba mpya ili kuondoa hii dhana ya eti lazima waziri awe mbunge.
 
Japo alikuwa na mapungufu yake late Legendary Pombe alikuwa kiboko na alifaa kwa haya madudu yanayojirudia.
Unakumbuka hata yeye alikuwa anawafukuza halafu baada ya muda anawarudisha tena kwenye uwaziri?
 
What is insanity?

Insanity is doing the same thing over and over again and expecting a different result.

Uteuzi uliofanywa na Madam SSH ni sawa na insanity. Mawaziri wanatenguliwa leo baada ya muda wanateuliwa tena. Mchezo unajirudia hivyo hivyo miaka nenda miaka rudi, halafu tunategemea kupata matokeo chanya?

Hivi hakuna watu wapya kabisa wa kushika hizo nyazfa?

Pathetic nation!!
 
Mini grid ndio nini ? Vyanzo vya uzslishaji vya Tanesco vinazalisha uneme mwingi kuliko tunao utumia.

Uzalishaji uko karibu 2000MW na matumizi yapo karibu 1600MW, tatizo ni usambazaji.
Miundo mbinu ya usambazaji ni hafifu na mingine imechoka mbali ya kutokidhi mahitaji ya wakati huu.
Kama hujui mini grid bro naona hatuna haja ya kujadili zaidi. Website ya Tanesco inaonesha uzalishaji ni MW 1601, hatujafika kwenye MW 2000 bado.
 
Rais Samia Suluhu kafanya mabadiliko madogo kwenye baraza la Mawaziri na mwanasheria mkuu wa Serikali kama ifuatavyo
  1. Rais Samia Suluhu amemteua Dkt. Stergomena Tax kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, anachukua nafasi ya marehemu Elias Kwandikwa
  2. Dkt. Ashatu Kijaji ameteuliwa kuwa waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari kuchukua nafasi ya Dkt. Faustine Ndugulile ambae uteuzi wake umetenguliwa
  3. January Makamba anachukua nafasi ya Merdard Kalemani wizara ya Nishati
  4. Makame Mbarawa anachukua nafasi ya Chamuriho wizara ya ujenzi na uchukuzi
  5. Dkt. Feleshi anachukua nafasi ya Kilangi kuwa Mwanasheria mkuu wa Serikali


Sina sababu lakini Nilikuwa namuona kalemeani ni mtu asiefaa, hapo rais amefanya sawa kumfuta kazi, lakini kwa Feleshi amekosa saana, feleshi ni mtu asiyefaa kwa nafasi hiyo nyeti.
 
Ni kweli kabisa hata ule uwanja wa ndege kule kijijini kwao aliujenga kijanja [emoji23][emoji23][emoji23]
Nafikiri tumeelewana Sasa, ndio aliujenga kijanja kwasababu kuna baadhi ya vitu vilitungiwa kabisa sheria na binge likapitisha, kwahiyo hata kama baadae vilikuja kuonekana na dosari bado havikuzua mijadala ya muda mrefu, ingawa kiuhalisia ulikuwa ni upigaji.

Ukilinganisha kashfa za Escrow na Richmond zinaweza kuonekana kuwa ni kubwa kuliko issue ya uwanja wa ndege kwasababu issue ya uwanja ilipigwa kijanja.

Kwahiyo kwenye swala la wizi huwezi kumtetea JK kisha ukamshtumu JPM, unless utangulize mahaba, kitu ambacho sio kizuri kwa mtoto wa kiume.
 
Back
Top Bottom