Uteuzi Julai 2, 2024: Kidata aondolewa TRA, Jafo na Ashatu wabadilishana Wizara

Serikalini siku hizi hakuna siri, yaani inapangwa jambo linatangazwa kabisa na kweli linatokea.

Niliona hadi watu wa ajabu ajabu kule twitter wanasema kidata aondoke kweli kaondolewa.

Rais samia kuna watu wanampangia nani awe nani na yeye anafuata tu.
 
Kwamba Rais wa Muungano anaweza mteua mteule wa Rais wa Zanzibar? Hii imekaaje?
 
Bw. Yusuph Juma Mwenda ameteuliwa kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mwenda alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA).
Wametupa ajenda nyingine tena ya kwenda nayo siku mbili tatu hizi ikiandaliwa nyingine!
 
Kwa msilolijua Yusuph Mwenda alikuwa ni mtumishi wa Tra hadi mwaka juzi alipoteuliwa na Rais Mwinyi kwenda zanzibar kuwa kamishna Mkuu wa ZRA
Yusuph Mwenda ni mbara na aliwahi kuwa Meya wa Kinondoni kabla ya Boniface Jacob kabla ya kuvunjwa Manispaa ya Kinondoni na kuanzishwa ya Ubungo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…