Uteuzi Julai 2, 2024: Kidata aondolewa TRA, Jafo na Ashatu wabadilishana Wizara

Uteuzi Julai 2, 2024: Kidata aondolewa TRA, Jafo na Ashatu wabadilishana Wizara

Serikalini siku hizi hakuna siri, yaani inapangwa jambo linatangazwa kabisa na kweli linatokea.

Niliona hadi watu wa ajabu ajabu kule twitter wanasema kidata aondoke kweli kaondolewa.

Rais samia kuna watu wanampangia nani awe nani na yeye anafuata tu.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa illyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-

Mhe. Dkt. Selemani Said Jafo (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Dkt. Jafo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Mhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira). Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Dkt. Kijaji alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.


Mhandisi Yahya Ismail Samamba ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara va Madini. Kabla ya uteuzi huu, Mhandisi Samamba alikuwa Katibu Mendaji wa Tume ya Madini. Mhandisi Samamba anachukua nafasi ya Bw. Kheri Abdul Mahimbali ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Bw. Yusuph Juma Mwenda ameteuliwa kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mwenda alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA).

Bw. Alphayo Japan Kidata ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais, Ofisi ya Rais - Ikulu. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Kidata alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)


Kwamba Rais wa Muungano anaweza mteua mteule wa Rais wa Zanzibar? Hii imekaaje?
 
Bw. Yusuph Juma Mwenda ameteuliwa kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mwenda alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA).
Wametupa ajenda nyingine tena ya kwenda nayo siku mbili tatu hizi ikiandaliwa nyingine!
 
Kwa msilolijua Yusuph Mwenda alikuwa ni mtumishi wa Tra hadi mwaka juzi alipoteuliwa na Rais Mwinyi kwenda zanzibar kuwa kamishna Mkuu wa ZRA
Yusuph Mwenda ni mbara na aliwahi kuwa Meya wa Kinondoni kabla ya Boniface Jacob kabla ya kuvunjwa Manispaa ya Kinondoni na kuanzishwa ya Ubungo.
 
Back
Top Bottom