Uteuzi na Uhamisho: Rais Samia amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali

Mkuu unaelezea vizuri nakubali ila ukipewa hicho kiti hata wewe hutatenda jinsi unavyoelezea unajikuta tu umebadilika hata wewe unabaki kushangaa. Tatizo ni mfumo na huu mfumo unatakiwa ufumuliwe kama carpet bomb ya Hiroshima ama kama gharika ya Nuhu. Wabaki tu watoto wachache wawekwe kwenye maabara maalum chini ya uangalizi wa karibu wa mjerumani wakichunguzwa na kutafiti bongo zao huku wakikua wanapokea mkong'oto mkali na wa haja kila siku hadi wawe watu wazima waweze kujitawala vizuri.
 
Shida ni uzembe hiyo mifumo yote ya usimamizi waliyonayo waongeze mifumo ipi tena.

Wanamfumo mzuri sana wa appraisal serikalini ukitaka kulijua hilo sikiliza watu wanaitwa wakurugenzi wizarani au wanaoshika technical position za mashirika yao (wakurugenzi wa vitengo). Wanafahamu kinaga ubaga how to implement strategies za maeneo yao, admin regulations/laws za kuzingatia kwenye maamuzi na mambo mengine yote ya managerial za sector zao; from the decision to implantation on the ground.

Hata report ya CAG inaelezea kila kitu sio wizi tu hata risks zinazohatarisha upotefu wa hela ni watu kutoheshimu taratibu za kufanya mambo kwa mifumo iliyopo ya matumizi au uelewa mdogo wa kiongozi kusimamia wengine.

Kwa hivyo issue sio mfumo kabisa, ni usimamizi wa juu. Shida inaanza badala ya ku-promote wakurugenzi kwenda kuwa makatibu wakuu wanaenda kuokota watu ambao hawana strategic knowledge na kuwapa hayo majukumu. Badala ya kuacha watu huko kwenye wilaya kwa muda wanawatoa kila siku; jumlisha na watu kutochukuliwa hatua za kinidhamu. Hiyo ndio shida sio mfumo, hiyo ipo tele.
 
Wale wanaolalamikaga udini huwezi kuwaona wakilalamika hapa
 
Hili swala la teuzi za mara kwa mara na kuhamisha Watendaji ni huo linanikera na huwa nachukuria ni sehemu mojawapo ya matumizi mabaya ya Kodi zetu. Unapo muhamisha Mtendaji kuna gharama za kasafiri yeye mhusika.... Familia (mke na watoto)... Fedha ya usumbufu.... Hii gharama yote serikalini inalipa kupitia Kodi zetu. Hii mifumo yetu inashida sana
 
Nikumbuke basi na mimi bi Mkubwa,nikakusaidie kuhamasisha shughuli za Maendeleo,hasa Kilimo,Tanganyika or Namanyere DC
 
Mara ya mwisho kuangalia kuhusu kodi niliambiwa nimpe Kaisari yaliyo yake.Maana yake ukishalipa kodi inakuwa si yako wewe mlipaji bali ya aliyeipokea.Hata matumizi hapangiwi.
 
PANGA PANGUA KILA SIKU AJIRA HIZI ZITANGAZWE WATU WAOMBE KWA SIFA SIO UCCM
 
Tz wanabadilishana kwa maslahi yao tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…