Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
La tatu K utajuaje umuhimu wa Rotation kwny OrganisationWeziwezi wote wafukuzwe.Hii panga pangua haijawahi kuleta maendeleo yoyote.
We ni kada?Nikumbuke basi na mimi bi Mkubwa,nikakusaidie kuhamasisha shughuli za Maendeleo,hasa Kilimo,Tanganyika or Namanyere DC
Labda akaoge maji ya Bahari.mwendo wa kupanga na kupangua.
vipi Lucas mwashambwa hajakumbukwa?
Kanuni ni moja, unasifia hata akijamba. Unatetea hoja yeyote.Kazi za kuteuliwa ni mtihani sana ,anytime unarudishwa kijijini.
Mimi nadhani inatakiwa kuwa na mkeka kikatiba kwamba boya yeyote akizingua ktk teuzi, akitumia nguvu ya umma vibaya, afilisiwe then 10years in prison, maximum security maana hao ni public enemy..Kipi bora uwe mkali kuwasimamia ili kuwe na consistent ya utendaji huko walipo, na mtu akiboronga anakaa chonjo.
Au uamishe amishe kila siku watu na kukosekana consistency, siku troubleshooter anaenda huko mkurugenzi sijui mkuu wa wilaya anamwambia yeye mgeni hayajui hayo matatizo vizuri.
Serikali inatakiwa kuwa consistent kwenye civil services, matatizo ya babati, hayawezi fanana na Geita, Ifakara, Nachingwea, wala Kigamboni.
Kila sehemu ina unique core challenges zake, kuondoa wahusika na kupeleka wapya kila mara na iwapo kila mtu ana different approach ya kutatua tatizo hilo hilo ndio msingi wa kukuta kero ya eneo moja inadumu kwa miaka 10 hakuna consistency kwenye kulitatua.
Shida ya africa sio wazungu, ni sisi wenyewe.
ipi bora uwe mkali kuwasimamia ili kuwe na consistent ya utendaji huko walipo, na mtu akiboronga anakaa chonjo.
Au uamishe amishe kila siku watu na kukosekana consistency, siku troubleshooter anaenda huko mkurugenzi sijui mkuu wa wilaya anamwambia yeye mgeni hayajui hayo matatizo vizuri.
Serikali inatakiwa kuwa consistent kwenye civil services, matatizo ya babati, hayawezi fanana na Geita, Ifakara, Nachingwea, wala Kigamboni.
Kila sehemu ina unique core challenges zake, kuondoa wahusika na kupeleka wapya kila mara na iwapo kila mtu ana different approach ya kutatua tatizo hilo hilo ndio msingi wa kukuta kero ya eneo moja inadumu kwa miaka 10 hakuna consistency kwenye kulitatua.
Shida ya africa sio wazungu, ni sisi wenyewe.
Sanasana ni hasara tu fikiria hao wote watalipwa kiasi gani kama gharama za uhamisho nkWeziwezi wote wafukuzwe.Hii panga pangua haijawahi kuleta maendeleo yoyote.
Unaenda tu kulima nyanya 🤣Kazi za kuteuliwa ni mtihani sana ,anytime unarudishwa kijijini.
Ili iwe nini!??🤷🤷 🚮🚮11 March 2024
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu usiku huu:
Picha maktaba: ndugu Anamringi Macha
TEUZI NA UHAMISHO :
---
- Naibu Katibu Mkuu wa CCM bara, ndugu Anamringi Macha ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga
- Christina Mndeme kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano (Mazingira) kabla ya hapo alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi kama ifuatavyo:
i. Amemteua Bw. Anamringi Macha kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Kabla ya uteuzi Bw. Macha alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
ii. Amemteua Bi. Christina Mndeme kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira). Kabla ya uteuzi, Bi. Mndeme alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
iii. Amemteua Bw. Japahari Kubecha Mghamba kuwa Mkuu wa Wilaya ya Lushoto. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mghamba alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Busega.
iv. Amemteua Bw. Mussa Kilakala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Pangani. Kabla ya uteuzi huu Bw. Kilakala alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kaliua.
V. Amemteua Bw. Robert Masunya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Kabla ya uteuzi huu Bw. Masunya alikuwa Afisa Mwandamizi katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Waanawake na Makundi Maalum.
vi. Amemteua Bi. Mwashabani Mrope kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
vii. Amemteua Bw. Jacob Simon Nkwera kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Nkwera alikuwa Afisa Mwandamizi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.
viii. Amemteua Bw. Sangai Mambai kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Busega.
ix. Amemteua Bw. Raymond Mweli kuwa Katibu tawala wa Wilaya ya Kaliua.
X. Amemhamisha Bw. Frederick Damas Dagamiko kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga.
xi. Amemhamisha Bw. Bashir Muhoja kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
xii. Amemhamisha Bw. Tito Philemon Mganwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.
Uapisho wa Wakuu wa Mikoa na Naibu Katibu Mkuu utafanyika tarehe 13 Machi, 2024 saa 04.00 asubuhi, Ikulu Dar es Salaam.
View attachment 2932257View attachment 2932258