Nehemia Kilave
JF-Expert Member
- Jan 9, 2022
- 1,414
- 3,118
Vizuri
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hamna chochote, hapo Bado mmoja hamalizi huu mwaka MWIGULU MCHEMBAKwa tenguzi hizi mbili, naona mwisho mbaya wa Mh. Samia 2025
Yes, kajigeuza Mwenyekiti wa Mabaraza ya ArdhiJerry silaa asingetolewa huko wizara ya ardhi alikua anaenda kuharibu mambo siku siyo nyingi
Una hakika wamewekwa benchi?Hatimaye wataalamu wa magoli ya mkono na offside wamewekwa benchi.
Mambo ni motooo ndani ya CCM.
Urais 2025 kutawaka moto.
Hio inafahamika toka zama za "Hii nchi itapigwa mnada" msamaha huwa haubadilishi status ya kuzingua🤣Kuomba omba msamaha
Nadhani Jerry Slaa alikuwa amefiti sana kwenye hiyo Wizara yenye migogoro na lawama.Jerry silaa asingetolewa huko wizara ya ardhi alikua anaenda kuharibu mambo siku siyo nyingi
Saga kunguni 😂😂Mama Samia Fukuza Mwigulu hivi mtu kama yule anakuaje waziri wa fedha??
Kwa mwendazake wengi tulifurahi maana alikuwa anakwenda kuingiza nchi kwenye machafuko nyang'au yule kama si Mungu kuingilia katiNilianza kumuona Nape wa ajabu pale aliposemaga Mungu ameamua ugomvi kati yake na JPM..Kwa maana nyingine alifurahia kifo Cha mwenzie...Kiongozi wa public unatamka maneno kama haya kweli????....kule Kanda ya Ziwa walikuwa wanasubiri siku itafika ya Mungu kuonyesha haki ilipo..
Yani ni kama uongozi wa wizara ya mambo ya nje umeondolewa wote. Something fishy was going on maybe. Balozi labda akaona ajitenge kutoka hapo...au inawezekana alikuw na taarifa / ni "watu wale" wa upande wa mama, naona atapangiwa kazi nyingine.Seems to me Wizara ya Mambo ya Nje, Pamoja na Nape walikuwa wanaplot something against Samia, Bybato was too Young to ruin his political carrier.
Message ya Nape kuwa "We can make you win" ilikuwa ina maanisha any one including Rais ana obligation ya kumuheshimu Nape ili apate nafasi
Esther Luxury?Yule jamaa much know one time alijimix akasema hata kama unamchukia au umempita akili boss usimuoneshe, ukisoma Cuba akili inakwambia huyu anambeza boss kubwa keshaota mapembe!!
Yule mwingine akamwaga mchele kitaa kuwa tunafunga tu maana refa wetu haina haja kuhesabu kura!! Cha Arusha kilipanda kichwani.
Binafsi nampongeza sana Bimkubwa ila bado kijana mmoja sijui kaponaje, hawa watatu and company wanautafuta ufalme kwa nguvu zote na hawamfai Bimkubwa kwenye safari yake!!
Dawa asafishe wote ataongoza kwa amani, mitano tena!!
Kweli kabisa...watu wengi wamepata haki zao chini ya Jerry.Nadhani Jerry Slaa alikuwa amefiti sana kwenye hiyo Wizara yenye migogoro na lawama.
Makamba mutoto wa mama vipi tena?My Take
Cheo ni dhamana, maisha yaendelee 🙏🙏👇👇
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi, utenguzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt, Moses Kasiluka, viongozi hao ni kama ifuatavyo;-
- Mhe. Jerry William Silaa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Silaa alikuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, anachukua nafasi ya Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
- Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Ndejembi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu);
- Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu). Kabla ya uteuzi huu Mhe. Kikwete alikuwa Naibu Waziri, Odisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;
- Balozi Mahmoud ThabitKombo ameteuliwa kuwa Mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kabla ya uteuzi huu Balozi Kombo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italy, anachukua nafasi ya Mhe. January Makamba (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
- Mhe. Cosato Dvid Chumi (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiki. Mhe. Chumi anachukua nafasi ya Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye atapangiwa kituo cha kazi;
- Mhe. Deus Clement Sangu (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;
- Mhe. Dennis Lazaro Londo (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki. Mhe. Londo anachukua nafasi ya Mhe. Stephen Lujwahuka Byabato (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
- Bw. Eliakim Chacha Maswi ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria. Kabla ya uteuzi huu Bw. Maswi alikuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA);
- Bi Mary Gasper Makondo ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma. Kabla ya uteuzi huu Bi. Makondo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria. Bi. Makondo anachukua nafasi ya Bi. Rehema Sefu ambaye amestaafu.
- Bw. Kiseo Yusuph Nzowa ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro. Kabla ya uteuzi huu Bw. Nzowa alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikuli;
- Bw. Musa Haji Ali ameteuliwa kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu Bw. Ali alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu;
- Bw. Louis Peter Bura ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato. Bw. Bura anachukua nafasi ya Bw. Said Juma Nkumba ambaye amepangiwa majukumu mengine;
- Bi. Kemirembe Rose Lwota amehamishwa kutoka Wilaya ya Manyoni kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti;
- Dkt. Vincent Biyegela Mashinji amehamishwa kutoka Wilaya ya Serengeti kuwa Mkuu wa Wilaya Manyoni;
- Dkt. Maulid Sleiman Madeni ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti;
- Bw. Afraha Nassoro Hassan amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Seringeti kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi. Bw. Hassan anachukua nafasi ya Bw. William Anyitike Mwakalambile ambaye uteuzi wake umetenguliwa na;
- Bw. Dennis Kwame Simba ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA). Kabla ya uteuzi huu Bw. Simba alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).
Rais ana idadi maalum ya kuteua Wabunge na alishamaliza idadi hiyo alipoteua Mbunge kwa mara ya mwisho.Duuuh
Wazee wa Goli la Mkono wamewekwa kando.
Najiuliza, kulikuwa na ulazima wowote wa kumstaafisha Mbunge ili kumteua mwingine?
Tunajua Waziri si mtendaji Mkuu wa wizara. Hivyo, ingelikuwa vema yule anayeonekana kufaa angepelekwa kuwa Katibu Mkuu wa wizara husika.