Pre GE2025 Uteuzi na Utenguzi: Nape, January na Byabato out! Jerry Silaa ahamishiwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Absolute power corrupts absolutely. Huyu nape hapana, kijana mdogo lakini anajiamini kijinga kweli.
 
TH

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaondoa katika nafasi za uwaziri, mawaziri wake wawili waandamizi; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye. Pia amemuondoa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Stephen Byabato.

Nape na Byabato wameondolewa ikiwa ni chini ya wiki moja tangu Nape anukuliwe akisema angemsaidia Byabato ambaye ni mbunge wa Bukoba Mjini, kaskazini magharibi mwa Tanzania kushinda ubunge katika uchaguzi wa 2025 kwa sababu anafahamu mbinu za uchaguzi na kwamba matokeo ya uchaguzi hayategemei ‘box’ (sanduku la kura) bali yanategemea nani anasimamamia uchaguzi na kuhesabu kura.

Kauli hiyo ilikosolewa na kupingwa katika majukwaa mbalimbali yakiwemo ya mitandao ya kijamii kwa tuhuma za kukiuka misingi ya demokrasia ya uchaguzi na kuheshimu uamuzi wa wapiga kura. Hata hivyo, Nape aliomba radhi kwa kauli yake hiyo huku akisema huo ulikuwa ni utani uliodumu kwa miaka tisa tangu atoe kauli nyingine tata kwamba chama tawala CCM kingeshinda uchaguzi wa 2015 hata kupitia bao la mkono.
Nafasi ya Nape inachukuliwa na Jerry Slaa aliyehamishwa kutoka Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, wakati nafasi ya Byabato itakaliwa na mbunge wa Mikumi Dennis Londo.

Pia kuan Naibu Waziri mpya mwingine wa Mambo ya Nje, mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi, anayechukua nafasi ya balozi Mbarouk Nassor Mabarouk aliyetangaza mapema Jumapili kujiuzulu lakini taarifa ya Ikulu imesema atapangwa kituo cha kazi.

TH

Maelezo ya picha,Bado hakuna sababu za dhahiri za kuondolewa kwa Waziri wa Mambo ya Nje
Bado hakuna sababu za dhahiri za kuondolewa kwa Waziri wa Mambo ya Nje, Makamba ambaye amewahi pia kuwa Waziri wa Muungano na Mazingira, pia Waziri wa Nishati. Nafasi ya Makamba sasa inachukuliwa na Mahmoud Thabiti Kombo aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Italia.

Katika mabadiliko hayo, Waziri mpya wa Ardhi na Makazi ni Deogratius Ndejembi ambaye awali alikuwa Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu.

Aliyekuwa naibu waziri wa menejimenti ya Utumishi wa Umma, Ridhiwani Kikwete sasa anakuwa waziri kamili wa Kazi. Ridhiwani ni mtoto wa Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete.

Nafasi ya naibu waziri iliyoachwa wazi na Ridhiwani inajazwa na Deus Clement Sangu. Kadhalika kuna uuteuzi na mabadiliko ya nafasi nyingine kwa adhi ya makatibu wakuu, wakuu wa wilaya, makatibu tawala wa mikoa na taasisi za umma.

Kwa mara nyingine, Rais Samia amewaondoa maafisa waandamzi kadhaa katika ofisi ya rais Ikulu na kuwapangia majukumu mengine. chanzo. BBC
 
Mzee hana namna nyingine, atasema nini tofauti na hicho? kilichobaki sasa ni kuwa chawa haswa wa mama ili mwanae afikiriwe upya.

Inabidi aanze tena zile sarakasi zake za wazuri hawafi, maana alikuwa kimya kwa muda.
 
Hahaha wazee kama hawa wanatakiwa wakae kimya kama mzee Pinda yule jamaa namkubali sana hana makubwa yuko huko anapambana na maisha yake..sasa njoo ukutane na wazee wa hovyo wasio kubali kupitwa yaan wao ni full kisebe sebengo 🤣🤣🤣
 
Pigo la pili kwa January Makamba na Nape Nnauye kwa Marais wawili tofauti Ni wao kujiona special toka enzi za CCJ.

Wadau kwa mtizamo na jicho la kitafiti mtakubaliana nami kuwa January Makamba na Nape Nnauye Wana Maisha ya kujiona special toka enzi na enzi, ukitizama historia Yao hata ya Elimu Ni Ukweli woote wawili wameunga unga tu kwa sababu wametoka familiar bora, anzia January Makamba kigonsera zero brain kabisa Ila pesa ikamng'arisha hadi nje, rudi kwa Nape kuanzia chini hadi anasoma INDIA.
Vuta kumbukumbu Ben Saanane kabla ya kupotea alikuwa Anasema yeye alisoma na Nape Nnauye INDIA japo vyuo tofauti Lakini uwezo wa Nape Nnauye ulikuwa mdogo kwa wanafunzi kutoka Afrika, sema akiwa INDIA alikuwa na pesa chafu za nyumbani na alikuwa mtu wa kujiona, special, kujisikia na kuona yeye ndo kila kitu.

Pigo la Nape na January Makamba Ni kujisikia na kujiona special na kuona wanaweza kufanya Chochote na ndo Maana hata historia ya vuguvugu la uhasi Ndani ya CCM Kipindi cha CCJ huwakosi watu hao, Lakini ukitizama Nape Nnauye Kuanzia akiwa Waziri wa Habari yeye alikuwa Ni mtu wa mgeni rasmi, kuzindua makongamano, Mara seminar Yaani Ni sanaa, Utapeli, suti nk na ndo Maana kila akitumbuliwa na Kuanzia JPM mpka SSM alikuwa ukumbini mgeni rasmi.

Mwisho January Makamba na Nape Nnauye Ni Viongozi wa kujikweza na Wana uwezo mdogo Katika utendaji wao, angalieni wizara zoote waliopita walishindwa kudeliver kwa ajili ya nchi bali walijitengenezea kesho yao nzuri na wapambe wao.
 
Attachments

  • FB_IMG_1723939082702.jpg
    FB_IMG_1723939082702.jpg
    51 KB · Views: 1
Kuna watu Wana maneno sijawahi ona.
Eti Kama kipara angeupata urais, waziri wake mkuu angekua ODDO na waziri wake wa Mambo ya nje angekua BUMUNDA.
Hiyo sijui ingekua serikali gani?
 
Kama usingizi ulikata ungesokota kamba za raba zako ulewe upate usingizi tena, hoja yako ya maana iliyokufanya uandike Post hii ni ipi! Nilichokisoma ni cha kawaida na kimeandikwa mara kadhaa na watu tofauti tofauti.
 
Hawajajikuza/kujikweza bali wamedekezwa,kubebwa,kugawiwa nafasi na kuachwa wajitawale na kujisahau.Lakini ndiyo hivyo.Kufeli shule si lazima ufeli na maisha.
 
Kuna watu Wana maneno sijawahi ona.
Eti Kama kipara angeupata urais, waziri wake mkuu angekua ODDO na waziri wake wa Mambo ya nje angekua BUMUNDA.
Hiyo sijui ingekua serikali gani?
Kipara 'Marope' asahau uraisi

Akitoka Samia S. Hassan ni zamu ya raisi mkristo
 
Pigo la pili kwa January Makamba na Nape Nnauye kwa Marais wawili tofauti Ni wao kujiona special toka enzi za CCJ.

Wadau kwa mtizamo na jicho la kitafiti mtakubaliana nami kuwa January Makamba na Nape Nnauye Wana Maisha ya kujiona special toka enzi na enzi, ukitizama historia Yao hata ya Elimu Ni Ukweli woote wawili wameunga unga tu kwa sababu wametoka familiar bora, anzia January Makamba kigonsera zero brain kabisa Ila pesa ikamng'arisha hadi nje, rudi kwa Nape kuanzia chini hadi anasoma INDIA.
Vuta kumbukumbu Ben Saanane kabla ya kupotea alikuwa Anasema yeye alisoma na Nape Nnauye INDIA japo vyuo tofauti Lakini uwezo wa Nape Nnauye ulikuwa mdogo kwa wanafunzi kutoka Afrika, sema akiwa INDIA alikuwa na pesa chafu za nyumbani na alikuwa mtu wa kujiona, special, kujisikia na kuona yeye ndo kila kitu.

Pigo la Nape na January Makamba Ni kujisikia na kujiona special na kuona wanaweza kufanya Chochote na ndo Maana hata historia ya vuguvugu la uhasi Ndani ya CCM Kipindi cha CCJ huwakosi watu hao, Lakini ukitizama Nape Nnauye Kuanzia akiwa Waziri wa Habari yeye alikuwa Ni mtu wa mgeni rasmi, kuzindua makongamano, Mara seminar Yaani Ni sanaa, Utapeli, suti nk na ndo Maana kila akitumbuliwa na Kuanzia JPM mpka SSM alikuwa ukumbini mgeni rasmi.

Mwisho January Makamba na Nape Nnauye Ni Viongozi wa kujikweza na Wana uwezo mdogo Katika utendaji wao, angalieni wizara zoote waliopita walishindwa kudeliver kwa ajili ya nchi bali walijitengenezea kesho yao nzuri na wapambe wao.
Usifurahie sana Mama yenu hatabiriki kesho utashangaa wamerudi mezani wanakula vinono.
 
Back
Top Bottom