Pre GE2025 Uteuzi na Utenguzi unaofanywa na Samia ni mbwembwe tu za Madaraka

Pre GE2025 Uteuzi na Utenguzi unaofanywa na Samia ni mbwembwe tu za Madaraka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Unashindwa kutofautisha kati ya uwezo wa Samia na kazi za Serikali zinazoendelea kwa sababu ya uchawa!

Kazi zinazoendelea si kwa sababu ya Samia hata asingekuwepo kazi hizo zingefanyika!

Kwa ujinga na uchawa wako unadhani zinafanyika kwa sababu ya Samia!

Hoja iliyopo hapa ni uwezo wa Samia kusimamia watu wake aliyowateua mwenyewe! Hana uwezo, anawahofia na anawaogopa hivyo silaha aliyobaki nayo ni kuwateua na kuwatengua ili mradi awajaze hofu washindwe kutekekeza majukumu yao!

Kwako hilo unalishangilia bila tafakuri kwa sababu ya uchawa!
Punguza jazba kwenye maongezi, unapotumia neno chawa zaidi ya mara moja ni kielelezo cha kutokwa mapovu.

JPM na sifa zote alizopewa alishindwa pia kuwasimamia hao wasaidizi wake akaishia kuwasimamisha kazi miaka mingi huku wakiendelea kulipwa mishahara.

Pia SSH anao upinzani kutoka kwa Nape, Makamba, Ummy na watu wengine walio nyuma ya hao. Anachukiwa lakini miradi yote inaendelea kumalizika.

Hatuongozwi na malaika tunachagua binadamu wenzetu wenye miili ya damu na nyama.
 
Ndiyo sababu tunakwambia wewe mpumbavu!
 
Wewe huna hoja una viroja! Hivyo viroja vyako ndiyo vinajibiwa!
Jikite kwenye hoja kaka. Hamza ni machine kubwa na hatimaye Samia kaamua kutenda haki. Alibaniwa awamu ya nne kipindi cha Kikwete akaja JPM akampa ukurugenzi wa mamlaka ya anga, amekuja Samia kampandisha cheo na kwa sasa ni AG.
 
Faida za DPW zimeshaanza kuonekana katika wingi wa gawio linalokwenda hazina kuu ya Taifa wala haihitaji mpaka SSH arudi kwao Kizimkazi.
Wacha wewe... Yaani wawekezaji wamefika majuzi tu leo mshaanza kupokea magawio?
Mnaweza kuweka hizo ripoti hadharani?
 
Wacha wewe... Yaani wawekezaji wamefika majuzi tu leo mshaanza kupokea magawio?
Mnaweza kuweka hizo ripoti hadharani?
Mfuate waziri wa fedha ofisini kwake akupe takwimu zote mpya. Tulikuwa tunapoteza muda kufanya kazi kizamani na pia tuliacha mapengo mengi ya ufisadi kuwafaidisha wachache.
 
Mfuate waziri wa fedha ofisini kwake akupe takwimu zote mpya. Tulikuwa tunapoteza muda kufanya kazi kizamani na pia tuliacha mapengo mengi ya ufisadi kuwafaidisha wachache.
Sasa wewe ndo umetaja gawio ulipaswa ulete takwimu kujazia hoja yako
Otherwise wewe na bi Kizimkazi lenu moja!
Matapeli wahed!
 
Tumeona kila mara anateua na kutengua! Wale wale aliowatengua anawateua tena na kuwatengua tena. Kwa kiingereza ana recycle watu wake bila kuwapa elimu wala semina elekezi.

Anachofanya Samia ni kuonyesha nguvu na madaraka aliyonayo kikatiba. Madaraka na nguvu za Rais ndicho anaonyesha. Kama alivyowahi kusema yeye ni Rais mwenye jinsia ya kike! Kwa hiyo anaonyesha namna Rais wa jinsia ya kike anavyoweza kutelekeza madaraka na nguvu yake kama Rais wa kike! Anateua na kutengua kama anabadilisha mavazi.

Kuteua na kutengua anakofanya Samia si kwa lengo la kuongeza ufanisi serikalini au kuleta mabadiliko ya kiutendaji serikalini, bali kuonyesha nguvu na madaraka ya Rais mwanamke!

Badala ya teuzi na tengua zake kuleta maendeleo kwa Taifa zinaleta hasara na kudidimiza maendeleo ya nchi! Tangu aingie madarakani kwa kudra ya Mwenyezi Mungu teuzi na tengua zake zimegharimu Serikali mabilioni ya fedha ambazo zingeweza kujenga shule, zahanati, barabara na miradi kadha wa kadha!

Mungu ibariki Tanzania!

PIA SOMA
- News Alert: - Uteuzi Agosti 14, 2024: Rais Samia kafanya uteuzi, utenguzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali
Naungana na wewe baraza lake anacheza mlemle, badala ya kuchukua brain mpya zipo wizara hata kwa katiba hii sio za kuangalia eti yule ni mbunge wakati unavyo viti 10 vya kuweza mteua mtu makin na ukampa uwaziri ,sasa vile viti hufanywa kama zawadi tu, mfano unamchukua Jenister na kumpa uwaziri why usimteue Pro Janabi ubunge na kumpa uwaziri n.k
 
Nenda wizara ya fedha ni hapo karibu na ikulu sio unaishia kufokea watu humu jukwaani.
20240817_141050.jpg
 
Naungana na wewe baraza lake anacheza mlemle, badala ya kuchukua brain mpya zipo wizara hata kwa katiba hii sio za kuangalia eti yule ni mbunge wakati unavyo viti 10 vya kuweza mteua mtu makin na ukampa uwaziri ,sasa vile viti hufanywa kama zawadi tu, mfano unamchukua Jenister na kumpa uwaziri why usimteue Pro Janabi ubunge na kumpa uwaziri n.k
Teuzi na tenguzi ndani ya mfumo wa ccm haziangalii uwezo au mchango wa mtu. Kinachoangaliwa ni uwezo wa kuimba mapambio. Ukiteleza kidogo tu unaliwa kichwa!
 
FAKE NEWS. Na hiki ndicho watanzania tunachokiweza sana. Kuwa manabii wa majanga, watu wenye kupenda sana habari za kimbea ambazo hazina ushahidi wowote.

DP W pamoja na mamlaka zilizowapa hiyo nafasi ya kufanya biashara ni watu waliojipanga kabla ya kuanza hiyo biashara.
Kwa hiyo JF inatoaga fake news?
 
Hili la diplomats kulipwa mishahara mara mbili ya awali ni kweli? Kama ni kweli basi kweli kasheshe tunayo.
 
Kwa hiyo JF inatoaga fake news?
Lengo ni kutaka kuuchafua mradi ulioletwa na Rais Samia, JF inaweza kuandika chochote kile kwani inaongozwa na watu kama wewe na mimi.

Ndio tunachoweza kukifanya watanzania, kuchafua biashara za watu bila hata kujua wanazifanya vipi. Ni roho zile zile za nyoka anakuuma mguuni unaingiwa na sumu unakufa halafu yeye huyoo anaserereka kwenye majani akikimbia.
 
You are a bipolar.
 
Huu ndiyo mwanzo wangu wa kufikiri ulipoanzia! Kwani maana ya R nne ni kuteua na kutengua kila kukicha. Kwamba uwezo wake wa kutambua watendaji wazuri wanaomfaa umeishia kama mama anachagua nyanya sokoni? Kwamba hana kazi zaidi ya kuteua na kutengua?

Samia hafai!
Na mimi ninachokiona anafanya mambo ya kutengua na kuteua kila wakati ili kuwapumbaza wananchi wamuone kama anachapa kazi hali ya kuwa nchi imemvuruga kazi imemzidi hajui atokee wapi na aingilie wapi.
 
Back
Top Bottom