UTEUZI: Rais Samia Amteua Adam Charles Mihayo kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB)

UTEUZI: Rais Samia Amteua Adam Charles Mihayo kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB)

Hivi aliyekuwa Mkurugenzi pale ndugu 77 Moshingi katemwa au kastaafu ?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Bw. Adam Charles Mihayo kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB).

Bw. Mihayo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Afrika Tanzania.

Uteuzi huu umeanza tarehe 19 Novemba, 2023

View attachment 2820916
View attachment 2820919
Adam Mihayo, kijana cool tangu alipokuwa kuwa seminari mdogo ya Mt. PETRO MOROGORO (kichwani yupo vizuri kwa maana, Academically kuanzia 0 level alipasua hasa, kadhalika na A - level alipasua fresh likewise), pia hana makando kando ya kutisha, nadhani ni Chaguo/teuzi sahihi na ataenda kufanya vyema katika nafasi aliyoteuliwa.

I declare interest, I personally knew the guy kwani alikuwa mbele yangu Sekondari kwa madarasa kadhaa, so I hope the guy atatenda vyema. All the very best Kaka Mihayo.
 
Wasukuma ni wachapakazi sana alafu siyo wezi. Hongera Mihayo
Kama Mihayo ni mtenda kazi mzuri kongole kwake lakini siyo kweli kwamba watu wa kanda ile siyo wezi na akati huko ndiko akina JOKA la makengeza a.k.a mzee wa vijisent anakotokea
 
Mihayo ni wanyamwezi, wacha kudanganya watu humu. Tangu lini mnyamwezi ni Musukuma? Au ukishaona mtu ameteuliwa na Rais tayari ni Musukuma?! Hii siyo awamu 5
Wasukuma na wanyamwezi ni wale wale tu wote ni watanzania !!
Acheni hizo ! Makabila siku hizi yamebaki umuhimu wake ni kwenye matambiko tu ! 😅😅🙏🙏
 
Nadhani umeandika kwa mhemko, unaweza cheki performance ya NMB tena chini ya mwanamama Mtanzania then ndio uandike haya maneno yako ndugu.
Hiyo siyo ya serikali 100%. Serikali ni mwana hisa tu. Na kwa miaka mingi uongozi na nina hakika hata sasa hauko chini ya serikali. Hamna benki ya serikali ya maana hata moja.
 
Back
Top Bottom