Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan,mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali katika nafasi tofauti tofauti.
Katika kuonyesha kuwa halali wala kupumzika wala kupoteza muda ameweza kuwateua viongozi takribani sita katika nafsi mbalimbali usiku huu.
Ambapo katika uteuzi huo amemteua dkt Milanzi kuwa Naibu katibu Mtendaji , Tume ya mipango atakayeshughulikia mipango ya kitaifa.
Amemteua Pia Daktari Lorah Basolile Madete kuwa Naibu katibu Mtendaji, Tume ya Mipango anayeshughulikia masuala ya ubunifu wa Biashara.
Amemteua pia Dkt Linda Ezekiel kuwa Naibu Katibu Mkuu ,Tume ya Mipango anayeshughulikia masuala ya Menejimenti ya utendaji na Tathmini.
Chanzo cha taarifa yangu ni kutoka kwa Mkurungezi wa Mawasiliano ya Rais ikulu, Zuhura Yunusi,ambaye amesambaza taarifa hiyo kwa umma na vyombo vya habari.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa.mam ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.