Kwa
Ukiangalia list ya wateule wote 22 utagundua kwamba zaidi ya asilimia 80 ya wateule wote kwa nafasi za ujaji wametokea mahakama na baadhi kwenye ofisi za wanasheria wa serikali.
Lakini mahakama kuu inasikiliza mashauri yenye wigo mpana zaidi mfano land tribunal, commercial, labour, tax nk.
Ningetarajia ili kukuza specialization uteuzi ungefanyika pia kupitia tribunals ambazo rufaa huenda mahakama kuu mfano CMA for labour cases, land tribunals for land matters FCC for commercial matters, tax nk. Wafanya maamuzi kwenye vyombo hivyo ambao ndio wanaozijua kiueledi sheria husika ndio wangepaswa kuwa promoted kwenye nafasi za ujaji ili kujenga jurisprudence (specialization).
Kutokufanya hivyo ni kuendelea kutengeneza mazingira ya mahakama kuu na mahakama ya rufaa kutokufanya kazi kiueledi hadi kufikia kutoa maamuzi kinzani (kama ilivyo kwa maamuzi mengi ya kesi za kazi yanavyoamuliwa kinyume na msingi uliowekwa na sheria husika)
Mfano jaji mteule mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka kumi kwenye uanasheria serikalini aende kuamua rufaa za mashauri ya kazi inayotokea CMA ambako ni purely labour laws tena kwa sasa hivi isiyohusisha serikali hawezi kuwa sawa na ambaye angetoka CMA.
Aidha maamuzi hayo yanademoralize utendaji kazi wa hizi tribunals na kuondoa misingi ambayo sheria ilimaanisha na kutengeneza ustawi katika secta husika
Ni rai yangu kwamba kabla ya uteuzi wa majaji, kigezo kinachohusu, specialization, uzoefu kwenye specialization, uweledi kwenye specialization vingezingatiwa ili kupromote high court yenye wabobezi na kuondoa mazoea ya kila jaji anaweza kufanya kesi yoyote.
Pia nashauri hizi tribunals zitazamwe kwa jicho la kipekee, si tu katika uteuzi wa majaji bali pia kwenye mabadiliko na marekebisho ya sheria husika.
Naomba kuwasilisha