Kwenye miungano yote, kuna kitu kinaitwa the majority na minority, kwenye muungano wetu, bara ndio the majority Zanzibar ni the minority, tena siku hizi mna bahati, zamani sisi wenzenu kuingia Zanzibar ilikuwa ni unaingia kwa passport!. Mzanzibari ana haki zote za Mtanzania huku bara kama Mtanzania mwingine yeyote, ikiwemo ajira ndani ya serikali ya JMT, na kumiliki ardhi, lakini m-bara hatuna haki ajira SMZ wala kumiliki ardhi Zanzibar!, ingekuwa tuko huru, saa hizi Visiwa vile vingekuwa vimezama!.
P
Mkuu
Hoja hapa ni unafiki (hypocrisy) inayochochowe na akina OMO. Ni unafiki kwa sababu hizi
Wanalalamika mambo ya muungano kuongezwa, lakini wanataka 21% ya mambo yasiyo ya muungano
21% ya ajira za muungano ni ajira za Tanganyika nyingi kuliko za SMZ, hawasemi hili , unafiki
Mifano
Wazanzibar wanasema Mahakama kuu si suala la muungano na waliondoa kupitia marekebisho ya katiba 2010
Wazanzibar wakiteuliwa mahakama kuu Tanzania hutawasikia akina OMO wakisema hawataki tena si hivyo bali analalamika kutoteuliwa kwenye mambo wanayosema yameongezwa. Unafiki
HESLB waliondoa na kutengeneza ZHESLB. Jambo la kushangaza HESLB inadhamini Wazanzibar wengi kuliko ZHESL tena hawarudishi mikopo. Huwasikii akina OMO wakiwakataza Wazanazibar wasihcukue HESLB, unafiki
Wameondoa Bandari katika muungano, lakini wanateuliwa na kuajririwa mamlaka ya Bandari. Unafiki
Hawataki mambo yaliyoongezwa katika muungano lakini wanataka ajira 21% kutoka Tamisemi na taasisi zisizo za muungano. Huu kama si unafiki sijui ni kitu gani.
Wakaondoa mafuta na gesi katika mambo ya muungano lakini leo wanapata 4% ya pato la Tanganyika kupitia mafuta, gesi, madini, kilimo, ufugaji na uvuvi. Huwezi kuwasikia wakisema hawapokei! unafiki
Huwezi kulaani mambo kuongezwa halafu unataka unufaike na mambo hayo hayo unayosema ni haramu
''HUWEZI KUSEMA NGURUWE NI HARAMU LAKINI MCHUZI WAKE NI HALALI''