Mkuu, msajili wa mahakama huwa ana majukumu ya kiutawala kuhakikisha shughuli zinaenda vyema mahakamani. Kuhusu kupractice, msajili na manaibu wasajili hawa ndio wanaosikiliza kesi za maombi ya gharama (bill of cost au taxation case), wanasikiliza maombi ya kukaza hukumu (utekelezaji wa hukumu) iliyotolewa na mahakama kupitia Jaji, wanaahirisha kesi pale Jaji asipokuwepo mahakamani nk.
Kesi za maombi ya gharama za kesi na hata za ukazaji wa hukumu ni kesi kama kesi nyingine, msajili husikiliza pande zote mbili, huchambua maelezo yao na uamuzi wake hutoka kwa mtoaji kuweka authorities nk, hivyo ni lazima afanye research.
Ondoa shaka kuhusu weledi wa naibu wasajili, weka shaka kwa Malata kuwa jaji - huyu amepotosha (misled) sana mahakama ili tu ashinde kesi. Mawakili wa serikali wengi wapo kwa ajili ya kushinda kesi na sio kwa ajili ya kuhakikisha haki inapatikana, watafanya chochote kile ili tu wapate ushindi.