Uteuzi Septemba 16, 2024: Rais Samia afanya uteuzi wa viongozi akiwemo Katibu wa Bunge

Uteuzi Septemba 16, 2024: Rais Samia afanya uteuzi wa viongozi akiwemo Katibu wa Bunge

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:

(i) Bi. Nenelwa Mwihambi ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Kabla ya uteuzi huu, Bi. Mwihambi alikuwa Katibu wa Bunge; na

(ii) Bw. Baraka Ildephonce Leonard ameteuliwa kuwa Katibu wa Bunge. Bw. Leonard anachukua nafasi ya Bi. Mwihambi ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Viongozi walioteuliwa wataapishwa tarehe 19 Septemba, 2024 saa 09.00 alasiri, Ikulu - Dar es Salaam.

1726506900264.jpeg
PIA SOMA
- Uteuzi Agosti 6, 2024: Rais Samia afanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi mbalimbali
 
Mwandishi kateleza, nampatia pole. Huwezi ukasema viongozi mbalimbali ikhali ni watu wawili tu walioteuliwa. Namuomba ajitahidi kuona namna bora ya kuandika maana si mara ya kwanza dada yetu anateleza. Dada atambue yeye ni kioo cha jamii.
 
Habari mbaya sn Hii kw bitulia
maana chuki alikua nayo Kwa yule dada bila shaka alitegemea demotion
 
Uliposema viongozi mbalimbali nikajuwa ni wengi sana .lakini nimeangalia mara mbili mbili nimeona ni wawili tu.au kuna majina mengine.au unaleta mengine tena baadaye. Ukanishituage basi.
Jitihada zako zote za kuwa chawa mpaka sasa hazija zaa matunda? Rudi kwenu Vwawa ukalime viazi.Achana na uchawa kwa mama Abdul!
 
Back
Top Bottom