Uteuzi Septemba 16, 2024: Rais Samia afanya uteuzi wa viongozi akiwemo Katibu wa Bunge

Uteuzi Septemba 16, 2024: Rais Samia afanya uteuzi wa viongozi akiwemo Katibu wa Bunge

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:

(i) Bi. Nenelwa Mwihambi ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Kabla ya uteuzi huu, Bi. Mwihambi alikuwa Katibu wa Bunge; na

(ii) Bw. Baraka Ildephonce Leonard ameteuliwa kuwa Katibu wa Bunge. Bw. Leonard anachukua nafasi ya Bi. Mwihambi ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Viongozi walioteuliwa wataapishwa tarehe 19 Septemba, 2024 saa 09.00 alasiri, Ikulu - Dar es Salaam.

Prof Ibrahim Juma,ndiyo baasi tena.
 
Kila anapoteua mheshimiwa Rais; ukitizama mkeka wa majina, "HALIONEKANI JINA LA NDUGU WALA JAMAA WA KARIBU !"
 
Kutoka kuwa katibu wa bunge kwenda kuwa jaji..ni demotion au promotion hiyo?
 
Uliposema viongozi mbalimbali nikajuwa ni wengi sana .lakini nimeangalia mara mbili mbili nimeona ni wawili tu.au kuna majina mengine.au unaleta mengine tena baadaye. Ukanishituage basi.
Mbalimbali inaanzia na wangapi?
 
Toka Thomas Kashilila aondoke hakuna katibu ninayemfahamu toka kipindi hicho
Utawafahamu vipi Wakati Bunge limepoteza kabisa mvuto. Binafsi hata Mimi simjui Katibu wa Bunge tangu Kashilila aondoke. Huwa nashtuka TU kuona magazetini kuwa Bunge linaendelea huko Dodoma.
 
Nani kakwambia kuwa huwa najitoa akili katika kuandika.Mimi huwa natumia akili katika kuandika.ndio maana naandika kwa hekima ,husara na hoja zenye kueleweka. Ila wewe ndugu yangu ndio huwa hatumii kabisa akili kuandika zaidi ya kuropoka tu
Kweli wewe unaandika kwa hekima, "husara" na hoja zenye kueleweka.
 
Uliposema viongozi mbalimbali nikajuwa ni wengi sana .lakini nimeangalia mara mbili mbili nimeona ni wawili tu.au kuna majina mengine.au unaleta mengine tena baadaye. Ukanishituage basi.
Watateuliwa wote lakini wewe utaendelea kupiga Deki Lumumba mpaka uote Kibiongo.
 
Makatibu wa Bunge kipindi hiki wamekuwa wakikaa kwa muda mfupi sana na kuondoka. Je, wanaondolewa kwa kushindwa kufanya kazi au bosi wao anashindwa kuendana na kasi yao?
 
Back
Top Bottom