Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Kama namuona vile sheikh Ponda akisoma uzi huu kwa kuurudia rudia.Mufti wa Tanzania amemteua aliyekuwa RPC wa Dar es Salaam, Alhaji Suleiman Kova kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maboresho ya BAKWATA.
Uteuzi huu umekuja kufuatia kujiuzulu ghafla kwa Mwenyekiti wa awali Sheikh Issa Othman, ambaye amefanya kazi hiyo kwa miezi mitatu tu, Sheikh Issa Othman ameachia ngazi kwa madai ya kukumbana na vikwazo vizito kwenye utekelezaji wa Majukumu yake.
Kila la heri Alhaji Kova
Waislam wa Tanzania wanahitaji sana sana kusikilizwa na kuendelezwa. Hatuendelezi dini bali Watanzania. Mikoa yenye waislam wengi imenyimwa maendeleo kwa makusudi.