Uteuzi wa Afande Ramadhani Kingai kuwa DCI (Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai). Je, Rais Samia amepotoshwa?

Ni huyu aliyekuwa anahusishwa na utekaji na yale mambo ya wasiojulikana, naona sasa nchi inahitaji mafia ili watu waheshimiane, serikali inajiona untouchable
Nasubiri kuona utaifanya nini serikali
 
Huyu yupo vizuri sana,

Yupo very straight kwenye mambo yake hana longo longo.

Nadhani wengi wanaopiga kelele hapa ni mambo ya kisiasa tu ila kiuweledi yupo vizuri.
DCI asiyejua PGO hafai kabisa
 
Huu ndio utopolo mtupu.
Ndio maana madai ya KATIBA MPYA ni muhimu. Nafasi kama hizi zinatakiwa kuombwa kama ada ya ufahamu na uelewa hata akiteuliwa!
Na isitoshe nafasi hizi zinatakiwa kupitishwa bungeni na wahusika kwenda kujieleza Kwa Nini anaona anafaa kwenye hiyo nafasi na atafanya Nini? Yawepo maswali yenye tija sio ya kubeA
 
Huyu yupo vizuri sana,

Yupo very straight kwenye mambo yake hana longo longo.

Nadhani wengi wanaopiga kelele hapa ni mambo ya kisiasa tu ila kiuweledi yupo vizuri.
Mkuu nakukubali sn lakini kwa Kingai big no bora hata Sabaya
 
Matahira bhana!Mkiambiwa kuwa CCM haifai hamsikii,ninyi ni kukomaa tu na Samia.🐒🐒🐒
 
CCM ina laana,badala ya kuteua watu wenye weledi kama hawa, unateua Mapaka!🐒🐒🐒
Your browser is not able to display this video.
 
Mbowe kashaingizwa chaka kwa maridhiano ya mchongo.
 
Mtoa mada huna hoja. Je hayo aliyoyafanya kingai je ni maamuzi yake binafsi au ni maelekezo, juu yake yuko IGP na viongozi wengine kwanini hujajiuliza hill kabla ya kumlaumu.
 
Unawezaje kumpa mtu nafasi ya DCI wakati umma wa Watanzania wanafahamu huyu mtu amechafuka?

Je, huu ndio mwanzo wa watu kubambikiwa kesi za mauaji hapa nchini?
Binafsi naliwaza kwa sauti kuu, nahisi aqngekuja mbele ya jamii ili aseme kitu ili aweze kuaminika na umma.
 
Wacha watu wakule maisha

Pambana na wewe
 
Waliomshauri Amiri Jeshi Mkuu Kumteuwa Camilius Wambura kuwa IGP na Ramadhani Kingai kuwa DCI hakika jicho lao limelega ipasavyo.

Wambura ni muadilifu sana, ana nidhamu , ni msikivu/mfuatiliaji wa shida za watendaji wa chini yaani hata awe ni Constable atafuatilia na haki itatendeka, pia ni mtu mwenye ushirikiano mzuri sana na vyombo vingine/ kimsingi ana busara sana. Lakini kubwa kuliko yote ni mtendaji mahiri/hardworking.

Kuhusu CP Ramadhan Kingai jamaa yupo Kikazi sana na ni mtu anayejali na kuheshimu Misingi ya kazi. Mtendaji Mzuri, mfuatiliaji yaani sio mtu wakufanya jambo bila kujiridhisha uhalisia wake, anazingatia sana Nidhamu ya Kijeshi. Ni mtu anayefikika na msikivu(Approachable). Kiufupi jamaa akili yake imetulia vizuri. Kingai ni hazina na ninampongeza aliyemshauri Rais.

Kuhusu CP Liberatus Saba's aliyeteuliwa kuongoza mambo ya Fedha na Logistics siwezi kumzungumzia lakini inasemekana JAMAA NI MSAFI SANA na MUADILIFU

Kuhusu CP Awadhi aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Operation kwa kweli jamaa Kazi anaiweza sana na sio mtu wa ofisini tu bali pia ni mtu wa field kwa sana. Yeye ni mtu anayependa kuona sheria zilizowekwa zinafuatwa kama zilivyoandikwa na hana cha kuangalia excuse za mazingira nk nk.

Japo hapa inaweza kutafsiriwa kama NI AINA YA KIONGOZI ALIYE RIGID, Mfano sheria inakataza eneo fulani dereva kuendesha speed ya 50 hivyo akikukamata unaendesha 70 hata kama unamuwahisha mgonjwa Muhimbili kuokoa maisha yeye anaweza kukung'ang'ania tu.

Kwa hiyo ni Mtu wa kunyoosha haswa yeye anachoangalia ni utaratibu, yaani hata itokee amekukabidhi chupa ya maji halafu ukayanywa pengine ulihitaji kumeza dawa kuponya kichwa chako yeye atakukomalia kuwa ulitakiwa upate ruhusa na sio kujiamlia.

Na vilevile inasemekana ni Mtu ambaye hana mahusiano mazuri na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama japo hapa binafsi sijajua ni kwanini na kivipi.

Kimsingi jamaa katika kazi ni jembe hasa. Hayo mengine nadhani anaweza kushauriwa kulingana na unyeti wa Madaraka aliyopewa sasa.
 
Wakati huku Tanzania akina Kingai walipandiswa cheo, huko Kenya ambako kuna Rais wa watu hali ni Tofauti.
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…