Uteuzi wa Afande Ramadhani Kingai kuwa DCI (Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai). Je, Rais Samia amepotoshwa?

Kama tunaamini urais ni taasisi basi hakuna haja ya kuwa na wasiwasi juu ya teuzi za rais. Naamini vetting ya kutosha hufanyika kabla rais hajaamua kutangaza uteuzi.

Na pia rais hawezi kuendesha mambo yake kwa kutegemea matakwa ya individuals. Taratibu zinazingatiwa.
Kama vetting yenyewe ndiyo hivi basi hata hao wafanyao vetting wanatakiwa kupigwa chini
 
Kingai mnamnalumu bure. Kwanza tunapaswa kujua kuwa boss wake ni nani ! Hivyo malalamiko yote mnayomlalamikia hakufanya kwa matakwa yake bali kwa kutii maagizo.

Hivyo unaweza kuta jamaa ni mtendaji mzuri sana hivyo tusubiri tuone.
Hapana Kisiasa kuna mtu anahitajika kupmzka kwa ajili ya Utii wa Mamlaka ya wananchi. Huyu alitakiwa hata ukuu wa kituo asipewe.
 
Kingai kupandishwa cheo ni kuonyesha jinsi gani hizi kitu zinaitwa vetting ni ubabaishaji mtupu,kingai alionyesha jinsi gani hajui taratibu za jeshi la porisi,alivyo mtupu kwenye sheria,mbali na kutumika ila hajui kazi zake
 
MH Rais mama yetu Samia Suluhu Hassan kwakweli japo jeshi Zima la polisi limekuwa bovu Sanaa lakini Kuna wachache ambao Wana hofu ya Mungu, na Taasisi kubwa na ya muhimu kama hili jeshi halitakiwi kuwa na kiongozi asiyetoa Haki au Mwongo.

Kama mama una nia kweli ya kulirekebisha watu kama KINGAI hawakupaswa kupewa ofisi kubwa maana kwa UONGO na uonevu aliowafanyia watu akiwa ngazi za chini akiwa Ngazi uliyompa atakuwa mbaya zaidi .

Sio polisi mwenye maadili hasa msingiziaji mporaji wa haki za watu mtesaji ana damu kwenye vganja vyake.

Jiepushe nae, HAWEZI kutenda Haki tunakuomba Unda na kulisuka upya Hili jeshi lililopoteza maana ya jeshi la kusimamia Haki.

Kwa hili nasema WAMBURA SAWA LAKINI SIO KINGAI, HAPANA.
Samia ana washauri wabaya aisee!!
 
Hii ni dharau kwa watanzania. Hivi rais Samia anapofushwa madaraka kiasi kwamba haoni Wala hasikii malalamiko ya watanzania?
Kwani Kingai ni Mnyarwanda!?...Na je una takwimu ya hao "Watanzania" wanaolalamika!? Pia unatambua Rais wa JMT ndio mwakilishi Halisi wa Watanzania (walio wengi)!?

Binafsi ninaamini Kingai anastahili uteuzi huu, baadhi ya Watanzania watalalamika only because Kingai alikua exposed Sana kwenye Media,but naamini ata IGP Mpya angekuwa kwenye firing line ya media si ajabu wengi mngekosoa uteuzi wake ..Polisi wote wanapitia same drill, na training ni zile zile...wote ni sawa, tofauti ndogo ya polisi wetu ni , kuna baadhi wanaendaga nje ya maadili kama vile kupokea Rushwa nk..But kitaaluma na kimfumo ,..they are all the same.
 
Kwanini kama Taifa tunarudia makosa ya kuteua watu wenye makando kando kama Afande Ramadhani Kingai? Huyu mtu kwa sasa anafahamika na kila Raia kwa matendo yake yaliyojidhihirisha pale Mahakamani wakati wa kesi ya Mbowe

Je, tunasubiri afanye ukatili na unyama wa kiasi gani kwenye hili Taifa?

Tulishajifunza wakati wa JPM umuhimu wa vetting ya viongozi kwa yaliyotokea. Je, bado tunaendelea kujifunza.

Afande Kingai hakupaswa kupewa nafasi ya DCI hata kidogo, Imani ya Raia kwa huyu mtu ni ndogo sana, Wakati wa kesi ya Mbowe huyu alihusishwa na utesaji na utekaji, Na hata majibu yake mahakamani alijichanganya sana kuhusu kuwahamisha watuhumiwa tokea kituo kimoja cha polisi kwenda kingine na malengo yake kuhusu utesaji

Uteuzi wa Afande Ramadhani Kingai kuwa Mkurugenzi wa makosa ya jinai unaligawa Taifa ambalo Rais Samia alikuwa anafanya jitihada za kuliunganisha kwa maridhiano

Kwenye kesi ya Mbowe pale mahakamani, Afande Kingai alikuwa shahidi mkuu upande wa jamhuri na ushahidi wake alioutoa pale mahakamani wa kuwanunulia watuhumiwa Mo energy ikawa mwanzo wa watu kuamini huyu Bwana ameshiriki Katika kesi ya mchongo kuanzia kudraft mpaka kupeleka mahakamani.

Afande Kingai alishindwa kujibu maswali ya mawakili wa utetezi hata moja na hata maswali yaliyohusiana na kitendea kazi chake ya General Orders of police ( PGO) alionekana haelewi pale Mahakama ya uhujumu Uchumi sinza.

Ushahidi wa Afande Kingai ambaye alikuwa Shahidi mkuu ulileta mkanganyiko pale mahakama ya uhujumu Uchumi na ndio ukawa mwanzo wa watu kufahamu siri ya kesi ya akina Mbowe pamoja na Kikosi kazi maalum kilichojumuisha Afande Goodluck

Maswali ya kujiuliza sisi kama Raia wa nchi hii:

Unawezaje kumpa mtu nafasi ya DCI wakati uma wa watanzania wanafahamu huyu mtu amechafuka?

Je huu ndio mwanzo wa watu kubambikiwa kesi za mauaji hapa nchini?

Je uteuzi huu Bwana Kingai sio ni mwanzo wa kufumua madonda ambayo Rais Samia alishaanza kuyaponya?

Moja ya watu kuzidi kudai katiba mpya ni kutokana na uteuzi wa watu aina ya Afande Kingai, Tungekuwa na tume maalum ya kuchuja na kuteua aina ya watu kama Afande Kingai kama Rasimu ya Jaji warioba alivyopendekeza tusingekuwa na utata
Mtu wa ovyo sana huyu kuteuliwa, kwanza ni incompetent (hajui hata vifungu vya PGO)
 
Kingai mnamnalumu bure. Kwanza tunapaswa kujua kuwa boss wake ni nani ! Hivyo malalamiko yote mnayomlalamikia hakufanya kwa matakwa yake bali kwa kutii maagizo.

Kwa mfano wewe hapo sasa hivi ubake binti mdogo wa miaka sita wa nyumba ya jirani na kwako, kwa kushauriwa na boss wako, lawama zote abebeshwe boss wako?.
 
Kwani Kingai ni Mnyarwanda!?...Na je una takwimu ya hao "Watanzania" wanaolalamika!? Pia unatambua Rais wa JMT ndio mwakilishi Halisi wa Watanzania (walio wengi)!?
Binafsi ninaamini Kingai anastahili uteuzi huu, baadhi ya Watanzania watalalamika only because Kingai alikua exposed Sana kwenye Media,but naamini ata IGP Mpya angekuwa kwenye firing line ya media si ajabu wengi mngekosoa uteuzi wake ..Polisi wote wanapitia same drill, na training ni zile zile...wote ni sawa, tofauti ndogo ya polisi wetu ni , kuna baadhi wanaendaga nje ya maadili kama vile kupokea Rushwa nk..But kitaaluma na kimfumo ,..they are all the same.
Sasa why ateue mtu kilaza kabisaa??
 
Rais HAPANGIWI.......Ni ukosefu wa ADABU na HESHIMA kuanza kumpangia na kumshinikiza Rais.

Pongezi kwa mteule.
kamwe usisikilize majungu.....piga kazi.
Majungu na fitina havina nafasi katika awamu hii ya 6.
 
sasa why ateue mtu kilaza kabisaa??
Nadhan atakua ni mmoja ya watu waliopendekezwa kwa Rais ili wateuliwe...na wanaopendekeza always wanatafuta best suited candidates ambao wanaweza kuhudumu kwa muda na wakati uliopo.
 
Ndo mjue sasa aliyowahi kuyafanya mkamchukia hakujiamulia ilikuwa ni amri.

Ninyi huku nje ndo mnamuona mchafu ila wanaomjua vizuri huko ndani wanaona anafaa kwa nafasi aliyopewa.

Hii inanifundisha kuwa zile tuhuma hazikuwa zake kuna pahali zilipaswa kuelekezwa yeye alikuwa anatekeleza alichotumwa.
Uko kama mimi huenda hata kujichang'anya kule ni kuwalinda 'wakubwa'..
 
Kwanini kama Taifa tunarudia makosa ya kuteua watu wenye makando kando kama Afande Ramadhani Kingai? Huyu mtu kwa sasa anafahamika na kila Raia kwa matendo yake yaliyojidhihirisha pale Mahakamani wakati wa kesi ya Mbowe

Je, tunasubiri afanye ukatili na unyama wa kiasi gani kwenye hili Taifa?

Tulishajifunza wakati wa JPM umuhimu wa vetting ya viongozi kwa yaliyotokea. Je, bado tunaendelea kujifunza.

Afande Kingai hakupaswa kupewa nafasi ya DCI hata kidogo, Imani ya Raia kwa huyu mtu ni ndogo sana, Wakati wa kesi ya Mbowe huyu alihusishwa na utesaji na utekaji, Na hata majibu yake mahakamani alijichanganya sana kuhusu kuwahamisha watuhumiwa tokea kituo kimoja cha polisi kwenda kingine na malengo yake kuhusu utesaji

Uteuzi wa Afande Ramadhani Kingai kuwa Mkurugenzi wa makosa ya jinai unaligawa Taifa ambalo Rais Samia alikuwa anafanya jitihada za kuliunganisha kwa maridhiano

Kwenye kesi ya Mbowe pale mahakamani, Afande Kingai alikuwa shahidi mkuu upande wa jamhuri na ushahidi wake alioutoa pale mahakamani wa kuwanunulia watuhumiwa Mo energy ikawa mwanzo wa watu kuamini huyu Bwana ameshiriki Katika kesi ya mchongo kuanzia kudraft mpaka kupeleka mahakamani.

Afande Kingai alishindwa kujibu maswali ya mawakili wa utetezi hata moja na hata maswali yaliyohusiana na kitendea kazi chake ya General Orders of police ( PGO) alionekana haelewi pale Mahakama ya uhujumu Uchumi.

Ushahidi wa Afande Kingai ambaye alikuwa Shahidi mkuu ulileta mkanganyiko pale Mahakama ya Uhujumu Uchumi na ndio ukawa mwanzo wa watu kufahamu siri ya kesi ya akina Mbowe pamoja na Kikosi kazi maalum kilichojumuisha Afande Goodluck

Maswali ya kujiuliza sisi kama Raia wa nchi hii:

Unawezaje kumpa mtu nafasi ya DCI wakati umma wa Watanzania wanafahamu huyu mtu amechafuka?

Je, huu ndio mwanzo wa watu kubambikiwa kesi za mauaji hapa nchini?

Je, uteuzi huu Bwana Kingai sio ni mwanzo wa kufumua madonda ambayo Rais Samia alishaanza kuyaponya?

Moja ya watu kuzidi kudai Katiba Mpya ni kutokana na uteuzi wa watu aina ya Afande Kingai, Tungekuwa na tume maalum ya kuchuja na kuteua aina ya watu kama Afande Kingai kama Rasimu ya Jaji Warioba alivyopendekeza tusingekuwa na utata
Sifa kubwa iliyompandisha cheo ni dini yake
 
Imani ya Rais kwa Kingai ingekuwa ndogo asingemteua kuwa DCI, Rais ana imani naye na ile kesi ya Gaidi Mbowe si kipimo cha utendaji wa Kingai. Muacheni achape kazi
 
Hakika

Hakuna aliyetarajia KINGAI kupata UKURUGENZI kutokana na Mwenendo mzima wa KESI ya Kutunga ya UGAIDI Kama KINGAI kapanda CHEO basi Tutarajie MAJAJI MAWAKILI NA MAPOLISI wote nao Waliohusika ktk KESI ya UGAIDI WATAPANDA VYEO

Kweli KUFA KUFAANA
Wengine Wanateswa na Kuumizwa Watesaji WANAPANDA VYEO.
 
Kwanini kama Taifa tunarudia makosa ya kuteua watu wenye makando kando kama Afande Ramadhani Kingai? Huyu mtu kwa sasa anafahamika na kila Raia kwa matendo yake yaliyojidhihirisha pale Mahakamani wakati wa kesi ya Mbowe

Je, tunasubiri afanye ukatili na unyama wa kiasi gani kwenye hili Taifa?

Tulishajifunza wakati wa JPM umuhimu wa vetting ya viongozi kwa yaliyotokea. Je, bado tunaendelea kujifunza.

Afande Kingai hakupaswa kupewa nafasi ya DCI hata kidogo, Imani ya Raia kwa huyu mtu ni ndogo sana, Wakati wa kesi ya Mbowe huyu alihusishwa na utesaji na utekaji, Na hata majibu yake mahakamani alijichanganya sana kuhusu kuwahamisha watuhumiwa tokea kituo kimoja cha polisi kwenda kingine na malengo yake kuhusu utesaji

Uteuzi wa Afande Ramadhani Kingai kuwa Mkurugenzi wa makosa ya jinai unaligawa Taifa ambalo Rais Samia alikuwa anafanya jitihada za kuliunganisha kwa maridhiano

Kwenye kesi ya Mbowe pale mahakamani, Afande Kingai alikuwa shahidi mkuu upande wa jamhuri na ushahidi wake alioutoa pale mahakamani wa kuwanunulia watuhumiwa Mo energy ikawa mwanzo wa watu kuamini huyu Bwana ameshiriki Katika kesi ya mchongo kuanzia kudraft mpaka kupeleka mahakamani.

Afande Kingai alishindwa kujibu maswali ya mawakili wa utetezi hata moja na hata maswali yaliyohusiana na kitendea kazi chake ya General Orders of police ( PGO) alionekana haelewi pale Mahakama ya uhujumu Uchumi.

Ushahidi wa Afande Kingai ambaye alikuwa Shahidi mkuu ulileta mkanganyiko pale Mahakama ya Uhujumu Uchumi na ndio ukawa mwanzo wa watu kufahamu siri ya kesi ya akina Mbowe pamoja na Kikosi kazi maalum kilichojumuisha Afande Goodluck

Maswali ya kujiuliza sisi kama Raia wa nchi hii:

Unawezaje kumpa mtu nafasi ya DCI wakati umma wa Watanzania wanafahamu huyu mtu amechafuka?

Je, huu ndio mwanzo wa watu kubambikiwa kesi za mauaji hapa nchini?

Je, uteuzi huu Bwana Kingai sio ni mwanzo wa kufumua madonda ambayo Rais Samia alishaanza kuyaponya?

Moja ya watu kuzidi kudai Katiba Mpya ni kutokana na uteuzi wa watu aina ya Afande Kingai, Tungekuwa na tume maalum ya kuchuja na kuteua aina ya watu kama Afande Kingai kama Rasimu ya Jaji Warioba alivyopendekeza tusingekuwa na utata
😆😆 Chadomo bwana ,mna ujumbe wenu huku 👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220720-092231.png
    Screenshot_20220720-092231.png
    137.2 KB · Views: 5
Back
Top Bottom