OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Baada ya mwanamama Barbra CEO wa Simba Sc kuteuliwa CAF kumekuwa na kejeli za kila aina kutoka Yanga. Kejeli hizi zinafanya nje na ndani ya JF. Kuhusu uwezo wake hakuna shaka, hata wanaokejeli humu wanalijua hilo.
Ila najiuliza shida nini tumekuwa haters wa kiwango hiki? Mtindo huu wa maisha ya Simba na Yanga ulioibuka miaka ya karibuni ni kazi ya watu waliowekeza kwenye kupandikiza chuki badala ya utani wa jadi.
Kejeli zimeenda mbali zaidi na kumdhihaki kingono.
Kabla zijafika mbali nikarudi kujiuliza au ndio ile kauli iliyowahi kutolewa kwamba ndugu zetu Yanga wana watu wawili tu wenye akili sawa sawa? Kama wewe ni miongoni mwa hao wawili,unawezaje kuwa juha wa kiwango hicho?
Nimeuliza swali?