Hapo nilipokoleza pahusike.
Unabii wake Bwana Lema hovyo kabisa😉
Mwaka juzi, kama si mwaka jana mwanzoni,
Aliwahi kuonya juu ya Kiburi cha bwana mmoja (Kipindi hicho huyo bwana alikuwa anajipigia ndogonogo cheo cha Ukiranja wa Malaika akienda Mbinguni)
Bwana huyo ('Mungu mtu' kwa maneno ya Lema)
Aliekezwa ajirekebishe kinyume na hivyo, asingeweza kuiona 2020,
Unajua kilichotokea?
Mungu tu akatoa bonas ya 'vimiezi' kama vitatu, lakini bwana yule hayupo tena kama ilivyotabiriwa.
Chakujiuliza ni iwapo Mungu alimpa Ukiranja wa Malaika yule bwana ama la .
Mwambieni Lema aache ubabaishaji jamani.