Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu Mpya wa TISS, Said H. Masoro, na Mtazamo wangu

Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu Mpya wa TISS, Said H. Masoro, na Mtazamo wangu

Magu alikuwa na kamsemo kake " hakuna vita mbaya kama vita ya uchumi". TISS wangelikuwa makini na hiyo kauli, jamaa tungekuwa naye hadi sasa.

Kifo cha Magu kinaonesha wazi kwamba TISS wako sharrow kwenye ujasusi wa kiuchumi na wamejikita zaidi kwenye ujasusi wa kisiasa. Magu ali out smart hiyo taasisi kwani maamuzi ya Magu yalikuwa mbele zaidi ya TISS.

CIA, M16, MOSSAD, KGB , etc ndo taasisi zinazofanya biashara kubwa duniani kama madini, mafuta, madawa e.t.c. hawa jamaa wanatoa funds kwa local private companies ili ziweze kuwapatia data za kibiashara. TISS yetu imelala usingizi wa pono kwenye upande wa uchumi ila wako active kuwakamata wanasiasa na kulinda chama.

Projects kama Kabanga Nickel, SGR na Bwawa la nyerere zikisimamiwa vizuri zitaleta impact kubwa kwenye uchumi wa nchi ila zinaendeshwa kisiasa na sidhani kama zitatoboa.

Kiukweli hii nchi ili iweze kusonga mbele, TISS inabidi wabadilike, wajikite zaidi kwenye uchumi. Waende sambamba na tech startup companies zenye innovations ila hazina mitaji wazisimamie ziweze kwenda na vizuri na kasi ya dunia.

Rwanda na Kenya wanajitahidi katika ujasusi wa kiuchumi ndiyo maana wanapeta kwenye nyanja za kimataifa.
Hawezi kuelewa haya Mambo

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
 
Hiki ulichoandika hapa sio kazi kuu za Idara za Usalama wa Taifa/Ujasusi duniani. Kazi za majususi ni ulinzi na usalama wa nchi masuala ya uchumi na biashara yataingizwa huko katika majuku yao kama ni kitisho cha usalama wa nchi zao au kama yataleta matokeo fulani kiusalama.

Hizi kazi za uchumi na biashara katika nchi ni kazi kuu za Wizara ya Fedha na Benki Kuu.
Nenda na wakati. Dunia nzima iliyoendelea inatumia Ujasusi katika mambo ya uchumi; aidha kuzuia wengine wasikopi bidhaa zao, au wao kukopi bidhaa za wengine, kuzuia rushwa nk.
Mchina kaendelea vipi?
 
Yoda bwana! Unafikir vita nyingi duniani husabanishwa na nini? Nyingi ni uchimi, Ukraine, Ghuba, Syria kote huko ni uchumi.
Lakini pia kumbuka mtu mmoja alitangaza vita ya kiuchumi hakutoboa, laiti tungekuwa na taasisi iliyojiimarisha huko ingesaidia.

Sent from my Infinix X693 using JamiiForums mobile app
Uchimi wamaanisha uchumi? Mm sikujua kumbe Vita vya Syria vimesababishwa na uchumi,kiaje aisee?
 
Hahaha kasome tanzania intelligence and security service Act 1996. Ujue kazi za hii idara ni nn... Nandomana Kuna kitengo kinaitwa FIU(financial intelligence unit) Kipo BOT kama left wing ya TISS na uzijue kazi za hii FIU hasa ni nn

Sent from my 701SO using JamiiForums mobile app
Reference ya hoja ama makala hii ni sheria ya Usalama wa taifa ya January 20 mwaka 1997. Sasa unaniambia nikasome sheria hiyo hiyo tena ambayo mimi nimeonyesha mapungufu?

By the way, Financial intelligence Unit ya BOT unafahamu imeanzishwa lini na nani kaianzisha baada ya nini kutokea?
 
Jibidiishe kusoma maandiko mbali mbali utaelewa na Kukubaliana na mtoa uzi.

Idara Ya Usalama wa Taifa ina cover almost sector zote ambazo zinafanya Ustawi wa Taifa na zinazochangia Maendeleo na au "Stability" ya Taifa.
Umeielewa makala kuu kweli? Hakuna mahali ambapo makala hii inasema kuwa TISS haifanyi haya yaliyopendekezwa, Hoja kuu ni kuwa Ujasusi wa kiuchumi upewe kipaumbele zaidi tofauti na sasa siasa inapewa kipaumbele. Nini kinakufanya usielewe hoja hii ndogo tu?
 
Nenda na wakati. Dunia nzima iliyoendelea inatumia Ujasusi katika mambo ya uchumi; aidha kuzuia wengine wasikopi bidhaa zao, au wao kukopi bidhaa za wengine, kuzuia rushwa nk.
Mchina kaendelea vipi?
Kwani tiss yetu haifanyi hayo mkuu

Ova
 
Hiki ulichoandika hapa sio kazi kuu za Idara za Usalama wa Taifa/Ujasusi duniani. Kazi za majususi ni ulinzi na usalama wa nchi masuala ya uchumi na biashara yataingizwa huko katika majuku yao kama ni kitisho cha usalama wa nchi zao au kama yataleta matokeo fulani kiusalama.

Hizi kazi za uchumi na biashara katika nchi ni kazi kuu za Wizara ya Fedha na Benki Kuu.
Tanzania inategemea sana kilimo,uvuvi, mifugo, maliasili inayojumuisha mazao ya misitu,wanyamapori na madini katika kukupatia fedha za kigeni...na usalama wetu na kutengemaa kwa Amani vinategemea sana ustawi wa sekta hizi...sasa sisi watanzania wa kawaida kabisa tunajua kwamba yeyote anayehatarisha sekta hizo ana hatarisha usalama wa Taifa hili pia...swali sasa...Sekta hizi ni salama kweli, wanyamapori na mazao ya misitu yako salama, vyanzo vyetu vya maji na uoto wa asili uko salama, au ndio tunaambiwa resources zetu wameachiwa familia sijui 9 au 12 ili wahatarishe usalama wa watu million 60?....Nadhani tutakua tunakosea sana kama Taifa tukifikiri kwamba vipaumbele vyetu ni sawa na nchi nyingine... mindset na namna tunavyofanya mambo yetu ni muhimu sana tukaviweka na kuvipima kuendana na Hali halisi ya Kitanzania.... models za intelligence za CIA ,MI6 au KGB ni way to advanced...sisi tujikite kwenye maswala yetu ya Msingi...tutatoboa tuu...kwa mfano hivi Tanzania kwanini tupoteze resources zetu kuwekeza kwenye cyber security na wakati vyanzo vya maji,mito,madini vinachezewa mchana kweupe?!...au ni kweli unahitaji kuwekeza kwenye mambo ambayo huna Tija nayo na kwa pesa nyingi wakati mambo ambayo hayahitaji ata darubini na yanasaidia uchumi wako unayaacha yanafanywa ndivyo sivyo!?.... C'MON PEOPLE.... THINK WISELY.....IF YOU WORK FOR LIVING WHY KILL YOURSELF WHILE WORKING.
 
Kabla haujabishana na Mtoa mada hakikisha unaelewa Mada, Usalama wa Taifa ni Jambo zito sana. Tatizo Nchi zetu hizi zinaweka Tumbo mbele zaidi ya Maslai ya Taifa na wananchi wake.

Mfano Amerika Donald trump alitaka kukataa kuondoka ikulu kulinda Maslai ya Nchi Mkuu wa Kikosi Cha Ulinzi wa Raisi alimwambia ikulu sio Mali Yako na walimpa massa kadhaa aondoke .

Je huu usalama wetu hapa wanaweza hivyo? Wanaweza kumkamata na kumrekebisha kiongozi aliyekengeuka kimaadili? Zaidi ya Uchawa?

Ukiendesha Nchi Kwa Uchawa hamna kitu utaweza kufanikisha kamwe.

Hata katika swala la matumizi ya raslimali za Taifa na Mikataba ya kitaifa na Kimataifa , Usalama wa Taifa walitakiwa kuipitia na Kuitolea miongozo kama Ina manufaa au ni Hasara Kwa Taifa.

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Magu alikuwa na kamsemo kake " hakuna vita mbaya kama vita ya uchumi". TISS wangelikuwa makini na hiyo kauli, jamaa tungekuwa naye hadi sasa.

Kifo cha Magu kinaonesha wazi kwamba TISS wako sharrow kwenye ujasusi wa kiuchumi na wamejikita zaidi kwenye ujasusi wa kisiasa. Magu ali out smart hiyo taasisi kwani maamuzi ya Magu yalikuwa mbele zaidi ya TISS.

CIA, M16, MOSSAD, KGB , etc ndo taasisi zinazofanya biashara kubwa duniani kama madini, mafuta, madawa e.t.c. hawa jamaa wanatoa funds kwa local private companies ili ziweze kuwapatia data za kibiashara. TISS yetu imelala usingizi wa pono kwenye upande wa uchumi ila wako active kuwakamata wanasiasa na kulinda chama.

Projects kama Kabanga Nickel, SGR na Bwawa la nyerere zikisimamiwa vizuri zitaleta impact kubwa kwenye uchumi wa nchi ila zinaendeshwa kisiasa na sidhani kama zitatoboa.

Kiukweli hii nchi ili iweze kusonga mbele, TISS inabidi wabadilike, wajikite zaidi kwenye uchumi. Waende sambamba na tech startup companies zenye innovations ila hazina mitaji wazisimamie ziweze kwenda na vizuri na kasi ya dunia.

Rwanda na Kenya wanajitahidi katika ujasusi wa kiuchumi ndiyo maana wanapeta kwenye nyanja za kimataifa.
Ni kweli asilimia kubwa ya wafanyabuashara kwenye madini ni wastaafu wa vyombo vya usalama kwa ulaya na marekani.
 
Pengine huu ni mwanzo mpya wa mageuzi ya Idara ya Usalama wa Taifa. Mabadiliko haya ya uongozi yana maana kubwa sana kwa Idara yetu, ni matumaini yangu kwamba mabadiliko yatakwenda mbali zaidi kuguza muundo wa idara, mfumo wa idara, sheria na kanuni za idara ili kuendana na ulimwengu mpya wa dunia ya sayansi na teknolojia.

DGIS mpya Ndugu Said Masoro si mtu maarufu katika korido za Ujasusi Dar es Salaam ukimlinganisha na mtangulizi wake Athuman Diwani ambae umaarufu wake ulijengwa akiwa Intelijensia ya Polisi, DCI na katibu Tawala, Masoro anaweza kuwa chachu ya magezi ya chombo hiki muhimu na uti wa mgongo wa taifa letu ikiwa hataruhusu kumezwa na siasa chafu za Dar na Dodoma.

Moja ya Sababu kuu mimi kuamua kuandika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi, ilikuwa ni "kuhimiza mageuzi ya idara ya Usalama Tanzania na mfumo mzima wa ulinzi na Usalama nchini".

Nilifanya hivyo baada ya utafiti mkubwa nilioufanya na kujiridhisha kwamba mfumo uliopo hauwezi kulisaidia taifa katika ulimwengu huu mpya zaidi ya kulirudisha nyuma na kudumaza utu na fikra za kijamii huku dunia ikisonga mbele katika mageuzi ya kilimwengu.

Katika kitabu, nimeeleza mageuzi makuu matatu ya muhimu na ya lazima kwa Idara ya Usalama wa Taifa kama tunalitakia mema taifa hili. Mageuzi hayo ni; kwanza yaanze kwenye Sheria iliyounda chombo hiki, pili ni Muundo wa Chombo hiki, na tatu ni Sera ya chombo hiki adhimu kwa uhai wa taifa letu.

Kwa mjibu wa Katiba ya Tanzania ya 1977 Idara ya Usalama haitajwi moja kwa moja kwenye katiba hii tofauti na majeshi mengine yote ya Nchi. Yaani Katiba ya Tanzania haitambuwi uwepo wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Badala yake Chombo hiki kinatambuliwa na sheria ya Usalama wa Taifa ya 20 January 1997 iliyosainiwa na Benjamin William Mkapa, Rais wa Tanzania. Kwa maoni yangu hili ni moja ya makosa, Katiba Mpya inatakiwa kutambua na kuipa nguvu idara/taasisi hii pamoja na kwamba Chombo chochote cha usalama kinachoanzishwa kwa mjibu wa sheria ya Tanzania au katiba ya Tanzania, chombo hicho kitakuwa mali ya Tanzania na kitafanya kazi kwa maslahi ya Taifa na si vinginevyo.

Katika Kitabu cha Ujasusi nimeainisha mapendekezo yangu kwenye sheria ya Usalama wa Taifa ambayo nafikiri kwasasa sheria hiyo ni lazima ifanyiwe marekebisho ili kuendana na mageuzi ya dunia ya leo, tuko karne ya 21 sio enzi za zamadamu.

Moja ya vifungu katika Sheria ya Usalama wa Taifa iliyosainiwa 20 January 1997 na Rais Hayati Benjamiji W. Mkapa ambavyo ni muhimu sana kufanyiwa marekebisho ni. Mfano, kifungu 14 -(1), (2),(3), (4)-(a) na (b). Kifungu cha 15 -(1),(2), (3) -(a) na (b). Kifungu cha 16-(1) (a)na (b), (2) na (3).

Katika kitabu nimehimiza muundo wa Idara ambao umepitwa na wakati ubadilike, muundo huu unahusu kuanzia uajiri (recruiting) na mengineyo, Mfumo wa chama kimoja wa 1962 ulikuwa ndio mfumo wa uajiri wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama, na ndio ulikuwa mfumo wa ajira zingine, ilikuwa huwezi kuingia katika vyombo vya ulinzi na usalama bila kupita TANU YOUTH League/UVCCM.

Hadi ilipofika 1992 ndipo mfumo huo ulianza kutoweka katika sekta zingine, lakini katika vyombo vya dola haukutoweka kabisa, Hivi leo watumishi wa vyombo vya dola wengi walioingia kazini kuanzia 1992 kurudi nyuma hadi 1962, hawa ni makada wa chama cha mapinduzi 100%.

Wengi wao leo ni watu wazima ndio ma RPC, OCD na wakuu wa vitengo mbalimbali katika vyombo vya utumishi na vya dola, Hivyo ukimuona RPC anashangilia ccm ikishinda sio kosa lake bali itikadi kwake imekolea na aliingia jeshini kwa tiketi ya chama na sio professional yake.

Kizazi kilichoingia kwenye vyombo vya ulinzi na Usalama miaka ya karibuni angalau hiki msingi wa kuingia kwao ni elimu, undugulaizesheni na kuipenda kazi husika, japo ukada bado una nguvu ndani ya vyombo hivyo, kwamba leo unaweza kuona maajabu RPC anastaafu leo na kesho akagombea uenyekiti wa ccm mkoa au Ubunge utajiuliza lini aliuwa mwanachama kama katiba ya ccm inavyotaka awe mwanachama angalau miaka miwili.

Sera ama Malengo makuu ya Ujasusi Tanzania yanatakiwa kujikita katika Uchumi kwakuwa hakuna njia ya mkato ya kufikia mafanikio ya Taifa kiuchumi bila kuruhusu uchumi wetu uongozwe katika misingi ya Idara ya Usalama wa Taifa na Jeshi la Wananchi Tanzani (TISS na MI).

Hapa ieleweke sana, sina maana biashara na makampuni ya uwekezaji yawe ya vyombo hivyo vya ulinzi, au yawe ya serikali, la hasha, nina maana pana zaidi kwamba ushughulikiaji wa taarifa za biashara na uchumi utiliwe mkazo zaidi kuliko ilivyo sasa taarifa za kisiasa ndizo zenye nguvu ya nchi, Mapendekezo ni TISS itilie mkazo taarifa za uchumi na biashara zaidi na kuzipa ulinzi shughuli na biashara zote za uwekezaji wa ndani na nje na wawekezaji wake. Hawa waitwe rasmi kuwa ni (asset).

Tanzania iwe na shirika la Ujasusi linaloangalia siasa kama njia tu, na sio msingi imara wa kulinda TAIFA, wanausalama watakao kuwa makini kuona kofia ya siasa haizidi kofia ya nguvu ya umma au TAIFA. Ni wakati mwafaka wa kutambua NCHI ndio nguzo ya UTAIFA na sio siasa kuwa ndio UTAIFA wenyewe.

Kusimamia Demokrasi kwa jicho la ndani na sio jicho la upendeleo wa kiitikadi bali kuongozwa na kusimamia maadilli ya NCHI dhidi ya siasa. Inatakiwa Shirika ambalo halitatumika kwa faida ya chama, Mtu au kikundi cha watu bali ukweli uwe Taifa lianitaji nini kutoka kwenye siasa. Nchi inaishi katika lindi la unafi hasa vijana.

Kwa undani zaidi, soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi popote ulipo duniani.


View attachment 2468554
Hao watu ni sehemu ya ambiguity, arbitrariness, capriciousness na impunity; nguzo 4 za Bad Governance. Si rahisi kubadili mfumo huu mbovu. Hasa kama ndiyo uliokuweka madarakani.
 
Tindo umeathiriwa sana na propaganda za uvyama mpaka inafikia mahala watu wakijadili mpira wewe unaingiza uvyama, wakijadili mziki wewe unaingiza uvyama, wakijadili mambo mengine ya taifa vilevile unakimbilia kuingiza uvyama.

Kwa aina hii ya maisha unayoishi, usipokuwa makini ipo siku utakuja kujiuwa kisa chama chako kimeshindwa uchaguzi fulani, afu wale walioshindwa kwenye chama chako husika wakiendelea na maisha yao ya kula bata.

Hii inanikumbusha baba yangu mdogo fulani (ambae sasa ashafariki) alitakaga kuchoma nyumba yake mwenyewe na yeye mwenyewe akiwa ndani, kisa team yake ya Simba imefungwa na Yanga miaka ya 90.
Isingekuwa watu kuwahi kuuzima moto na kuvunja mlango ili wamtoe, jamaa angekuwa amewahi kujiuwa kabla ya muda wake wa kufa haujafika. Wakati huo huo viongozi wa team ya Simba na wachezaji wao walikuwa wanaendelea na maisha yao ya kula bata bila kujali kufungwa kwao.
Hili ninalokwambia ulitafakari, bila hivyo kwa aina hii ya wanasiasa wetu wa bongo waliojaa janja janja ya kupiga pesa za umma, au kulamba asali ili kujiandalia maisha yao na ya vizazi vyao kuna siku utakuja kuumia, au kupata ugonjwa wa moyo ambao haukuwa nao before.

Lazima ujue kuna maisha nje ya siasa na mtu ukaishi vizuri tu bila presha wala shutuma kwa mtu mungine.
Real talk
 
Kitengo kilicho BoT ni kitengo chini ya BoT sio chini ya TISS. JWTZ wote wana kitengo cha Military Intelligence, polisi wana kitengo chao cha uchunguzi, mamlaka ya kuzuia dawa za kulevya wana kitengo cha cha upelelezi na ufuatialiji, hata Immigration wanaweza kuwa na kitengo cha cha uchunguzi n.k hivi vitengo vyote viko chini ya hizo taasisi zao kutimiza wajibu wa taasisi zao.
Sio kila kitengo cha uchunguzi katika idara ya serikali ni cha TISS, kwa makusudi au bahati mbaya nchi nyingi tofauti na za magharibi huwa wanapenda kuona muundo, miongozo na namna ya utendaji wa vyombo vya ujasusi unabaki gizani na hii imezifanya hizi taasisi kutoelewaka zinaanzia au kuishia wapi.
Na idara ya elimu ina left wing ya upelelezi, wanapeleleza nin?
 
Pamoja na kudharau uwezo mdogo wa mleta mada ila mmejikuta mnatufundisha mengi kupitia bandiko lake hili na yeye pia anazidi kujifunza zaidi mwisho wa siku atawazidi hata ninyi mnaojua au kujifanya kujua zaidi Hongera Yericko Nyerere
 
Back
Top Bottom