Uteuzi wa Nehemia Mchechu: Tunamchekea Rais Samia, lakini hapa ameonyesha udhaifu mkubwa

Walivyoondolewa ulipewa sababu? Uliona wakipelekwa Mahakamani?

Kwa nini useme Rais ana udhaifu?

Kwa taarifa yako Samia haongozwi na chuki
Tatizo anaongozwa na urafiki. nasikia na uhawala hawala ni mtaji.
 
Huyo ambaye mlimweka alifanya nini zaidi kurudisha nhic nyuma zaidi...watu wanayoijua nhic ilipokuwa kabla ya Msechu na alipoifikisha Msechu hawawezi kamwe kubeza kazi nzuri aliyoifanya..mnyonge mnyongeni haki yake mpeni..na Msechu kilichomtoa nhic si kingine ni wapika majungu waliokuwa na interest binafsi..na mzee baba akaingia king
 
Magufuli aliyajua madhambi ya Mchechu lakini akamuogopa Kikwete. Angemgusa Mchechu kwa namna moja ama nyingine angekuwa anamgusa JK, ikabidi amuondoe tu kwenye kile cheo.
 
Tatizo hutaji huo "ubadhirifu" wa Mchechu,

Hebu punguza povu kidogo fafanua kuhusu ubadhirifu wa Mchechu😀
 
Ninavyojua hawa wapigaji walikuwa na network, sasa ni kama Magufuli alikuja kukata ile network ila amekuja huyu naona anaunganisha tena network.

Niandike tu kwa kifupi; Katiba Mpya (Rasimu ya Warioba) ndio suluhisho la kudumu.
Magufuli aliondoa network ya Kikwete akiweka ya kwake
 
Tuache kukurupuka mamlaka za uteuzi kabla kufanya maamuzi lazima wapitie mafaili hawaji na majina yao mfukoni lazima kamati ya vetting impelekee taarifa kamili ya muhusika ndio aamue. kama alikuwa na makando kando huyu asigerudi.
 
Mchechu hakuwa na tatizo lolote katika uendeshaji wa NHC uenda alikataa kuhamishia miradi mikubwa ya NHC kuleeee jamaa akamtimua.
 
Tatizo hutaji huo "ubadhirifu" wa Mchechu,

Hebu punguza povu kidogo fafanua kuhusu ubadhirifu wa Mchechu😀
Ingia JF, fanya reference. Kama huwezi kufanya literature review unataka nani ahangaike kueleza mara nyingine tena. Hiyo ni hadithi ambayo iko JF kwa miaka mingi na kwa anayejua kusoma na kuandika unachouliza ni uzembe mkubwa.
 
Lema ni mkandarasi siyo Eng.
 
Ninavyojua hawa wapigaji walikuwa na network, sasa ni kama Magufuli alikuja kukata ile network ila amekuja huyu naona anaunganisha tena network.

Niandike tu kwa kifupi; Katiba Mpya (Rasimu ya Warioba) ndio suluhisho la kudumu.
Rasimu ya Warioba bado ina mapungufu, inasema Rais akishindwa kuendelea na Urais kwa sababu yoyote ile basi Makamu wa Rais atakuwa Rais Kwa kipindi kilichobaki,

Hii haiko Sawa,
Ilipaswa iwe kama muhula wake umebaki Kwa chini ya miezi 12 basi Makamu achukue nafasi yake Kwa kipindi kilichobaki mpaka uchaguzi, Ila zaidi ya hapo ndani ya siku 90 hasa siku ya 90 uitishwe uchaguzi mkuu kum-replace marehemu. Siyo hii ya sasa. Haitoi fursa ya awamu kuzaliwa!
 
Hivi hizi hasira tutazimalizia wapi na lini maana tunataka kupasuka kwa ukuda unaofanyika kuna hii ishu ya mgao Nani ana taarifa??
 
Ingia JF, fanya reference. Kama huwezi kufanya literature review unataka nani ahangaike kueleza mara nyingine tena. Hiyo ni hadithi ambayo iko JF kwa miaka mingi na kwa anayejua kusoma na kuandika unachouliza ni uzembe mkubwa.

Umejibu vizuri sana Mkuu!
 
Walivyoondolewa ulipewa sababu? Uliona wakipelekwa Mahakamani?

Kwa nini useme Rais ana udhaifu?

Kwa taarifa yako Samia haongozwi na chuki
...........haongozwi na chuki.
NImemkumbuka Ndugai!
 
...........haongozwi na chuki.
NImemkumbuka Ndugai!
Ndugai aliyewaapisha COVID 19 kwenye garage na kutusababishia bunge la hovyo katika historia ya Tanzania, kuna mtu kweli bado ana dadisi alitokaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…