Uteuzi: Watatu wapewa hadhi ya Ubalozi, yupo Katibu Mkuu Kiongozi

Uteuzi: Watatu wapewa hadhi ya Ubalozi, yupo Katibu Mkuu Kiongozi

Kumngoa Katibu mkuu kiongozi nyakati hizi anazidi kutupa maswali nini kinapandwa huko.
 
Ni hadhi. Mara nyingi Katibu Mkuu Kiongozi huwa ni Mabalozi hapo kabla.

Nadhani yeye pamoja na Dkt Bashiru ndiyo hawakuwa na Mabalozi. Hivyo Rais hufanya namna na kuwatunuku hadhi hiyo ya Ubalozi.

Hivyo anaendelea na majukumu yake kama Katibu Mkuu Kiongozi. Ila sasa atatambulika kama Balozi Dkt Moses Mpogole.

..Ni mbwembwe tu.

..kuna Makatibu Wakuu kiongozi hawakuwahi kuwa na hadhi ya ubalozi.

..mmojawapo ni Timothy Apiyo ambaye alitumikia wakati wa Nyerere na Mwinyi.

..hata Lumbanga aliyekuwa Katibu Mkuu kiongozi wakati wa Mkapa alipewa ubalozi baada ya kuondoka Ikulu.
 
HII INA MAANA GANI KUBAKI NA VYEO VYA ZAMANI..hawatakwenda balozini? au anawapa kinga maana sasa ni kizaa zaa
Ubalozi ni hadhi. Ukiwa balozi si lazima uwe na kituo cha kazi ubalozini.

Watu kama Mkuu wa Itifaki Wizara ya Mambo ya Nje mara nyingi anakuwa balozi ambaye anafanya kazi Wizara ya Mambo ya Nje (rejea Balozi Joshua Opanga, Balozi Cisco Mtiro).

Kuna Makatibu Wakuu Viongozi wengi wamekuwa mabalozi bila ya kuwa na vituo vya ubalozi kwa maana ya kwenda kuwa mabalozi katika nchi. (Rejea Balozi Philemon Rupia)

Hadhi ya ubalozi inaendana na kupewa hadhi ya diplomatic immunity kimataifa, hii hadhi inawezesha watu kufanya kazi nyingine nyeti kwa niaba ya taifa.

Kwa hivyo, kupewa hadhi ya ubalozi si lazima uende kuwa balozi kwenye nchi fulani.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
amefanya uteuzi wa Viongozi wafuatao kuwa na Hadhi ya Balozi kama
ifuatavyo:-
1. Dkt. Moses Mpogole Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi kuwa Balozi;

2. Dkt. Salim Othman Hamad, Msaidizi wa Rais anayeshughulikia
masuala ya Siasa kuwa Balozi; na

3. Dkt. Kassim Mohamed Khamis, Msaidizi wa Rais anayeshughulikia
masuala ya Hotuba kuwa Balozi.

Uteuzi huu wa Hadhi ya Balozi umeanza tarehe 12 Juni, 2023.
Aidha, Vyeo walivyonavyo vinabaki kama vilivyo.

Wateule wataapishwa tarehe 16 Juni, 2023 kuanzia saa 04:00 asubuhi - Ikulu,
Chamwino - Dodoma.
View attachment 2656278
Hiyo ndo kazi anayeimudu kwa sasa
 
Wonders shall never end in this regime.
 
..Ni mbwembwe tu.

..kuna Makatibu Wakuu kiongozi hawakuwahi kuwa na hadhi ya ubalozi.

..mmojawapo ni Timothy Apiyo ambaye alitumikia wakati wa Nyerere na Mwinyi.

..hata Lumbanga aliyekuwa Katibu Mkuu kiongozi wakati wa Mkapa alipewa ubalozi baada ya kuondoka Ikulu.
Kipindi cha Nyerere naweza kukubali kwa sababu, nchi haikuwa na Mabalozi wa kutosha enzi hizo. Nchi ilikuwa changa.

Baada ya enzi za Mwl, wengine wote walikuwa Mabalozi. Isipokuwa Luhanjo.

Hata hivyo, naamini haina mantiki yeyote.
 
Ubalizi ni hadhi. Ukiwa balozi si lazima uwe na kituo cha kazi ubalozini.

Watu kama Mkuu wa Itifaki Wizara ya Mambo ya Nje mara nyingi anakuwa balozi ambaye anafanya kazi Wizara ya Mambo ya Nje (rejea Balozi Joshua Opanga, Balozi Cisco Mtiro).

Kuna Makatibu Wakuu Viongozi wengi wamekuwa mabalozi bila ya kuwa na vituo vya ubalozi kwa maana ya kwenda kuwa mabalozi katika nchi. (Rejea Balozi Philemon Rupia)

Hadhi ya ubalozi inaendana na kupewa hadhi ya diplomatic immunity kimataifa, hii hadhi inawezesha watu kufanya kazi nyingine nyeti kwa niaba ya taifa.

Kwa hivyo, kupewa hadhi ya ubalozi si kazima uende kuwa balozi kwenye nchi fulani.
Rais, makamu wa Rais, Katibu mkuu kiongozi na mawaziri wana hadhi za ubalozi hata bila kupewa rasmi huo ubalozi.
 
Rais, makamu wa Rais, Katibu mkuu kiongozi na mawaziri wana hadhi za ubalozi hata bila kupewa rasmi huo ubalozi.
Nafikiri unaongelea diplomatic immunity, ambayo ni kinga ya kidiplomasia, lakini kinga ya kidiplomasia sio ubalozi.

Hata maafisa wa balozi wasio mabalozi wana kinga ya kidiplomasia.

Nyerere hajawahi kuwa balozi. Kikwete hajawahi kuwa balozi. Magufuli hajawahi kuwa balozi. Samia hajawahi kuwa balozi.

Marais waliokuwa na hadhi ya ubalozi Tanzania ni Balozi Ali Hassan Mwinyi, alikuwa balozi Cairo Egypt, na Balozi Benjamin William Mkapa, alikuwa balozi Lagos Nigeria na Ottawa Canada. Ni hao tu.

Of course rais ni diplomat number one wa nchi, lakini u diplomat wake ni kwa kupitia urais, si ubalozi.
 
Back
Top Bottom