Uteuzi: Watatu wapewa hadhi ya Ubalozi, yupo Katibu Mkuu Kiongozi

Uteuzi: Watatu wapewa hadhi ya Ubalozi, yupo Katibu Mkuu Kiongozi

Ila wao huku hadi ukuu wa wilaya wanapata.Hivi Nyerere kwa nini alikubali haya?Kweli Karume alikuwa kichwa,kumuingiza Nyerere mkenge namna hii jamani.
Tuna muungano wa hovyo sana. Babu nyerere alituingiza chaka sana. Mpaka wao wanaamua kutupiga mnada na Bandari zetu zote ila za kwao hawagusi huo si upuuzi 🙄😳. Ifike mahali tuchague serikali tatu au moja tu kuliko kuwa na muungano wa serikali mbili kuzaa serikali mbili.
 
Ubalizi ni hadhi. Ukiwa balozi si lazima uwe na kituo cha kazi ubalozini.

Watu kama Mkuu wa Itifaki Wizara ya Mambo ya Nje mara nyingi anakuwa balozi ambaye anafanya kazi Wizara ya Mambo ya Nje (rejea Balozi Joshua Opanga, Balozi Cisco Mtiro).

Kuna Makatibu Wakuu Viongozi wengi wamekuwa mabalozi bila ya kuwa na vituo vya ubalozi kwa maana ya kwenda kuwa mabalozi katika nchi. (Rejea Balozi Philemon Rupia)

Hadhi ya ubalozi inaendana na kupewa hadhi ya diplomatic immunity kimataifa, hii hadhi inawezesha watu kufanya kazi nyingine nyeti kwa niaba ya taifa.

Kwa hivyo, kupewa hadhi ya ubalozi si kazima uende kuwa balozi kwenye nchi fulani.
Asante
 
Katiba hii, Rais wetu akijisikia tu kumwagia mtu ma vyeo basi hakuna wa kuhoji.
 
Tuna muungano wa hovyo sana. Babu nyerere alituingiza chaka sana. Mpaka wao wanaamua kutupiga mnada na Bandari zetu zote ila za kwao hawagusi huo si upuuzi 🙄😳. Ifike mahali tuchague serikali tatu au moja tu kuliko kuwa na muungano wa serikali mbili kuzaa serikali mbili.
Kiuhalisia hakuna muungano, maana watanganyika hatuna haki kule Zanzibar. Ila wao huku wana haki asilimia mia .Yaani Mzanzibari ni Mtanganyika pia,ila Mtanganyika ni Mtanganyika pekee.Huu ni upumbavu.
 
Lakini Babu Nyerere hakuwa na lengo la muungano wa aina hiyo hata kidogo. Ni hawa wajukuu zake ndio wameyatengeneza haya kwa manufaa yao wenyewe kupitia kwenye chama chao cha CCM.
 
Ni hadhi. Mara nyingi Katibu Mkuu Kiongozi huwa ni Mabalozi hapo kabla.

Nadhani yeye pamoja na Dkt Bashiru ndiyo hawakuwa na Mabalozi. Hivyo Rais hufanya namna na kuwatunuku hadhi hiyo ya Ubalozi.

Hivyo anaendelea na majukumu yake kama Katibu Mkuu Kiongozi. Ila sasa atatambulika kama Balozi Dkt Moses Mpogole.
Kama katibu mkuu kiongozi anapaswa kuwa na sifa zenye hadhi ya kibalozi, ilikuwaje akapewa ukatibu mkuu kiongozi kwanza kabla ya kupewa ubalozi?

Yaani inakuwaje unavaa viatu kwanza kisha unavaa soski. Huo ni uwendawazimu.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
amefanya uteuzi wa Viongozi wafuatao kuwa na Hadhi ya Balozi kama
ifuatavyo:-
1. Dkt. Moses Mpogole Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi kuwa Balozi;

2. Dkt. Salim Othman Hamad, Msaidizi wa Rais anayeshughulikia
masuala ya Siasa kuwa Balozi; na

3. Dkt. Kassim Mohamed Khamis, Msaidizi wa Rais anayeshughulikia
masuala ya Hotuba kuwa Balozi.

Uteuzi huu wa Hadhi ya Balozi umeanza tarehe 12 Juni, 2023.
Aidha, Vyeo walivyonavyo vinabaki kama vilivyo.

Wateule wataapishwa tarehe 16 Juni, 2023 kuanzia saa 04:00 asubuhi - Ikulu,
Chamwino - Dodoma.
View attachment 2656278
Nini mantiki ya mtu (kiongozi) kupewa hadhi ya kibalozi pasipo kwenda kutumikia kazi ya ubalozi (kupangiwa ubalozi)?

Wanalipwa kuwa na cheo cha ubalozi bila kuwa na ubalozi?
 
Ila wao huku hadi ukuu wa wilaya wanapata.Hivi Nyerere kwa nini alikubali haya?Kweli Karume alikuwa kichwa,kumuingiza Nyerere mkenge namna hii jamani.

Kwa sababu alikuwa anapenda sifa za kimataifa kwamba ni mpinga ubaguzi, mjenga umoja. Hata jeshini aliacha wazungu watawale Waswahili. Siku moja Waswahili wakatokea Ikulu kuwatandika fimbo, wakakuta keshakimbia na Kawawa wake. Juzi Mama Maria amebainisha kwamba waliwaacha yeye na Sophia Ikulu. Kambona akaenda kuwapoza wanajeshi, Nyerere akaomba msaada majeshi ya Nigeria na Uingereza ndio akatoka kwenye shimo la uani Kigamboni huko.

Toka siku ile akapata fundisho, jeshini Wakurya tupu mpaka alipoondoka ndio jeshi lika diversify.

Kuna mjeshi wa JWTZ, within the inner most circle of the leadership brass, amenambia huu utopolo unaondelea nchini ingekuwa ni jeshi lenye mizizi ya Ufaransa, kama ya West Afrika, wangesha watemesha nyongo kitambo. Kwa saab wao wanafundishwa zaidi ulinzi na utii kwa nchi, sio kwa himaya.
 
Lakini Babu Nyerere hakuwa na lengo la muungano wa aina hiyo hata kidogo. Ni hawa wajukuu zake ndio wameyatengeneza haya kwa manufaa yao wenyewe kupitia kwenye chama chao cha CCM.
Unataka kuniambia haya ya Mtanganyika hawezi miliki ardhi Zenj ila mzenj ana haki ya kumiliki ardhi Tanganyika, unaona kina Karume wana nyumba Dar na Unguja. Hii ya vitambulisho kwa wazaliwa wa zenj,Kuingiza mizigo kutoka Tanganyika kwenda Zenj unalipa Kodi Zanzibar .Na mimi siwezi kuwa mbunge Zenj,wala kuwa Rais Zenj,ila wazenj wanahaki ya kuwa chochote wanachotaka huku Tanganyika. Haya yote yamewekwa enzi hizi?
 
Kwa sababu alikuwa anapenda sifa za kimataifa kwamba ni mpinga ubaguzi, mjenga umoja. Hata jeshini aliacha wazungu watawale Waswahili. Siku moja wakamtokea Ikulu kumtandika fimbo, wakakuta keshakimbia na Kawawa. Kambona akaenda kuwapoza.

Toka siku ile akapata fundisho, jeshini Wakurya tupu mpaka alipoondoka ndio jeshi lika diversify.

Kuna mjeshi amenambia huu utopolo unaondelea nchini ingekuwa ni jeshi lenye mizizi ya Ufaransa wangeshawa watemesha nyongo zamani. Wanafundishwa zaidi ulinzi na utii kwa nchi, sio himaya.
Wafaransa hawana ujinga wetu wa kibongo,viongozi wanawajua wananchi wao.Wananchi wakiamua ni hatari.Wafaransa walimchinja Louis wa 16.Hawataki mchezo.
 
hiyo ndiyo anayoiwezea, kudhibiti maadili na ufujaji wa mali za umma anakaa kimya....huko madaktari wanabaka wagonjwa haoni.....wameiba mali na dawa wamechoka wameanza kubaka wagonjwa sasa 😀 😡
 
Back
Top Bottom