Uteuzi: Watatu wapewa hadhi ya Ubalozi, yupo Katibu Mkuu Kiongozi

Uteuzi: Watatu wapewa hadhi ya Ubalozi, yupo Katibu Mkuu Kiongozi

Ila wao huku hadi ukuu wa wilaya wanapata.Hivi Nyerere kwa nini alikubali haya?Kweli Karume alikuwa kichwa,kumuingiza Nyerere mkenge namna hii jamani.
Yaani miaka karibia 60 ya Muungano leo ndio unayajua hayo ? Halafu unataka kuuchambua mkataba wa DPW ! Hahahaaa watanzania bana !
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
amefanya uteuzi wa Viongozi wafuatao kuwa na Hadhi ya Balozi kama
ifuatavyo:-
1. Dkt. Moses Mpogole Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi kuwa Balozi;

2. Dkt. Salim Othman Hamad, Msaidizi wa Rais anayeshughulikia
masuala ya Siasa kuwa Balozi; na

3. Dkt. Kassim Mohamed Khamis, Msaidizi wa Rais anayeshughulikia
masuala ya Hotuba kuwa Balozi.

Uteuzi huu wa Hadhi ya Balozi umeanza tarehe 12 Juni, 2023.
Aidha, Vyeo walivyonavyo vinabaki kama vilivyo.

Wateule wataapishwa tarehe 16 Juni, 2023 kuanzia saa 04:00 asubuhi - Ikulu,
Chamwino - Dodoma.
View attachment 2656278
Kwali hii zamu ya Zanzibar na waarabu kuula! Kati ya wateule watatu, Bara yenye asilimia 98 ya watanzania wote inaambua mmoja tu!
 
Wafaransa hawana ujinga wetu wa kibongo,viongozi wanawajua wananchi wao.Wananchi wakiamua ni hatari.Wafaransa walimchinja Louis wa 16.Hawataki mchezo.

Na nilikuwa sijui kwa nini majeshi ya Francophone Afrika hata sajenti na wenzake sita wana balls za kwenda Ikulu kulichekecha.
 
Na nilikuwa sijui kwa nini majeshi ya Francophone Afrika hata sajenti na wenzake sita wana balls za kwenda Ikulu kulichekecha.
Huko Marais hawalali usingizi, anytime coup d'état. Mfano Rais wa Guinea Conakry, ndo kwanza ndo alikuwa kashinda muhula mwengine.Akaondoshwa na Mwanajeshi aliyemteuwa mwenyewe.
 
Yaani miaka karibia 60 ya Muungano leo ndio unayajua hayo ? Halafu unataka kuuchambua mkataba wa DPW ! Hahahaaa watanzania bana !
Ninayajua,tokea nilipojitambua.Nilianza kuambiwa kwenda Zanzibar hadi uonyeshe ID.Kwa akili yako unafikiri ndo nimejua leo?G55 unawajua wewe ?
 
Yaani miaka karibia 60 ya Muungano leo ndio unayajua hayo ? Halafu unataka kuuchambua mkataba wa DPW ! Hahahaaa watanzania bana !
DPW muda utaongea, wenyewe watalaumiana.Kwani Bunge lililopitisha mkataba wa Bandari ya Bagamoyo Magufuli si alikuwemo?Ila alipokuwa Rais alisemaje?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
amefanya uteuzi wa Viongozi wafuatao kuwa na Hadhi ya Balozi kama
ifuatavyo:-
1. Dkt. Moses Mpogole Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi kuwa Balozi;

2. Dkt. Salim Othman Hamad, Msaidizi wa Rais anayeshughulikia
masuala ya Siasa kuwa Balozi; na

3. Dkt. Kassim Mohamed Khamis, Msaidizi wa Rais anayeshughulikia
masuala ya Hotuba kuwa Balozi.

Uteuzi huu wa Hadhi ya Balozi umeanza tarehe 12 Juni, 2023.
Aidha, Vyeo walivyonavyo vinabaki kama vilivyo.

Wateule wataapishwa tarehe 16 Juni, 2023 kuanzia saa 04:00 asubuhi - Ikulu,
Chamwino - Dodoma.
View attachment 2656278
Hizi hadhi za nini wakati wanafanya kazi zilezile hawaenda kuwakilisha nchi ubalozini. Watu weusi tunapenda sana title za ajabuajabu. Rais kwanini naye anashiriki kwenye mambo km haya?
 
Unataka kuniambia haya ya Mtanganyika hawezi miliki ardhi Zenj ila mzenj ana haki ya kumiliki ardhi Tanganyika, unaona kina Karume wana nyumba Dar na Unguja. Hii ya vitambulisho kwa wazaliwa wa zenj,Kuingiza mizigo kutoka Tanganyika kwenda Zenj unalipa Kodi Zanzibar .Na mimi siwezi kuwa mbunge Zenj,wala kuwa Rais Zenj,ila wazenj wanahaki ya kuwa chochote wanachotaka huku Tanganyika. Haya yote yamewekwa enzi hizi?
Ndiyo.
hayo yote uliyoeleza hapo hayakuwa ndivyo muungano uwe hivyo milele. Lengo la mwanzo lilikuwa ni kuondoa wasiwasi wa wachache kujihisi kuwa wamemezwa; sasa badala yake hao wachache ndio wameruhusiwa kuwameza wengi, kwa vile tu CCM inataka itawale milele.
 
Katibu Mkuu Kiongozi hakung'olewa, ameongezewa hadhi ya ubalozi juu ya cheo chake cha sasa.
Kuvuja kwa mkataba wa DP world hakutamuacha salama.

Anapelekwa ubalozini soon hiyo kupewa ubalozi ndio anatakiwa aanze kufungasha virago hivyo.
 
Back
Top Bottom