Uthibitisho: Mwigulu Nchemba ni majina bandia ila vyeti ni vya kweli

Mwigulu alifeli darasa la 7 akatumia cheti cha mtu aliefaulu darasa la 7 kujiendeleza. Kwahiyo ana cheti bandia na majina bandia.
Yeye anasema aliwahi kwenda hospital huko kijijini kwao wakati flani na clinical officer "akagoma" kuyaandika majina yake (too local...!?) then huyo officer "akambatiza" majina mapya, hayo anayotumia sasa.

Inawezekena kweli kwenye kila watu wanne kuna mmoja ni chizi maana ni Tanzania tu mtu anaweza kujitokeza kwa ujasiri kabisa akaongea hii kitu na watu wakamsikiliza na kukubali
 

Ni jambo la kushangaza sana
 
Bila cheti cha kuzaliwa lazima kuhoji uraia wa Mwigilu.
Kutumia majina bandia nalo kosa kwa sababu katika hali ya kawaida raia yeyeto anatumia majina yaliomo kwenye cheti cha kuzaliwa. Sijawahi kuona raia tena kiongozi wa taifa anatumia majina bandia.
 
Hapo ndipo nilipomshangaa hospitali kupoteza ubini wa mtu.
 

Mkuu pasco! wapi kwenye hiyo post yenye utetezi wa waziri, aliposema kwamba Nesi wake aliitwa kwa majina ya 'Mwigulu Nchemba'?!!!!
 
Mkuu pasco! wapi kwenye hiyo post yenye utetezi wa waziri, aliposema kwamba Nesi wake aliitwa kwa majina ya 'Mwigulu Nchemba'?!!!!
Mkuu KaiSikapeta, soma tena utetezi wake, usipopaona nitakusaidia.

Kila kitu kiko wazi kabisa, haiwezekani mtu
Upikiwe chakula
Upakuliwe kwenye sahani,
Uchotewe kwenye kijiko,
Ulishwe mdomoni, wewe kazi yako ni kutafuna tuu na kumeza.
Sasa unataka hadi utafuniwe, jaribu kutafuna mwenyewe kwa kusoma tena, ukishindwa kutafuna ndipo uje nitakutafunia, na hata ukishindwa kumeza, nitakumezesha.
Pasco
 
Mkuu naona kama hizi picha ni za watu wawili tofauti japo wote ni kina Faustine na kila kitu kinafanana utofauti ni picha ndo watu wawili tofauti au macho yangu?
Mkuu Musi, hilo ni kosa dogo la misplaced photos tuu yaani kuna picha zimechanganywa. Lakini Tangazo ni hilo hilo moja.
Pasco
 

Well, naomba kuuliza kwanza, hii message ulikuwa unataka iende kwa KaiSikapeta au KayScarpetta?
 
Cha kufanya ni kumtafuta yule kijana ambaye mzazi wake alishiriki kuuza jina ili aende mahakamani kudai haki yake.
 
Wandungu, hii PhD ya Mhe. Mwigulu ni uthibitisho kuwa huyu jamaa ni kichwa cha ukweli.

Hongera sana kwa shule nene ya kutoka chuo cha ukweli, UDSM.

Paskali
 
Wandungu, hii PhD ya Mhe. Mwigulu ni uthibitisho kuwa huyu jamaa ni kichwa cha ukweli.

Hongera sana kwa shule nene ya kutoka chuo cha ukweli, UDSM.

Paskali

Sijawahi kua na mashaka na mwiguli, alisoma na jamaa yangu akawa anasema alikua anapita ananyoosha vidole 3 juu akimaanisha div 1.3 form 6 ila bahati mbaya alipata II.10.
 
Mr Pasco huenda kweli Mwigulu jina siyo lake ni kweli , tusijifanye hatujui miaka ya nyuma watu walikuwa wanarudia shule zaidi ya mara mbili Kwa Kutumia majina ya watu na ukifuatilia watu wengi wasomi Wa miaka ya 2004 kurudi miaka ya nyuma majina walionayo wengi siyo ya kwao, Pili miaka ya nyuma primary hapakuwa na pastort kwenye vyeti Kwa hiyo ilikuwa ni rahisi sana Kwa mtoto Wa maskini kuchukuliwa jina lake Na mtoto Wa Taita , Hayo ndo yapo Kwa akina Bashite na Mwigulu.Lakin Kwa leo hii ni vigumu kutumia cheti cha MTU mwingine kutokana na utaratibu ulioopo.
 
Dr.Mabuga, sio huenda, hayo ni majina ya given names tuu, hakuna ubaya wowote mtu kuwa na given names hata mia, ila kwenye every official communications, cheti cha kuzaliwa, kuandikishwa hospitali, kuandikishwa shule, kuomba passport lazima kuwe na majina ya baba na jina la ukoo, katika majina hayo, hakuna jina la mzazi, wala la ukoo, hivyo hayo ni majina bandia ila sio majina ya kughushi, hajaiba jina la mtu, wala nafasi ya mtu, darasani ameingia yeye Mwigulu mwenyewe, kuhudhuria masomo mwenyewe in person, kufanya mitihani na kufaulu kwa majina hayo hadi sasa ni Ph.D holder, hivyo he is very genuine learned person unlike Bashite na Dr. Kigwa, mmoja alifeli la saba akatumia nafasi ya mtu mwingine aliyepasi anashindwa kulipia, na Bashite alizungusha form 4 pale Pamba, akatumia jina na vyeti vya mtu mwingine kujiendeleza.

Jina is not a big issue mtu unaweza kuapa tuu na kubadili, muhimu ni elimu na vyeti halali, elimu ya Mwigulu ni elimu halali na vyeti vyake ni vyeti halali.

Paskali
 
Hata aruke sarakasi ajuazo ukweli elimu kakomaa yeye mwenyewe sehemu kubwa.
Lakini huku chini msingi akumbuke jina alilotumia kwa kununua kwa ngombe tisa na biashara ikaisha na mwenye jina hana tatizo maana kachukua chake.
Utaratibu huu ulikuwepo huko nyuma na wengi wameutumia kwenda sekondari. Ikiwa serikali ikiamua kufanya follow up hapa nusu ya watumishi twaweza kuwakosa.
Mwigulu yuko sahihi kueleza hayo ni ujasiri maana wazungu husema being silence means yes. Sasa ikiwa atakaa kimya mtajua ni kweli. Kujitokeza ni ishara ya kukataa hata kama ni kweli.
Yeye kalitendea jina haki kwa kusoma na kufaulu but kuna ukakasi mkubwa kwa majina yake.
Hakuna dhambi ndogo zote ni sawa, nashauri serikali iwalipe pensheni zao wale iliowatumbua maana hizo hela zipo na waliozikalia wengine wana majina sahihi ila elimu feki n.k.
Haya yamejadiliwa sana humu kuhusu mwigulu wapo wanaomjua sawasawa walileta post humu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…