Uthibitisho: Mwigulu Nchemba ni majina bandia ila vyeti ni vya kweli

Sasa si alishasema kuwa alikaa nyumbani miaka miwili kuchunga ngombe?
Ina maana aliporudi aliendelea na jina la mtu mwingine
 
Mkuu Mahanju, Mhe. Mwingulu Nchemba ni verified member humu na trusted source hivyo alichosema humu ndio ukweli wenyewe halisi. Wewe ndio unadanganya.
Pasco
Ni ukweli wake na sii lazima uwe ukweli halisi.

Pasco lihurumie taifa acha kumshabikia mwongo.
 
mmh,kasema jina alipewa akiwa na siku saba.

kwa maana hiyo aliitwa tangu akiwa mtoto.

tena anasema baada ya kuambiwa arudi shule baada ya kuacha aliamua kuchukua jina la daktari.

iweje achukue jina ambalo alikuwa nalo tangu akiwa na siku saba?.
tena majina mawili yote,mmh.

anatakiwa aseme kuwa alitumia jina lake lingine ambalo hata akiwa anasoma na alipoacha alikuwa nalo na kuna watu waliomuita hilo jina.

anaposema alichukua la daktari alipoacha,je lile ambalo alipewa akiwa na siku saba ni lingine?.

pia hajasema akiwa darasa la kwanza hadi alipoacha alikuwa anatumia njina gani!!!
 
Nafikiria tu saahizi Paskalii angekuwa NDO msemaji wa pale jumba jeupe kupitia kambi ile ya KUZUNGURUSHA
Mkuu Yohana Mbatizaji utakuwa hujui. Mimi namfahamu Paskali vizuri sana kwa sababu mimi na yeye ni mapacha wa tumbo moja. Msemaji wa pale alikuwa awe ni yule jamaa wa Mtanzania, msaidizi wake ni huyu jamaa wa DW aliyepo, Paskali yeye angekula tuu tenda za production ya vipindi vya TV kupitia kampuni yake ya PPR.
Pasco
 
pasco kama kuna jina bandia basi kuna vyeti feki.,, yeye anatoa historia ya kuzaliwa utadhani alikuepo wakati hsyo matukio ya kuzaliwa na majina aliyopewa kama umesoma Topic moja inaitwa Logic kwenye hesabu sentensi zako nikiunganisha majibu yaleta uwongo na majibu ya mwigulu pia ni uwongo..
 
Yaani hivyo tu. Na wewe umeridhika.
 
Huja address swali langu kwa nn MTU ana opt Ku acha kutumia majina yake sahihi anatumia bandia? Anaficha nn? Na hayo majina bandia na kiuhalisia ni ya nani au yamepatikanaje?? Mimi ni Osokoni naona umeshanipa jina bandia Mkuu Pasco
Mkuu Osoko, as long as hakuna kosa lolote la jinai kutumia jina lolote, then mtu yoyote yuko huru kutumia jina lolote kujiandikisha popote, ila cheti cha kuzaliwa, kuandikishwa shule, passport na Nida lazima utumie majina halisi ya wazazi, hivyo tusimsakame Mhe. Mwigulu Nchemba , nendeni immigration mkaone DN data zake au Nida.
Pasco
 
Mkuu nazidi kuwa na mashaka, haiyumkini account yako imedukuliwa.

Maelezo ya mtuhumiwa unaya classify kuwa ya kweli kwa sababu amesema hivyo!!!!?

Hawa watu "hata kama wanaongelea gizani" (anonymity) wanapaaza sauti kusema "MNADANGANYWAAAA" unapendekeza tukubali tu maelezo rahisi ya "verified user"????

MUNGU ALIMTIMUA SHETANI MBINGUNI, MAANA HAKUNA NAMNA UTAFANYA USHETANI KISA UKO MBINGUNI.

Verification of username haitakuwa na maana kama muhusika anashindwa ku clear tuhuma inayomkabili ya kutudanganya kama taifa.

Amefanya mtihani wa darasa la saba mara mbili kwa manufaa yake!!?
 
Kwanini MTU atumie jina bandia wakati cheti ni sahii acha wehu wako toa mantik hapo ili uajiliwe serikalini nilazima elimu yako ijulikane sasa hapo alitumia jina bandia kwa sababu gani
 
Hilo ndio swali ninalotaka Pasco alijibu.
Mkuu Kisu cha Ngari, nimelijibu hili mara kibao kuwa kuna majina ya aina tatu
1.given names
2. Middle names could be la ubatizo la la mzazi
3. Surname or family name, jina la ukoo.
Bandiko la Mwigulu ameonyesha majina ya Mwigulu Nchemba ni just given, hakuna kosa lolote kutumia given names popote hadi kwenye vyeti, bungeni hadi kwenye passport ila kwenye fomu za kuandikishwa shule majina ya wazazi yapo. Kule Immigration kuna DN file yake yenye majina halisi ya wazazi wake na Nida pia.

Kwa vile hakuna mwenye majina yake ya kuandikishwa, mwenye DN yake au kule Nida kuonyesha wazazi wake ni nani, akikutwa kule amedanganya hapa ndio tutasema mengine ila hata ilitokea akawa amedanganya bado kuna bonge la caveat ya kijana fulani Banyamulenge wa Kihaya kwa jina la Katto.
Pasco
 

Umelonga mkuu!
 
Pasco umetumia criteria gani kusema majina ni universal? Embu Fanya utafiti kuhusu wanaume Wa Java (Indonesia), mbona hawana jina la baba wala ukoo only one given name eg
Suharto
Sukarno
 
pasco eti tena veryfied user humu hawezi kudanganya kama amedanganya kwenye vyeti atashindwa kudanganya Jamii Forum hili nalo linahitaji Elimu kujua kwa mtu aliesoma shule na akafauru vizuri hawezi kutetea majina feki na vyeti bandia kwamba kimoja kipo sahihi kimoja hakipo sahihi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…