Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Hongera sana mkuu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Subiri na ww uwe na hela mkuu, maskini hua tunaona na tuna ideas nyingi sana, ila tukishaikamata pesa sijui akili huwa inakwenda wapi..
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu napendekeza ww usaidike mana hata kuna uzi wako unaelezea hii biashara ua so real ,,
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Subiri na ww uwe na hela mkuu, maskini hua tunaona na tuna ideas nyingi sana, ila tukishaikamata pesa sijui akili huwa inakwenda wapi..

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana mkuu mimi sidhani kama naweza kujiingiza kufadhiri mitimu,kufadhiri timu hizo sifa tu mtu anatafuta lakini hakuna maana yoyote mkuu. Tena mo ndio kabisa wafanyakazi kwenye viwanda vyake wanafanya kazi ktk mazingira kwa muda mrefu bila kupumzika,ujira kidogo,huku upande mwingine ukimwaga mihela isiyo na maana yoyote kwa timu. Angalau bakhresa wafanyaka kazi wanafanya kazi kwa kufuata sheria za kimataifa,wanalipwa vizuri. Jiulize wewe ni bilionea una viwanda,lakini unapoishi tu wanaokuzunguka kuna masikini wa kutupwa,anza na wao,kama sio kuwaajiri wawezeshe kwa namna yoyote hata anza nao mafunzo ya ujasiliamali. Badae kamtaa kote mnakuwa mko vizuri japo hamuwezi kuwa sawa,lakini vijumba vya kubumba vinaondoka mtaa wote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sorry mkuu location ya izo ndizi mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimecheka sana hapa
Umenikumbusha jamaa yangu aluyeua duka mtaji wa Viatu kwa issue ya mikeka.
Ila nimependa ulivyojitetea chini
 
Nina Hotel ambayo inatoa huduma ya Chakula Ila hakuna Vinywaji asilia na Bahati nzuri jirani yangu ambae pia Ni rafiki yangu ana deep freezer. Niazime hiyo Elfu hamsini Ninunue Blender ya sh.45,000 Matunda ya 3000 na Sukari Nusu pamoja na Viungo vingine nitengeneze Juice hapa niuze Glass Moja 500, ambapo kwa Matunda hayo ninauwezo wa kupata Vikombe 20 kwa wastani jumla inakua 10,000, nikiwekeza faida 2500 kila siku huku 2500 ingine nakuza Mtaji nitakua na uwezo wa kuirudisha hiyo Pesa in two weeks. Kwa sababu za kiusalama Namba sitaweza kuweka Ila Kama utapendezwa PM yangu ipo wazi.. Natanguliza shukrani.
 
Safi
 
Naunga mkono hoja MaBillionaire ni watu wa hovyo kabisa.

How come, MO ana utajiri wa Trillion 4 roundly hivi akitenga only 1B tu sawa na million 1000/= akawawezesha vijana kwa vigezo purposefully 1M kila mmoja sawa na vijana 1000 Tz kwa 1B moja tu ambayo haitekenyi hata itajiri wake Hell.

Hell.

Portfolio | 2020
 
Elfu 50 nitaitumia kufanya betting kwa nidhamu ya hali ya juu, kila siku nitakua natafuta odd za uhakika jumla odd 1.5 kwa siku, naamini kuanzia hiyo tarehe 21 Ijumaa kunakuwa na team za uhakika na odd ya 1.5 ni rahisi sana kwangu kupata. Then Jumanne asubuhi nakurushia hiyo 50k yako uendelee kusaidia vijana wengine.
 
Akifanya hivyo atateka mioyo mingi ya watanzania, na wengi watatamani awe hata rais yao, hapo ndo shida itakapoanza na watawala au politicians, hakuna serikali inapenda raia wa kawaida awe na msaada kuliko serikali yenyewe hasa hizi serikali za Africa..... Yani ni sawa leo Mo asifiwe na kila mtanzania kuliko Jiwe....
 
Kama nakuelewa vile
Naamini na pyupyu zitamwandama
 
Hakuna tajiri mwenye dhamira ya kumkomboa masikini maana umasikini wetu ndiyo utajiri wao.
Ndiyo sababu wako tayari kutapanya pesa ovyo (kuwalipia viingilio uwanjani, kudhamini team mnazozipenda n.k) lakini si kuwekeza kwenye sekta zitakazowagusa moja kwa moja kiuchumi.
Kwa tajiri kumuwezesha masikini ni kujibomoa mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahahahaha, kweli nimeamini kubet ni ugonjwa. Nimelipenda wazo lako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wazo zuri, unaonekana una nia lakini muhusika wakutoa mitaji kapita wimaa!
labda ajaisoma hili wazo lako, tusubirii
 
Mkuu hongera mno kwa kupewa uono wa jicho la fursa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…