Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Hiyo 50000 naenda mnadani napoint handbag Kali za mtumba kila moja Bei 10000. Napata pochi Tano nazipiga picha safii natupia insta kwenye fekero langu la udaku kila moja 25000X5 napata 125000. Hizo nauwakika ndani ya week zimekwisha .

Naelewa hii biashara inalipa nishaifanya Sana ila Sasa nimeacha muda wa kupoint Sina inabidi udamke alfajir sana
 
Mkuu kama kweli upo serious, elfu 50 unashindwa kuipata hata kwa ndugu au rafiki?
Hiyo elfu 50 mchanganuo, wake kwa biashara ya mishikaki.

Naenda kwa Fundi kuchomelea aniandalie Jiko elfu 25,

Natafuta kijiwe kizuri sehemu wanayopita watu wengi,

--Sokoni nyama kg 2 steki tupu =16000,
--mkaa wa 1500
-Viungo vyake 5000(hiyo siyo vya siku moja ukinunua ni vingi mpaka viishe vitakaa kaa kidogo. )
-vijiti vile vistiki vyake 2000.

Naandaa mishikaki yangu ya wastani tu ya kuuza mia 2 mia 2 tu,

Kwenye kg 2 nina uhakika wa kupata faida ya 10K kila siku hapo baada ya kutoa matumizi ya mkaa, vijiti na Nyama.

Ndani ya wiki tayari nimekurudishia 50k yako.

NB:
Nilishawahi kufanya hii kazi hivyo nina uhakika nayo. Ndio kazi iliyonipa mtaji wa kibanda cha kuchakata viazi kuwa Chips.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera mkuu. Huo ndio ubinadamu. Ingekuwa wale wenye mitaji mikubwa wangewafanyia hivi wengine Tanzania ingebadirika haraka sana. Huwa najiuliza sana mtu kama mo au bakhresa kwa nini asikopeshe wenye kutaka biashara lakini hawana mitaji?.

Kuliko kufadhiri litimu kama simba wanakula hela tu tena nyiiingi sana ukipiga hesabu kwa mwaka. Lakini hakuna faida yoyote wala muendelezo wa hizo timu,zote zinashindana kushindana zenyewe tu na kuishia hapa hapa.

Lakini kwa wazo kama hilo wangekuwa wanawakopesha watu hata kwa liba ndogo tu hata iwe 3% ya kuilinda tu ile hela. Hongera sana mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo wakianza kukopesha inabidi hiyo huduma waisajili,lasivyo unaweza ukafilisiwa (binadamu ni kinyonga)
 
Hiyo elfu 50 mchanganuo, wake kwa biashara ya mishikaki.

Naenda kwa Fundi kuchomelea aniandalie Jiko elfu 25,

Natafuta kijiwe kizuri sehemu wanayopita watu wengi,

--Sokoni nyama kg 2 steki tupu =16000,
--mkaa wa 1500
-Viungo vyake 5000(hiyo siyo vya siku moja ukinunua ni vingi mpaka viishe vitakaa kaa kidogo. )
-vijiti vile vistiki vyake 2000.

Naandaa mishikaki yangu ya wastani tu ya kuuza mia 2 mia 2 tu,

Kwenye kg 2 nina uhakika wa kupata faida ya 10K kila siku hapo baada ya kutoa matumizi ya mkaa, vijiti na Nyama.

Ndani ya wiki tayari nimekurudishia 50k yako.

NB:
Nilishawahi kufanya hii kazi hivyo nina uhakika nayo. Ndio kazi iliyonipa mtaji wa kibanda cha kuchakata viazi kuwa Chips.

Sent using Jamii Forums mobile app
Safi ukipata uendeleze biashara
 
Sio kwamba unataka kuiba wazo la watu? Kama ulichoandika ndio nia yako hongera sana maana hata wenye mitaji lakini ni wavivu wa kufikiri watafaidika

Precisely my thought. Yale yale ya Kusaga aliemwendea Mengi na wazo la kuanzisha kituo cha radio na television mangi akaanzisha yeye kwa kutumia wazo hilo hilo.
 
Back
Top Bottom