Analyse
JF-Expert Member
- Jan 19, 2014
- 17,637
- 47,413
Kwa pale Dar es salaam maeneo ya mnazi mmoja, kuna vile vitenge huwa vinakaa viwili viwili, bei wanauza pair kwa Tsh 7,000/=. Ila vitenge hivyo hivyo, ukienda mikoani wanauza pair Tsh 10,000/=. Lakini, mikoani humo humo ukiingia mitaani, wanauza pair Tsh 15,000/= (na wa mitaani hawanunui nje ya mikoa yao)
Kwahiyo 50,000/= unayotaka kutoa, zitapatikana pair 7,ambazo zitagharimu 49,000/=. Itabaki 1,000/=
Kutakuwa na mjomba, dada, kaka au shangazi wa kuweza kuongezea 5,000/= katika buku iliyobaki, so jumla itakuwa 6,000/=. Mzigo ukishapatikani, hautotumwa kwa njia ya bus, wale ni gharama, parcel ya namna hiyo haipungui 10,000/=,utaupeleka pale kidongo chekundu, kuna mawakala wa kusafirisha mizigo kuja mikoani, kwavile wanabeba mizigo mingi, huu hauzidi 5,000/=. Ukiuagiza siku hiyo, utakufikia kesho yake.
Ukishaupokea, uza pair moja mitaani kwa Tsh 13,000/= ( hapa utawapiga bao wanaouza 15,000/=). Kwavile huna frame wala duka, wapitishie wale unaofahamiana nao kwanza. Watakaochukua kwa mkopo walipe ndani ya wili mbili ila wao wafanyie 14,000/= kwa pair.
1. Ikitokea zote umeuza kwa cash utapata 91,000/=. Ukitoa gharama za mtaji (50,000/= + 5000/=) unabaki na 36,000/=. Inamaana ndani ya mwezi unaweza kuagiza na kuuza vitenge vyako kwa mara mbili au zaidi kutegemeana na uchangamfu wako.
2. Ila kama umeuza kwa mkopo, maana yake utaingiza 98,000/=,ukitoa gharama za mtaji 55,000/= ,unabaki na 43,000/=. Hapa ndani ya mwezi utaagiza na kuuza mara mbili tu, maana mkopo ni wiki mbili.
Njia zote mbili ukiwa makini ndani ya mwezi u arudisha 50,000/= uliyoazimwa na unabaki na kiasi kizuri cha kutosha kuendeleza biashara.
Na ili biashara isizorote, kila mzigo unaochukua, unajiwekea idadi ya pair za kutoa mkopo na idadi ambazo zitakuwa cash.
N.B
1. Sihitaji huo mkopo, ila nimeshare ili wazo kwa yule dada/kaka anayehitaji huo mkopo ilihali hana uhakika wa kitu gani afanye ili kukuza huo mtaji. Au yule ambaye kila siku amekuwa akifiiria kitucha kufanya ila changamoto zimekuwa nyingi.
2. Hii biashara wateja ni jinsia zote, maana wengi ununua na kushonesha nguo.
Kazi kwenu.
Niite Analyse
#Baharia_nchi_kavu.
Sent using Jamii Forums mobile app