Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Kwa pale Dar es salaam maeneo ya mnazi mmoja, kuna vile vitenge huwa vinakaa viwili viwili, bei wanauza pair kwa Tsh 7,000/=. Ila vitenge hivyo hivyo, ukienda mikoani wanauza pair Tsh 10,000/=. Lakini, mikoani humo humo ukiingia mitaani, wanauza pair Tsh 15,000/= (na wa mitaani hawanunui nje ya mikoa yao)

Kwahiyo 50,000/= unayotaka kutoa, zitapatikana pair 7,ambazo zitagharimu 49,000/=. Itabaki 1,000/=

Kutakuwa na mjomba, dada, kaka au shangazi wa kuweza kuongezea 5,000/= katika buku iliyobaki, so jumla itakuwa 6,000/=. Mzigo ukishapatikani, hautotumwa kwa njia ya bus, wale ni gharama, parcel ya namna hiyo haipungui 10,000/=,utaupeleka pale kidongo chekundu, kuna mawakala wa kusafirisha mizigo kuja mikoani, kwavile wanabeba mizigo mingi, huu hauzidi 5,000/=. Ukiuagiza siku hiyo, utakufikia kesho yake.


Ukishaupokea, uza pair moja mitaani kwa Tsh 13,000/= ( hapa utawapiga bao wanaouza 15,000/=). Kwavile huna frame wala duka, wapitishie wale unaofahamiana nao kwanza. Watakaochukua kwa mkopo walipe ndani ya wili mbili ila wao wafanyie 14,000/= kwa pair.

1. Ikitokea zote umeuza kwa cash utapata 91,000/=. Ukitoa gharama za mtaji (50,000/= + 5000/=) unabaki na 36,000/=. Inamaana ndani ya mwezi unaweza kuagiza na kuuza vitenge vyako kwa mara mbili au zaidi kutegemeana na uchangamfu wako.

2. Ila kama umeuza kwa mkopo, maana yake utaingiza 98,000/=,ukitoa gharama za mtaji 55,000/= ,unabaki na 43,000/=. Hapa ndani ya mwezi utaagiza na kuuza mara mbili tu, maana mkopo ni wiki mbili.

Njia zote mbili ukiwa makini ndani ya mwezi u arudisha 50,000/= uliyoazimwa na unabaki na kiasi kizuri cha kutosha kuendeleza biashara.

Na ili biashara isizorote, kila mzigo unaochukua, unajiwekea idadi ya pair za kutoa mkopo na idadi ambazo zitakuwa cash.

N.B

1. Sihitaji huo mkopo, ila nimeshare ili wazo kwa yule dada/kaka anayehitaji huo mkopo ilihali hana uhakika wa kitu gani afanye ili kukuza huo mtaji. Au yule ambaye kila siku amekuwa akifiiria kitucha kufanya ila changamoto zimekuwa nyingi.

2. Hii biashara wateja ni jinsia zote, maana wengi ununua na kushonesha nguo.

Kazi kwenu.

Niite Analyse

#Baharia_nchi_kavu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabisa mkuu,yaani hata utajiri wako hautikisiki hata robo. Katika hiyo pesa kidogo tu kutoka kwako unakuwa umetengeneza vitu vingi kwa wakati mmoja,kwanza unakuwa umetengeneza matajiri,ambao nao wanaenda kutengeneza wengine,vile pesa inakuwa imesambaa kwa wengi,kwa hiyo na wengine wataipata. Vile vile utaheshimika kwa kukulinda sio kama hawa matajiri wetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mo Hana ule wito Kama wa kiongozi wa Malaysia mo mahathir,
Unapotezaji mabilion kufadhili sector Kama hiyo isiyo na shukrani?
 
Bado natmrudia hapo hapo mshukuru Mungu kwa kukupa jicho la 3 la kuona fursa na ikafanikiwa kuna wanaoteseka sana tena sana na wanaacha kazi wanajitahidi kwenye biashara wanafail kila biashara wanaamua kurudi kwenye ajira

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pumzika kwa amani mzee mengi alikuwa msaada sana kwa watu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pumzika kwa amani mzee mengi alikuwa msaada sana kwa watu

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajua mkuu,hakuna kitu kibaya sana wewe ni bilionea lakini unaishi katikati ya watu masikini sana. Hata hawa matajiri sana unafikiri wana amani hapa Tz?. Ndio maana wanajaribu kutupumbaza kufadhiri kwa pesa nyiiingi hivi vilabu vya mpira tunavyovipenda,ili kujaribu kutafuta uungwaji mkono hata kiasi fulani wa wananchi. Lakini hawana amani hata ya maisha yao. Ndio maana wanachuma humu lakini pesa wanahifadhi nje. Ni hivyo hivyo hata kwa wanasiasa wanaojilimbikizia mali nyingi bila kujali hali za wananchi huko. Ndio maana wengine wanasiasa wakistaafu tu wanaanza kuongea lugha tamu tamu kwa wananchi ili kujaribu kupata huruma huko mitaani kwa wananchi wanakoishi nao. Yaani mfano ikatokea hao mabilionea wetu mmojawapo anaunguliwa na nyumba,unafikiri nini kitatokea kwa wananchi? Badala ya kumsaidia kuzima moto,watakuwa wanafanya juhudi kubwa kubomoa ili wapate kilichomo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mchanganuo wa 50,000/=

Biashara ya supu ya utumbo,mapupu na vitu vingine vya ndani.

Mahitaji
-Sufuria kubwa (Lipo)
-Jiko (5000)
-Utumbo + mapupu+ nyama (25,000)
-Vibakuri + Vijiko(6000)
-Viungo (3000)
-mkaa (3000)
-benchi la kukaa 8000/=

Location;Msamvu Morogoro (stendi)

Wateja; bodaboda, wapiga debe na wengineo

Bei ya kila bakuri la supu 1000 na unaweza kupata zaidi ya bakuli 80 kwa nyama ya 25,000/= (1000×80=80,000/=)kwa siku na faida ni 30,000/=

Ndani ya siku mbili Hela yako inarudi na unabaki na faida

Please!Naomba hiyo 50,000/= niifanyie kazi

Ahsante.
 
Ninaomba mheshimu wazo langu.


Binafsi hiyo pesa ni nyingi sana kwangu.
Wazo langu ni hili:


Hapa ninapoishi ninaishi na traditional societies ambazo kwa kawaida hupenda burudani ambazo pia ni traditional.
Pahali hapa huwa pana makutano ya maelfu ya wanajamii mara nne kwa mwezi na ni mazingira ya wengi wao kupata pesa na kufanya starehe za kijadi kila kutano.
Nimeitafiti hali hii nikaona ninaweza kuifanyia mradi na mradi ule ukawa na tija na endekevu.
Mimi nitajikita kutengeneza pombe ya kienyeji aina ya 'wanzuki'.
Kwa makadirio ya chini,nitaanza kwa kutengeneza chupa mia mbili tu zenye ujazo wa lita moja kila moja.
Kwa hivyo nitahitaji maji kiasi cha dumu za lita ishirini 20 na ambazo kila ndoo itanigharimu shilingi 200 hivyo kufanya hesabu kuwa 20×200=4000.
Nitahitaji sukari kilo 10×2400=24000
Majani ya chai pakti 4×500=2000
Hamira kopo 2×1500=3000
Kuni mizigo(fungu) 5×1000=5000
Kopo za maji tupu 200×50=10000
Fegi za kianzio pakti moja 1×1500
Nabaki na chenji jero.

Matokeo sasa:
Kila chupa moja naiuza Tshs.500 tu!
Kwa hiyo kumbe ni 500×200= Tshs.100,000. Ukiichukua sasa hiyo 100,000 ukaizidisha kwa vipindi vinne vya makutano ya mwezi mmoja hesabu itakuwa
100,000×4= Tshs.400,000!
Kila senti inazaa senti×senti.
The CHEMISTRY is my Intellectual property.
I CAN DO IT!
Nipe msimamo wa ligi boss.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Saafi kabisa
Kitochi Original
 
Wazo zuri ,hivi wanzuki SI Ni jamii ya beer ile?
 
Mmetisha.
Nimeamini kama serikali ingeamua kuwaunga mkono vijana umaskini ungekimbia nchini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…