Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Naamini mwaka1993 ama ulikuwa na umri wa miaka 3 au zaidi kidogo ya hapo lakini si zaidi ya miaka 5.
Unadhani chanzo cha uhasama wa IPP Media na Clouds Media ni nini?

Nadhani enzo hizo Mengi akiwa ni mwenyekiti na Managing Partner wa Coopers & Lybrand hapa Tz wewe ulikua bado uko kiunoni.
 
Akifanya hivyo atateka mioyo mingi ya watanzania, na wengi watatamani awe hata rais yao, hapo ndo shida itakapoanza na watawala au politicians, hakuna serikali inapenda raia wa kawaida awe na msaada kuliko serikali yenyewe hasa hizi serikali za Africa..... Yani ni sawa leo Mo asifiwe na kila mtanzania kuliko Jiwe....
Bhakhresa ni Capitalist hawezi kufanya hivyo.
 
Mimi natafanya mobile shoe shine.

Nanunua brashi mbili 2000.
Rangi ya viatu nyeusi 2000.
Darktan 2000.
Rangi nyingine. 2000.
BEGI la kubebea zana 10000.
Sabuni ya kuoshea. 2000.
Sindano 2 za kushonea. 600.
Kisu cha kukatia Uzi. 1000.
Perfume ya viatu 5000.
Nauli 3000.
Chakula. 2000.
Kandambili za kuvaa WATEJA pair 2=4000.
Chupa ya maji ya kuoashea natoka nayo home.
Kazi hii naifanyia mjini kwenye maofisi na maeneo ya vyuo nasafisha na kung'arisha viatu vya WATEJA wangu kwa ustadi na unadhifu mkubwa sana.

Huduma.
~kubrashi viatu sh 2000/=
~ kushona kiatu Sh 1000/=
~ kuzungushia Uzi kiatu kizima sh 1500/=
Lakini bei itategemea na mteja gani na muhudumia....nitakuwa na Bango langu navaa limeandikwa shoe repair/FUNDI viatu .....lengo nikueleweka kwa wageni na wenyeji na pia watu wawe smart muda wote wawapo mjini/makazini.
Jumla ya mtaji wangu ni 35,600/=, 50,000-35,600=14,400 hiyo ni ya kuongezea zana zingine na dharura mbalimbali.
Nikibrashi viatu 10 kwa siku,10×2000=20,000.
Au nikishona viatu 10 kwa siku.
10×1000=10,000.
Kwa mwezi 10000×30=300,000.
Kwa wiki 10000×7=70,000 .pia hesabu ya
20,000×siku 30=600,000/kwa mwezi.
Kwa hiyo ndani ya wiki 20,000×7=140,000,nakuwa nnimerudisha pesa yetu 50,000.
 
Zali liwe upande wangu wakuu..natanguliza shukrani za dhati.

Uzoefu wangu ni biashara ya kupoint viatu/kazi za watoto wazuri hapa town..mapema niko karume nachukua mzigo ...baada ya hapo naenda mwenge nasafisha viatu vyote na kuviset vikae mkao

Karume nalenga kiatu Tsh 2000,3000 mpaka kwa 4000..kulingana na huo mtaji siwezi kuchukua vya bei ya juu zaidi..hapo uhakika wa kulenga pair 15 na chenchi ya nauli pamoja na kandoro inabaki ..japo nikinunua bei ya juu ndivo nitakavyopiga zaidi bei ya juu zaidi ..

Soko langu kubwa ni madada duu wa vyuo ,saloon na Hawa namba zao zote ziko on my phonebook...kinachofanyika natupia status mteja akifika bei tunafanya Kazi....bei ya mwisho ya viatu vya bei hizo nauza ten....ila mrembo akilia lia namuachia kwa elfu nane....usisahu kuna wale unawalenga parefu wanato noti bila maelezo....pia unaangalia muonekano wa Mteja unamlengaje hivyo hakuna bei maalum ya kuanzia..

Baada ya kutupia status naenda kwenye kila goli la msela naacha pia kadhaa kwa kila msela na nampanga bei yangu ninayotaka....hata uwe na gundu vipi kwa siku hukosi kuuza pia kuanzia Tatu na kuendelea ....nafanya hivi kwa sababu ya umembers na pia kutokuwa na goli langu Mwenyewe

Ukiuza pair moja kesho una uhakika wa kuzimua mzigo wa pair Tatu...kwa sisi wakuu wa hizi kazi tukiona hali ni ngumu tunaforce kwa kutembezea raia wa kwenye mafrem yote ya sinza ..hapo hukosi kusuma pia tano mpaka kumi...

Ukiwa na mzigo mkali uhakika wa kumaliza mzigo upo % ..mkuu chekecha hiyo pesa ndani ya mwezi huu narudisha nikiwa nimeshave mtaji wa kilo na nusu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari Mkuu

Mimi nitaitumia 50000/= katika mchanganuo ufuatao kupitia biashara ya mahindi ya kuchoma

Naishi temeke stereo jirani na soko hapo wanauza mahindi mabichi nami ndiyo biashara niliyowah kuifanya Tandika sokoni

Mchanganuo
Mahindi 50@300= 15000
Usafiri = 500
Mkaa. = 1500
Chumvi. = 300
Ndimu. = 300
Ushuru. = 500
Pilipili. = 300

JUMLA. 18900


MAUZO

Nitauza mhindi 1 kwa shilingi 800 hiyo kwa mahindi 50 kwa siku n shilingi ( 50×800= 40000)

jiko ninalo hivyo sihitaji kununua

JUMLA YA MAUZO - JUMLA YA MCHANGANUO.


40000 - 18900= 21100

kwa hyo ninauhakika wa kurudi na elfu 21100 kila siku kumbuka situmii nauli kurudi nyumbani

Ninauwezo wa kuuza mahindi 50 kwa sababu Tandika n sehemu ambayo inawatu wengi ni soko kubwa hvyo mwingiliano wa watu ni Mkubwa

Baada ya siku 7 ninauwezo wa kuwa na shilingi 147700

Pia kumbuka katika elfu 50 ya mtaji baada ya matumizi ya siku ya kwanza ilibaki (50000-18900= 31100) itabaki shilingi 31100 nitaitumia kuongeza mtaji taratibu kwa siku zinazofuata maana biashara sio siku zote huwa nzuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wazo bora sana hili kwa kijana mwenye uthubutu hii n biashara yenye faida sana hasa kwa maeneo yenye watu wengi nimefanya hiii biashara naifahamu iliponifikisha haihiitaji aibu biashara hii inabid utoe ubrazamen
WAZO BORA KWANGU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo 50000 inatosha kununua mikungu miwili ya mdizi mzuzu kwaajili ya kuuza mnadani siku ya nyama choma ambayo hufanyika huku kwetu kila Jumamosi Mkungu mmoja unandizi 200, ndizi ikishachomwa au kukaangwa inauzwa 300 so hapo mkungu mmoja ninauhakika wa kupata minimun 40000 , kwa mikungu miwili uhakika wa 80000 then nikitoa mtaji 44000 + 2000(nauli ya kufata mzigo sokoni) jumla 46000. Kwahiyo 80000 - 46000 = 34000 ( Faida ya jmos moja) X jmos 4 = 136000 ( Faida kwa mwezi ) note: mtaji hubaki pale pale mikungu miwili ya ndizi kila wiki inatosha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WAZO HILI HAPA

Kwa mtaji wa elfu 50 nitaenda kariakoo kununua tishirt za shilingi elfu 4 classic kwa bei ya jumla tishirt 13 zitagharimu shilingi Elfu 48

( siongei theoretical hii biashara nina experience nayo kuna mda nilikuwa naagizwa na mtu kumchukulia mzigo tishirt ni classic kweli.)

baada ya hapo nitakuja kuziuza kwa bei ya TSH 800 kwa kila tishirt ambapo kwa tishirt 13 nitapata elfu 96000
Note: hizo tishirt nitaziuza kwa mda wa one week only.


Baaada yahapo nitarudisha nilichikuwa nimekopeshwa na kusimama mwenyewe .



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom