Me kwa upande wangu naona akili ni Kama battery ya ubongo. Yani Kila kiumbe kina ubongo. Ila uwezo wa kutumia ule ubongo ndio tunaita akili, hii inatokana/inaathiriwa zaidi na mazingira tunayoishi na tunayokutananayo.
Kwa mfano ngombe Ana ubongo, nyani, Simba, chui, mbuzi na viumbe vyote vina ubongo ..lakini namna wanavyotumia bongo zao kufikiri ndio tunaita akili lakini itaathiriwa na mazingira yao Kama wao. Na kwa binadamu pia ..hakuna asiye na ubongo Ila kwa Nini Kuna watu wanaweza kufanya mambo makubwa ilihali wote tuna ubongo? Hapo ndio uwezo wa akili unapoibuka, Yani akili ni Kama vile computer zilivyo na version mbali mbali window xp,7,8,8.1pro, 10 na Sasa 11 ndivyo akili ilivyo ..Yani uwezo unatofautiana. Jinsi unavyoweza kutumia ubongo wako ndio tunaita akili.
NB: Viumbe vyote vina ubongo lakini siyo Kila kiumbe chenye ubongo kina akili.