Utofauti kati ya kumbukumbu zinazohifadhiwa kwenye ubongo(Brain) na kumbukumbu zinazohifadhiwa na akili (Mind)

Utofauti kati ya kumbukumbu zinazohifadhiwa kwenye ubongo(Brain) na kumbukumbu zinazohifadhiwa na akili (Mind)

Mind is not a storage facility for it is not a physical organ but rather, a logical processing tool.
Daah... It is. Na shemu inayohusika ni hiyo niliyotaja.
Mkuu labda unipe elimu kuhusu Conscious mind, unconscious mi na subconscious mind... Please tupe elimu tujifunze
Hakuna storage yoyote inayoweza kufanyika kwenye mind. Hicho kitu hakipo leo na hata milele.
Hapa umetumia hisia na nadharia tu na sio tafiti
Kiwa mfano, mtu anaweza akawa na Ubongo usio na akili, kwa mfano mtu kichaa, lakini mtu hawezi kuwa na akili bila ya kuwa na ubongo. Leo umeniangusha sana kwenye post yako hii
Hapana. Naomba kwqnza unieleze kitu kimoja kimoja nilichouliza hapo juu
 
Kwa hivyo "storage facility" ni lazima iwe (physical) organ? Kwa nini? Btw, kwa nini kuhitajike physical organ kuhifadhi non-physical things (data, info., kumbukumbu)?

NB: Mimi sio mtaalamu wa hizi mambo kabisa. Nataka kujifunza tu na nipo tayari kufunzwa. Asanteni.
You can not create something from nothing
Storage facility sio lazima iwe physical. Mfano kwenye Web browser yako kuna Cookies ambazo ni details za matumizi yako ya internet je kwenye hiyo browser yako kuna physical storage????
 
Ubongo kimuonekano ni kama kitu cha duara cheupe kilichogawanyika mara mbili, pande la kushoto na pande la kulia, kama ilivyonyumba imeundwa na matofali, ubongo nao hivo hivo umeundwa na neurons (vitu kama kamba kamba vilivyounganyika pamoja kuunda circuit)
View attachment 1965742

Picha ya ubongo
View attachment 1965748
Picha ya neurons zilizojipanga kuunda circuit,

Kumbu kumbu zinakaa kwenye ubongo, ikitokea mtu kapata ajali ya boda boda kaumia ubongo wa mbele umeharibika, huyu mtu hataweza tena kukumbuka chochote au kufanya maamuzi ambayo ni logical,

Huoni kuwa huu ni ushahidi kwamba kumbu kumbu zinakaa kwenye ubongo?
Ni kweli kabisa.
Kwanini useme kumbu kumbu zinahifadhiwa kwenye mind? Au pengine hukuelewa mind ni nini?
Nadhani kuna kitu unamiss mkuu.. au hukusoma mada nzima Kiongozi.
Nimeeleza kabisa kwamba ubongo ndio hutunza kumbukumbu lakini pia akili hutunza kumbukumbu. Na akili inaweza kuAccess kumbukumbu zilizopo kwenye ubongo ila ubongo hauwezi ku access kumbukumbu za zilizopo kwenye akili
Kiufupi akili haihusiani na roho wala mizimu,
Akili ipo kwenye roho.. sio masula ya mizimu
akili ni kitendo cha ubongo kuchakata taarifa na kuendesha mambo ya kibaolojia na yasiyo ya kibaiolojia ili kumsaidia mtu kwenye maisha yake ya kila siku.
Sijui umenielewa mkuu?

All in all unaposema kumbu kumbu zinakaa kwenye akili it is illogical
Mmhhh.. kuna kitu unakosa mkuu. Nadhani ni Utofauti kati ya Mind,braina,soul, spirit nk..
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Okay, nakuelewa unachokisema hapa. Ingawa nashindwa kuona inavyojibu swali nililouliza.

Mtoa hoja kwenye makala yake (kama nimemuelewa vema) anasema brain na subconscious mind zote zinatunza kumbukumbu. Ameenda mbele zaidi na kuelezea aina ya kumbukumbu zinazotunzwa huko kote.

Sasa nilihisi kama kwa namna fulani unatofautiana na mleta hoja. Kwa hivyo nilitaka kujua ni nini hasa au sehemu gani mnatofautiana ili tujifunze zaidi au hata kupuka kupotoshwa.

Ametoa description yake ya mind (soul), je unakubaliana nae?
Hiyo description ya mind - soul ni ya mwaka 1600's enzi hizo sayansi ya mionzi haijagunduliwa namaanisha CT SCAN, MRI na vipo vingine kama BRAIN ELECTRO ENCEPHALOGRAM,

Zamani wanasayansi waliamini mind ni spirit, yaani mtu anaipata kiroho, plato yeye aliamini mind ni gods, yaani ni sawa na hizi nadharia za mleta thread,

Baadae daktari mmoja aliyemfanyia upasuaji wa ubongo mgonjwa, aliondoa uvimbe kwenye sehemu ya ubongo wa mbele, baadae mgonjwa alivopona akawa na tatizo la kupoteza kumbu kumbu, sasa hapo ndio wakaanza ku reason if mind is a spirit why huyu mgonjwa kapoteza kumbu kumbu baada ya kuondoa sehemu ya ubongo? Jibu likawa mind inakaa kwenye ubongo mind sio spirit,

Baadae ndio wakaanza kufanya study mbali mbali za watu walioumia maeneo mbali mbali ya ubongo ndio waka conclude kuwa mind ipo kwenye ubongo sio roho

Sijui umenielewa hapo?
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Sub counscious mind is controlled by the celebellum and the stem of brain, subconscious mind means set of brain activities that control your body semi counsciously (yaani yale mambo ambayo yapo kati kati ya hiari na yasiyo ya hiari) mfano kuua bila kukusudia chukulia umetoka pilini kukata kuni, umefika nyumbani kwako na panga mkononi ghafla ukamkuta mkeo kabananishwa kwenye kona analiwa uroda na njemba nyingine do you know what will happen?
Mate huko unaelekea kwenye Thalamus na limbic system
 
Okay, nakuelewa unachokisema hapa. Ingawa nashindwa kuona inavyojibu swali nililouliza.

Mtoa hoja kwenye makala yake (kama nimemuelewa vema) anasema brain na subconscious mind zote zinatunza kumbukumbu. Ameenda mbele zaidi na kuelezea aina ya kumbukumbu zinazotunzwa huko kote.

Sasa nilihisi kama kwa namna fulani unatofautiana na mleta hoja. Kwa hivyo nilitaka kujua ni nini hasa au sehemu gani mnatofautiana ili tujifunze zaidi au hata kupuka kupotoshwa.

Ametoa description yake ya mind (soul), je unakubaliana nae?
Popote pale duniani Wanasaikolojia watakueleza kwamba subconscious mind kazi yake ni kurekodi na kutunza kumbukumbu ya kila kitu kinachomtokea mwanandamu.. anaekataa hili ni ubishi wake tu
 
Mchango wako mkuu mbona unaguna?
1633537761839.png
 
Okay, nakuelewa unachokisema hapa. Ingawa nashindwa kuona inavyojibu swali nililouliza.

Mtoa hoja kwenye makala yake (kama nimemuelewa vema) anasema brain na subconscious mind zote zinatunza kumbukumbu. Ameenda mbele zaidi na kuelezea aina ya kumbukumbu zinazotunzwa huko kote.

Sasa nilihisi kama kwa namna fulani unatofautiana na mleta hoja. Kwa hivyo nilitaka kujua ni nini hasa au sehemu gani mnatofautiana ili tujifunze zaidi au hata kupuka kupotoshwa.

Ametoa description yake ya mind (soul), je unakubaliana nae?
Thalamus ni kisehemu ndani ya ubongo wa mwanandamu ambacho kila upande kimezungukwa na kitu kiitwacho Paleomammalian Cortex kwa lugha rahisi hufahamika kama Limbic System, Limbic System ni mfumo ambao kazi yake ni kuratibu mfumo wa Tezi na mfumo wa Autonomic Nervous System, Autonomic Nervous System (ANS) ni mfumo ambao huratibu mambo mbalimbali ila moja ya jambo ambalo huratibiwa na mfumo huu ni Emotions yaani vile mtu anavyojisikia.

Emotions ni kama vile hasira,upendo,ujivuni, wasiwasi, uogo, huruma, kuchanganyikiwa nk . ANS ndio inaratibu hisia moja ya hisia hizo ni
 
Great post.
Uzuri wa post zako mtu anatakiwa atulie ndio aelewe na akiisha elewa anajifunza kitu kikubwa sana. Hats off.

Hii mada umeileta wakati sahihi kwangu, thank you for this.
Sasa kuna uwezekano wa ku reprogram subconscious mind? Maana inaonekana negative thought zina nguvu sana, kuliko positive.
 
Great post.
Uzuri wa post zako mtu anatakiwa atulie ndio aelewe na akiisha elewa anajifunza kitu kikubwa sana. Hats off.
🌹🌹🌹😘😘
Hii mada umeileta wakati sahihi kwangu, thank you for this.
Sasa kuna uwezekano wa ku reprogram subconscious mind? Maana inaonekana negative thought zina nguvu sana, kuliko positive.
Naam mkuu unaweza kuziprogram. Hapo sasa ndio unaweza ku-Utilize subconscious and Nature kukupatia kila kitu unachohitaji.
Wengi hudharau hii njia maybe wanaona inachukua muda mrefu ila inafanya kazi vizuri sana
 
MATE;
Previous I wrote a topic centered on Illusion projection and I discussed a bit about how the brain process and encode memory, So this Topic will be serving as a stand-alone sequel of that Topic. Will be focusing on memory stored in brain and Soul respectively.

Kuna hivi vitu viwili tunaweza kua tunavichanganya pindi tunapokua tunataka kuvitumia, vitu hivyo ni kumbukumbu zinazohifadhiwa kwenye Ubongo(Brain) na kumbukumbu zinazohifadhiwa kwenye Akili (Mind). Sababu ni kwamba tunachanganya tofauti ya ubongo na akili. Ubongo ni mfumo endeshi (operating System upande wa Hardware yaani physical body) wa mwili wa binaadamu ambao umegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni Ubongo wa mbele, wa kati na wa mwisho….. Roho (Soul) imegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni Mind, Intellect na Impression, tunaweza kusema soul ni mfumo endeshi wa mwanadamu ambao unashughulikia mambo ya kiroho na mazingira/Nature (operating system inayoongoza upande wa Software katika mwili wa mwanadamu). Mind ndio inahusika kwenye kufikiria, hasa kwenye kutambua lipi baya na lipi jema.

Memory ni kisehemu katika ubongo ambapo taarifa (data au information) zinachambuliwa, zinahifadhiwa na kutolewa pindi zinapohitajika. Lakini pia Memory/kumbukumbu ni uwezo wa kukumbuka mambo ya zamani kama vile tabia/habits, uzoefu/experience, maarifa/skills, hisia, facts nk. Ubongo na Akili vyote vinatumika katika kuhifadhi kumbukumbu lakini zimetofautiani katika utendaji kazi, hivyo hapa tutaangali jinsi ubongo unavyokusanya taarifa na kuzihifadhi pia na akili jinsi ikusanyavyo.

Taarifa zinazotunzwa na Ubongo(Brain)

Katika ubongo wa mwanadamu sehemu inayohusika kuhifadhi kumbukumbu inaitwa Hippocampus ambapo kama sijasahau inapatikana katika ubongo wa kati, Ubongo wa mwanadamu hukusanya taarifa(data) mbalimbali kwa kupitia milango mitano ya fahamu ambayo ni Pua (Taarifa za harufu), Ulimi (radha), Macho(taarifa za picha), Masikio (taarifa za sauti), na Ngozi (taarifa kuhisi/sense). Kumbukumbu za mwanadamu zimegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Kumbukumbu ya muda mfupi (short-term memory) hii utunzwa kwa muda mfupi sana kichwani yaweza kua sekunde,saa au siku na hutokea labda pindi umepishana na mtu barabarana kadri unavyotembea utasahau kama ulikutana na mtu huyo au ukiwa unasoma namba labda za simu baada ya muda utazisahau na Kumbukumbu ya muda mrefu (Long-term memory) hii hutokea pindi kitu ulikiona mara kwa mara au mlitumia muda mrefu kua pamoja hata kwa nusu saa.

Chukulia kwamba ubongo ni CPU ya computer na Flash/Hard Disk yako ni mlango wa fahamu, CPU haina chochote ndani tofauti na sehemu ya kuhifadhi computer ambayo inaitwa Cache Memory hivyo basi unapoweka flash kwenye computer na kufungua vile vitu vilivyomo ndani ya Flash CPU itaviona ba kuvifungua kwenye kioo chako cha computer, lakini pia vile vitu ulivyofungua hua vinatunzwa ndani ya CPU katika eneo hilo liitwalo Cache Memory ili pindi utakapotaka kufungua kitu ulichokifungua muda uliopita computer isichukue muda mrefu lakini jinsi unavyokaa muda mrefu bila kufungua kile kitu ndio Cache memory inakipoteza taratibu.

Sasa kama ilivyo CPU ubongo pia hua haukasanyi data bali huletewa data kwa kutumia milango hiyo ya fahamu niliyoitaja na kuzifanyia (executing data), mfano kama macho yalimuona mtu Fulani sehemu falani mkaongea na kuondoka ubongo wako kupitia macho utachuku data kuhusu mtu huyo kama vile urefu wake, unene,rangi yake,jinsi alivyovaa nk nk piakupitia masikio ubongo utachukua sauti yake, mambo mliyoongea, kama kapaka mafuta Fulani basi ubongo kupitia mapua yako utachukua data hizo kuhusu harufu na kuzihifadhi kwenye Hippocampus.

Blending in….

Kwa siku moja ubongo huhifadhi mabilioni ya taarifa kichwani so kama ulimuona mtu sehemu mkaongea kidogo mkaachana kadri ya muda unavyoenda Folder lililotunza taarifa zake kichwani linazidi kua mbaaaali zaidi kabisa Sasa ikitokea siku umemuona tena Yule mtu labda baada ya miaka kumi ubongo kupitia macho,masikio na mapua utachukua taarifa ya picha ya mwili mzima, sauti yake nk kisha inafananisha/Matching/inaScan vitu hivyo kule kwenye Hippocampus ili kuona kama kuna taarifa zinazomuhusu mtu huyo baada ya kuScan itakuletea machaguo/suggestion kadha zilizofanana na taarifa za mtu huyo sasa hapo utaanza kuchukua zile taarifa za machaguo uliyoyaaona ndani ya kichwa na tarifa za huyo mtu aliyopo mbele yako ndio utaanza kusema sasa hivi wewe sio Fulani, wewe au ni Fulani hapo ubongo unakua unapekua mafaili chapchap ili kupata matokeo mazuri sasa kama Yule mtu anakukumbuka akikuambia “hunikumbuki ni mimi Fulani tulikutana sehemu Fulani mwaka Fulani” ubongo utayachukua hayo maneno na kuyaScan na kupata folder zima la mtu huyo nawe ndio utajikuta unasema aaahaaa ni wewe ilikua hivi na hivi..
Hivyo basi kumbukumbu zote zinazohifadhiwa na ubongo ni kwa ajli ya kumuwezesha mwanadamu kuyakabili mazingira yake na vyote vinavyomzunguka .



Kumbukumbu zinazohifadhiwa kwenye Akili (Mind)

Roho
(Soul) imegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni Mind/Akili, Intellect na Impression.Mind ndio inahusika kwenye kufikiria, hasakwenye kutambua lipi baya na lipi zuri ,Mind imegawanyika katika pande tatu ambazo ni Conscious mind, Unconscious mind na Subconscious Mind …..Subconcious Mind hii ndio sehemu kuu ya Roho (Soul) ambayo kazi yake ni kurekodi shughuli zetu zakila siku ziwe za kimwili au kiroho. Huku juu tumeona jinsi Ubongo unavyokusanya taarifa kupitia milango ya fahamu na kuzihifadhi kwa ajili ya matumizi ya baadae…Akili pia (subconscious mind) hukusanya na kutunza kila taarifa sema kumbukumbu zinazotunzwa na akili huhifadhiwa kwa ajili ya matumizi ya kiroho.



BIOS (Basic Input/Output system) hiki ni kifaa kidogo ambacho hua kimepachikwa kwenye motherboard ya Computer, kinabeba na kuhifadhi taarifa za Computer husika kama vile jina la computer nk lakini pia kazi yake ni inaongoza mzunguko wa data kati ya Operating system na baadhi ya vifaa vingine vilivyounganishwa kama vile Video Adapter,Hard disk , Keyboard,mouse nk Bila hii chip huwezi kuwasha computer. Sasa basi Soul ni kama Bios chip ya mwanadamu, mwanadamu bila roho si mwanadamu maana Subconscious Mind ndio imebeba taarifa zake zote kama vile wapi alipotoka, wapi alipo, wapi anaenda, vitu upendavyo, hisia, tabia, vitu unavyofahamu kila anachotenda mwanadamu iwe kwa kuwaza,kuongea,kuona,kunusa,kuhifadhi Subconscious Mind hurekodi na kuhifadhi nk nk. Subconscious Mind pia inauwezo wa kuingia kwenye ubongo na kuchukua taarifa/kumbukumbu zote zilizopo humo na kuzihifadhi ila ubongo hauwezi kuingia kwenye Subconscious Mind na kuchukua taarifa.



Kila kilichorekodiwa na kuhifadhiwa kwenye Subconscious Mind huja kutimika katika maisha ya mwanadamu, kila unachokiwaza,kuongea au kutenda sana basi Subconscious Mind huwasiliana na Nature kisha itakua inakulete yale inayoyaona kwako mara nyingi. Kwa mfano ukiwa unawaza kwa muda mrefu kwamba kitu Fulani kitakutokea basi Subconscious Mind inawasiliana na nature kwamba mtu huyu anahitaji na kupenda kitu Fulani basi nature itakuletea kitu hicho ndio maana unashauriwa kujiwazia mambo mazuri tu, na kama hupendi vitu Fulani vikutokee basi usijaribu kukitenda kitu hicho maana nature itakua inakuletea kitu hicho mara kwa mara kwakua Subconscious Mind inakua imesharekodi kwamba unapenda kitu hicho. Ukifa Mungu hana haja na Mwili wako anachukua tu Roho yako maana humo ndio kuna kila taarifa.

Akili na ubongo vyote vinahifadhi kumbukumbu ila akili ikihifadhi kitu basi hakipotei daima lakini ubongo hua unafuta baadhi ya kumbukumbu kama nilivyoeleza, akili inaweza kuchukua taarifa za ubongo ila ubongo hauwezi, akili inaunganisha ubongo,mwili, mazingira/nature na mambo ya kiroho. Kama ubongo ni hardware basi akili ni Operating System.

Alamsiki…..

Da’Vinci

-Excelsior
Akili inahifadhi vipi Kumbukumbu ?

Akili ni nini hasa ?
 
Hadi utakapoeleza akili ni nini na inapatikana sehemu gani ya mwili ndio nitaweza kujadili hoja zako.

Otherwise iwe utofauti kati ya kumbukumbu zinazohifadhiwa kwenye roho na ubongo na hiyo roho inapatikana wapi ndani ya mwili!
Mtoa mada laiti angejua akili ni nini ? Nina hakika asingeandika hiki alicho kiandika.

Swali lako ulilo uliza ni miongoni mwa maswali kongwe yaani maswali ya tangu na tangu. Watu wazamani walikuwa wanauliza maswali makuu matatu :

1. Akili katika mwili wa mwanadamu iko wapi ? Waliuliza swali hili baada ya kujua Ubongo ni nini na Moyo ni nini ? Baada ya hapo wakaja na swali hili :

2. Je akili ipo kwenye Ubongo au Moyo ?

3. Je mtu anapataje maarifa na yanakaa wapi maarifa ?

Nakumbuka nilishawahi kumpa nasaha mtoa mada awe anaangalia wapi anatoa maarifa yake au wapi anachukua mawazo yake.

Ni vigumu sana kuijadili Akili wakati hujui Akili ni nini...?
 
Mtoa mada laiti angejua akili ni nini ? Nina hakika asingeandika hiki alicho kiandika.

Swali lako ulilo uliza ni miongoni mwa maswali kongwe yaani maswali ua tangu na tangu. Watu wazamani walikuwa wanauliza maswali makuu matatu :

1. Akili katika mwili mwanadamu iko wapi ? Waliuliza swali hili baada ya kujua Ubongo ni nini na Moyo ni nini ? Baada ya hapo wakaja na swali hili :

2. Je akili ipo kwenye Ubongo au Moyo ?

3. Je mtu anapataje maarifa na yanakaa wapi maarifa ?

Nakumbuka nilishawahi kumpa nasaha mtoa mada awe anaangalia wapi anatoa maarifa yake au wapi anachukua mawazo yake.

Ni vigumu sana kuijadili Akili wakati hujui Akili ni nini...?
Ni kijana wa Quantum Physics anayejihisi ana maarifa sana.
Simdharau ila hajafahamu kwamba huwa hatuendi hivyo
 
Nitajie kumbu kymbu zinazokaa kwenye mind according to your theory nikupe proof kuwa akili inapatikana kwenye ubongo

Nitajie mkuu
Mimi nasema akili inapatikana katika moyo (Yaani mahali ilipo akili ni kwenye MOYO) ila moyo na ubongo vinashirikiana katika upangaji mambo katika sehemu zake na kumbukumbu pia.
 
Ni kijana wa Quantum Physics anayejihisi ana maarifa sana.
Simdharau ila hajafahamu kwamba huwa hatuendi hivyo
Watu wa Quantum Physics sijui kwanini hawajihusishi na uhalisia na kuhoji mambo kama yalivyo.

Kijadili mambo haya yanataka umakini mkubwa sana.
 
🌹🌹🌹😘😘

Naam mkuu unaweza kuziprogram. Hapo sasa ndio unaweza ku-Utilize subconscious and Nature kukupatia kila kitu unachohitaji.
Wengi hudharau hii njia maybe wanaona inachukua muda mrefu ila inafanya kazi vizuri sana
I wish siku ulete post namna ya ku reprogram Da'vinci.
 
Mnanisimitisha kuona kwamba mmeacha kujadili mada mnamjadili mtoa mada. This isn't a Personal post, ni post ya kuelimishana na pale mtu anapokua ana mawazo mbadala dhidi ya yale ya mtoa mada basi ruhusa kuyachangia ili sote tujifunze... I'm not that Smart panty guy.
Napenda tu kushea mawazo yangu juu ya vile navyoelewa na kufikiria vitu.
Ni kijana wa Quantum Physics anayejihisi ana maarifa sana.
Simdharau ila hajafahamu kwamba huwa hatuendi hivyo

Watu wa Quantum Physics sijui kwanini hawajihusishi na uhalisia na kuhoji mambo kama yalivyo.

Kijadili mambo haya yanataka umakini mkubwa sana.
 
Back
Top Bottom