Sasa si umsaidie kuliko kuja kumnanga. Nida Id ni moja wapo ya viambatanisho kudai mafao yakoWastaafu huwa mnasumbuliwa sana sijui ni uzee au wengi wenu uelewa wa mambo ni mdogo
Mf miePole mzee! Majina mangapi yametofautiana?
Kumbe wenye matatizo ya majina kutofautiana inabidi kufanya mchakato haraka sana wa kuhalalisha majina hayo
Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Kama hujui uliza na utulize kijambio, majina ya NIDA , certificate of service,NSSF na barua lazima yawe sawaMajina ya NIDA yanahusiana vipi na mafao,nadhani mafao wanaangalia barua yako ya ajira na hiyo barua ya mwisho plus check Number.
Itasumbua sana hata herufi Moja tu inatosha kukuzungusha mjini kubadiliMf mie
NSSF,kazini, NIDA, DL,Bank kuna majina ma3
Vyeti vya shule kuna ma2
Haitonisumbua lolote huko mbele?
Mbona kamzozoItasumbua sana hata herufi Moja tu inatosha kukuzungusha mjini kubadili
USSR
Sent from my TECNO B1c using JamiiForums mobile app
Nenda stationary wata scan hizo barua na certificate watabadili majina tu yaendane na NIDA na NSSF mkuu ukikwama ni pm nikusadieHabari wapendwa.
Nina shida katika ya majina kitambulisho cha (NIDA) na (NSSF) majina sawa ila katika barua yangu ya ukomo wa (ajira) na (certificate) majina tofauti na ya hivyo vitambulisho cha NIDA na NSSF
Nimeongea na mwajiri wangu anisaidie kubalisha kwenye barua na certificate anasema haiwezekani
NIDA, mahakaman, aridhi, gazeti nimeshaenda lakini bado nahangaika
Nifanyeje ili niweze kupata mafao yangu?
Hili ni janga la nchi. Tanzania watu wanarahisisha sana mambo ka sababu ya uzembe. Watu hawako makini kuandika majina na wanajiandikia wanavyotaka. Hata tofauti ya herufi moja ni kosa kubwa na kisheria ni jina tofauti. Ni vizuri wakasumbuliwa na kukwama kabisa kwani wengi ni wabishi. Watu wanafanya uzembe hata kuandika maneno marahisi kabisa lakini ukimpa alert anakutukuna. Na hapa sizungumzii kukosea kwa bahati mbaya ambako mtu yoyote anaweza kufanya hivyo. Naongelea uzembe wa kutojali.Mf mie
NSSF,kazini, NIDA, DL,Bank kuna majina ma3
Vyeti vya shule kuna ma2
Haitonisumbua lolote huko mbele?
Upo sahihi ndugu ila nilienda mahakamani nikapewa kiapo nikaenda aridhi kwa msajili wamajina akanipa deedpool na mihuri nyuma yatanganyika lakini nilivyopeleka nssf wakaniambia eti nikabadilishe ile card yao jina yafanane nikaenda sehemu yakubadilishia nikatoa 5000 lakini zoezi likashindikana hadi nida na nida yeneyewe ndio muzunguko huu mwezi 3 sasa nahangaika tu ndio maana nikaja humu kwa msaada zaidi.Kula kiapo mahakamani kuyakubali kuwa yote hayo ni majina yako.
Lakini hakikisha majina yalioko benki yapo sawa na kiapo kimojawapo.
Kwa faida ya wengine, ili upate mafao yako vifuatavyo lazima vipelekwe kwenye mfuko wa mafao;-
1. Barua ya ajira
2. Barua ya kuthibitishwa kazini
3. Bank statement
4. Salary slip
5. Kitambulisho cha NIDA/Leseni ya udereva/mpiga kura
6. Barua ya cheo cha mwisho
7. Picha za PPS nadhani sita hivi
Ukiishazeeka umestaafu, nani anajali kwa humu Tanzania. Hao wanaokusumbua wanasahau kuna siku na wao watastaafu.Wastaafu huwa mnasumbuliwa sana sijui ni uzee au wengi wenu uelewa wa mambo ni mdogo