Utofauti wa majina yangu kwenye vitambulisho umepelekea nishindwe kupata mafao yangu, nifanyeje?

Utofauti wa majina yangu kwenye vitambulisho umepelekea nishindwe kupata mafao yangu, nifanyeje?

Majina ya NIDA yanahusiana vipi na mafao,nadhani mafao wanaangalia barua yako ya ajira na hiyo barua ya mwisho plus check Number.
Ukienda kwa mfano NSSF lazima wa update taarifa hasa Jina liendane na nida na watalazimisha majina yaliyomo nida ndiyo yatumike na kama nida wamekosea Jina hapo ndio shida itakapoanzia. Mi nimepatwa na Hilo lakini namshukuru Mungu nimemalizana nao
 
Wala usisumbuke erickelly tafuta Mwanasheria, atakuandalia AFFIDAVIT kuthibitisha, jina lililopo NIDA ndiyo wewe mwenye jina kwa card ya NSSF.
Ni ngumu kama unavyo fikiria. Hayo yote nishafanya lakini inagonga mwamba
 
Andaa Affidavit of proof of names uwapelekee halafu usikilizie watasemaje? Kwani yametofautiana sana kwa mfano labda cheti kimoja kina jina la Abdullah Juma wakati NIDA ina Juma Ramadhan?
Tofauti ipo hivi (barik daudi godi) jina lingine ni (joseph daudi godi) hilo la juu ni jina langu lakuzaliwa kabisa ila kutokana na hilo jina linafanania na lakike ndio nikaona nibadilishe ndio nikajiita hilo jina la pili.Ila hayo majina hapo sio ni mfano tu.
 
issue ipo hivi (Bariki daudi godi)Hili ni jina langu la kuzaliwa (Joseph daudi godi)Hili ndio nimependa kujipa mwenyewe.Kwa sababu hili jina langu lakuzaliwa yanaendana na la kike sana lipo kikeni sasa mimi nimeona sio jambo jema ndio nikaanza kubadilisha kila document ninayosomea naandika jina jipya kasoro kitambulisho cha nida tu bhasi.Huo ni mfano.Tu jinsi ilivyo
 
From Bariki to Joseph mbona mbali sana? Hapo inakua watu wawili tofauti mkuu Ni kweli lazima wakusumbue,ingekua labda badala ya Bariki imeandikwa Barki ungeapa tu mahakamani
 
Yah ipo hivyo lakini mbona walikuwa wananipelekea michango yangu na jina sio hilo mbona hawakushtuka hilo iwe sasa wakati wa kutoa eti?
 
Habari wapendwa,

Nina shida katika ya majina kitambulisho cha (NIDA) na (NSSF) majina sawa ila katika barua yangu ya ukomo wa (ajira) na (certificate) majina tofauti na ya hivyo vitambulisho cha NIDA na NSSF.

Nimeongea na mwajiri wangu anisaidie kubalisha kwenye barua na certificate anasema haiwezekani.

NIDA, mahakaman, aridhi, gazeti nimeshaenda lakini bado nahangaika.

Nifanyeje ili niweze kupata mafao yangu?
Hebu mkuu jaribu kufuatilia hii taarifa uone itakusaidiaje kwenye kubadilisha majina yako kwenye NIDA. Kuna namba za simu hapo.
 
Attachments

  • IMG-20230608-WA0000.jpg
    IMG-20230608-WA0000.jpg
    59.7 KB · Views: 27
Anza mchakato wa kukubali hayo majina mengine kama yako:-
  • Nenda ofisi ya ardhi wakupatie abc​
  • Nenda ofisi ya wakili (advocate) kuna nyaraka watakuandalia ya kuhusu hayo majina yako mengine; watapeleka kwa ajili ya kuapa​
  • Rudisha hiyo nyaraka ardhi ikiwa na picha zako, watagonga mihuri na utalipia kiasi kidogo​
  • Utapewa nyaraka za kutambua hayo majina​
  • Ambatanisha kwenye madai yako ya mafao​
  • Baada ya hapo, huyo anayekuambia hustaili kulipwa, mtaje jina hapa jukwaani; kwa sababu kuna wengine wapo kazini hawajui kazi walizosomea.​
Nje ya mada,kwanini ardhi inatumika kwenye ussue ambayo haihusiani na mambo ya ardhi?
 
Yaan inakuaje mtu unakua na majina tofauti!?? Aisee Yan umeanza la kwanza ad form four hujui majina yako? Watu wazembee sana by the way pole sana na Acha uzembe
 
Vipi Majina ya vyeti vya academic yakiwa matatu ila la katikati Lina initial peke yake(herufi ya kwanza tu) na sehemu nyingine kuna Majina matatu kwa urefu?
 
Nje ya mada,kwanini ardhi inatumika kwenye ussue ambayo haihusiani na mambo ya ardhi?
Niliwauliza hilo swali na jibu walilonipa, lengo la kubadili jina lina madhara kwenye umiliki wa mali, na mali inaanzia kwenye ardhi; kama ni majengo n.k
 
Ukienda kwa mfano NSSF lazima wa update taarifa hasa Jina liendane na nida na watalazimisha majina yaliyomo nida ndiyo yatumike na kama nida wamekosea Jina hapo ndio shida itakapoanzia. Mi nimepatwa na Hilo lakini namshukuru Mungu nimemalizana nao
Ulimaliza vipi mkuu, wengi tuna shida hiyo.
 
Back
Top Bottom