Utofauti wa majina yangu kwenye vitambulisho umepelekea nishindwe kupata mafao yangu, nifanyeje?

Utofauti wa majina yangu kwenye vitambulisho umepelekea nishindwe kupata mafao yangu, nifanyeje?

Mf mie
NSSF,kazini, NIDA, DL,Bank kuna majina ma3

Vyeti vya shule kuna ma2

Haitonisumbua lolote huko mbele?
Sidhani kama itasumbua kwa sababu ukistaafu haupeleki vyeti vya taaluma, nahisi utapeleka barua ya ajira + salary + na hiyo Nida. Sasa hivyo vyote vikifanana majina hakuna shida, ila sina uzoefu

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Habari wapendwa,

Nina shida katika ya majina kitambulisho cha (NIDA) na (NSSF) majina sawa ila katika barua yangu ya ukomo wa (ajira) na (certificate) majina tofauti na ya hivyo vitambulisho cha NIDA na NSSF.

Nimeongea na mwajiri wangu anisaidie kubalisha kwenye barua na certificate anasema haiwezekani.

NIDA, mahakaman, aridhi, gazeti nimeshaenda lakini bado nahangaika.

Nifanyeje ili niweze kupata mafao yangu?
Nenda kaape kwa mwanasheria ni jambo dogo sana hilo
 
Nenda stationary wata scan hizo barua na certificate watabadili majina tu yaendane na NIDA na NSSF mkuu ukikwama ni pm nikusadie

USSR

Sent from my TECNO B1c using JamiiForums mobile app
USSR! Sasa aku PM kwa lipi wewe mwongoze huku ili na wengine wapate faida, ila huko unakutaka naona umeingia kwenye ukishoka tamaa mbaya mno dadangu USSR!
 
Haiwezi kukuk
Mf mie
NSSF,kazini, NIDA, DL,Bank kuna majina ma3

Vyeti vya shule kuna ma2

Haitonisumbua lolote huko mbele?
kukusumbua sababu ZAMANI majina ya shule yalikuwa sio lazima matatu ila Cheti Cha kuzaliwa na ivyo ulivyoorodhesha ndio majina matatu
 
Itasumbua sana hata herufi Moja tu inatosha kukuzungusha mjini kubadili

USSR

Sent from my TECNO B1c using JamiiForums mobile app

Itamsumbua vp wakati NSSF na Kazini majina ni hayohayo. Vyeti vya shule vitatumika wakati gani kwenye kufuatilia mapato? Hapo hakuna shida kwa huyu raia ambaye NSSF na Kazini majina ni hayohayo
 
Itasumbua sana hata herufi Moja tu inatosha kukuzungusha mjini kubadili

USSR

Sent from my TECNO B1c using JamiiForums mobile app
Utabadili nyaraka zipi ikiwa zamani vyeti vilikuwa vinatolewa kwa majina mawili, na kwenye ajira na NIDA ukalazimishwa kuongeza jina la tatu?

Au nahisi itabidi upate nyaraka ya kisheria kukiri kwamba hayo majina yote ni yako! Kubadili majina haiwezekani ikiwa NIDA inataka majina matatu na vyeti vilishatolewa siku nyingi vikiwa na majina mawili tena ambavyo havina picha, NECTA watakubali kweli?

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Kula kiapo mahakamani kuyakubali kuwa yote hayo ni majina yako.
Lakini hakikisha majina yalioko benki yapo sawa na kiapo kimojawapo.
Kwa faida ya wengine, ili upate mafao yako vifuatavyo lazima vipelekwe kwenye mfuko wa mafao;-
1. Barua ya ajira
2. Barua ya kuthibitishwa kazini
3. Bank statement
4. Salary slip
5. Kitambulisho cha NIDA/Leseni ya udereva/mpiga kura
6. Barua ya cheo cha mwisho
7. Picha za PPS nadhani sita hivi
Hapo sawa umeeleweka. Kuna member huko juu kadanganywa kwamba hadi majina ya vyeti vya taaluma lazima yaendane na barua ya ajira + NIDA.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Hili ni janga la nchi. Tanzania watu wanarahisisha sana mambo ka sababu ya uzembe. Watu hawako makini kuandika majina na wanajiandikia wanavyotaka. Hata tofauti ya herufi moja ni kosa kubwa na kisheria ni jina tofauti. Ni vizuri wakasumbuliwa na kukwama kabisa kwani wengi ni wabishi. Watu wanafanya uzembe hata kuandika maneno marahisi kabisa lakini ukimpa alert anakutukuna. Na hapa sizungumzii kukosea kwa bahati mbaya ambako mtu yoyote anaweza kufanya hivyo. Naongelea uzembe wa kutojali.
Pamoja na uzembe wa kuandija majina kwa sasa, lakini miaka ya 2000 kushuka chini, wengi wao vyeti vya taaluma vina majina mawili kuanzia darasa la saba, kidato cha nne, mpaka chuo. Kwenye ajira wakambiwa lazima waongeze jina la tatu ambalo limo ndani ya cheti cha kuzaliwa. Na NIDA hivyo hivyo.

Sasa huyu hana kosa, inabidi apate nyaraka ya kisheria kuthibitisha majina ya kwenye vyeti vya taaluma (mawili) na ajira na NIDA (matatu) ni yake.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Niliuliza NIDA kuhusu kubadili majina nikaambiwa jambo mojawapo ni kutangaza kwenye gazeti la serikali, vipi ulipitia huo mchakato au ni shortcut?
 
Habari wapendwa,

Nina shida katika ya majina kitambulisho cha (NIDA) na (NSSF) majina sawa ila katika barua yangu ya ukomo wa (ajira) na (certificate) majina tofauti na ya hivyo vitambulisho cha NIDA na NSSF.

Nimeongea na mwajiri wangu anisaidie kubalisha kwenye barua na certificate anasema haiwezekani.

NIDA, mahakaman, aridhi, gazeti nimeshaenda lakini bado nahangaika.

Nifanyeje ili niweze kupata mafao yangu?
Something is here to learn
 
Gazeti nimepata issue ni hapo n
Niliuliza NIDA kuhusu kubadili majina nikaambiwa jambo mojawapo ni kutangaza kwenye gazeti la serikali, vipi ulipitia huo mchakato au ni shortcut?
gazeti nimepata issue ni hapo nida wameniambia niandike tena barua kwenda kwa mkurugezi wa nida kuomba ridhaa ya kubadilisha hilo jina
 
Anza mchakato wa kukubali hayo majina mengine kama yako:-
  • Nenda ofisi ya ardhi wakupatie abc​
  • Nenda ofisi ya wakili (advocate) kuna nyaraka watakuandalia ya kuhusu hayo majina yako mengine; watapeleka kwa ajili ya kuapa​
  • Rudisha hiyo nyaraka ardhi ikiwa na picha zako, watagonga mihuri na utalipia kiasi kidogo​
  • Utapewa nyaraka za kutambua hayo majina​
  • Ambatanisha kwenye madai yako ya mafao​
  • Baada ya hapo, huyo anayekuambia hustaili kulipwa, mtaje jina hapa jukwaani; kwa sababu kuna wengine wapo kazini hawajui kazi walizosomea.​
 
Back
Top Bottom