Utofauti wa mishahara katika Utumishi wa umma, kunavunja moyo na kusababisha watu kubeza kusoma sana

Utofauti wa mishahara katika Utumishi wa umma, kunavunja moyo na kusababisha watu kubeza kusoma sana

Kwahiyo kila mtu akifanya kazi katika hizo taasisi, nani atafanya kazi katika hizi Halmshauri zetu?
Burundi wao wameanza utaratibu mpya kuwa ni amri hata wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye mashirika ya UN, yaliyopo burundi azima mishahara yao ilingane na watumishi wengine wa serikali!!!kwani kazi wanazofanya huko hata wenzao walioko serikalini wanaweza zifanya!!Africa kuna vituko sana!!
 
Uzi umepozwa na mleta mada!!! Post ya kwznza tu nilitegemea kukuta tarakimu za takwimu zinazodhibitisha ujumbe uliobebwa kwenye kichwa cha uzi huu!!

Kwa hiyo uzi upo "kipropaganda za kisiasa "badala ya uhalisia.
 
Sio lazima ufanye kazi serikalini
 
Lets say Serikali haina uwezo wa kupandisha mishahara ya Electrical engineers wote iwe 2mil.

Kwa hiyo Solution ni huyo Electrical Engineer wa 2mil ashuke ili naye alipwe laki 9 ili hao wafanyakazi wa serikali wawe sawa?

Hebu nijibu hili swali directly bila kupindisha pindisha maneno.
Hivi mshahara wa TBS Kwa mtu mwenye degree mfano food science analipwa salary shillings ngapi.
 
Ni ajabu leo angalao umekuja na constructive criticism!

Suala la harmonisation ya mishahara ya watumishi wa umma wakiwemo wanasiasa hususani wabunge, mawaziri, masipika etc vs wale wa mashirika ya umma hususani TRA, TPA, TANAPA, BOT etc, lilikuwapo siku nyingi enzi za Mwalimu. Kulikuwa na mamlaka iliyokuwa inaitwa SCOPO ambayo ndiyo ilikuwa na jukumu hilo.

Utaratibu huo ulikuja kutupiliwa mbali na wanasiasa baada ya Mwalimu kung'atuka. Kila taasisi ikaruhusiwa kupanga mishahara na marupurupu yake. Wabunge wakawa wanajipangia mishahara na marupurupu yao ili yalingane na wabunge wa nchi za nje na mashirika ya umma yakafanya hivyo hivyo hadi ma CEO wa mashirika haya wakafikia kuwa wanapata mishahara hadi ya shs 45 million kwa mwezi, achilia mbali posho na marupurupu ya kutisha.

JPM amejitahidi angalao kuiteremsha mishahara hii ya ma CEO wa mashirika ya umma hadi tsh 15 million kwa mwezi. Kwa wanasiasa kama wabunge si jambo rahisi lakini angalao yeye kajipunguzia mshahara hadi kuwa shs 9 million kwa mwezi. Ipo siku ndani ya hii 5 tena atarudisha SCOPO kama ilivyokuwa enzi za Mwalimu! Hayo ndiyo matumaini yetu.
 
Usivunjike moyo mkuu, unaweza kuhamia kwenye hizo taasisi na wewe ulipwe kama wao. Bahati nzuri recruitment zake zinapitia utumishi (ajira portal).
Life is not fair and it won't be fair. Tofauti zetu ndio zinafanya tuendelee kuishi sababu tunategemeana.
Hiyo harmonization hata ikifanyika bado haiwezi kuleta equality. Mfano: kuna professions ni rare kwenye nchi kama madaktari bingwa huwezi kusema mishahara iendane na daktari wa kawaida.
 
hivi ile tume iliyoundwa kulevel mishahara imeishia wapi?
 
Lets say Serikali haina uwezo wa kupandisha mishahara ya Electrical engineers wote iwe 2mil.

Kwa hiyo Solution ni huyo Electrical Engineer wa 2mil ashuke ili naye alipwe laki 9 ili hao wafanyakazi wa serikali wawe sawa?

Hebu nijibu hili swali directly bila kupindisha pindisha maneno.
Sio lazima mmoja amfuate mwenzie,unawezatafutwa wastani.
Kati ya laki 9 Na 2m. MF wanawezalipwa 1.4m.
 
Usivunjike moyo mkuu, unaweza kuhamia kwenye hizo taasisi na wewe ulipwe kama wao. Bahati nzuri recruitment zake zinapitia utumishi (ajira portal).
Life is not fair and it won't be fair. Tofauti zetu ndio zinafanya tuendelee kuishi sababu tunategemeana.
Hiyo harmonization hata ikifanyika bado haiwezi kuleta equality. Mfano: kuna professions ni rare kwenye nchi kama madaktari bingwa huwezi kusema mishahara iendane na daktari wa kawaida.
Hapo hoja ni Kuwa unakuta wote ni mabingwa lakini mishahara inatofautiana sana.
 
Hizo taasisi zinazozalisha fedha ni ujanja wao?Taasisi inazalisha fedha kwa vile imeundiwa utaratibu huo,sio ujanja wa wafanyakazi. Mfanyakazi akiwa TRA lazima fedha zizalishwe. Ukimpeleka halmashauri atazalisha chache.
 
Burundi wao wameanza utaratibu mpya kuwa ni amri hata wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye mashirika ya UN, yaliyopo burundi azima mishahara yao ilingane na watumishi wengine wa serikali!!!kwani kazi wanazofanya huko hata wenzao walioko serikalini wanaweza zifanya!!Africa kuna vituko sana!!
Hili jibu liko Na akili kubwa. Watu wanajidai taasisi ile inazalisha fedha kanakwamba ni ujanja was hao wafanyakazi kumbe ni majukumu ya kitaasisi. Ukimtoa mtu halmashauri ukimpeleka TRA atazalisha fedha kama atakaowakuta hapo TRA
 
Unataka kusema nini.
Mishahara inapangwa kutokana na mnachozalisha.hii iliwekwa kwa makusudi ili watu wajitume
 
mtoa mada anahoja nzuri ila watu humu wanatoa majibu sio mfano mm nina jamaa zangu nilisoma nao chuo fulani wanemalia degree ya elimu hesabu na wote gpa zao ni 4.2 mmoja aliajiriwa kufundisha shule ya secondary mshahsra TGTS D1 ni 716,000 apo hajakatwa makato mwingine aliajiriwa kama tutor udsm mshahara ni 1.6M

kumbuka wote elimu sawa kabisaaa

shida hapa serikali inatakiwa kuwavuta wale wenyemishahara midogo angalau wapande wafanane na wengne
 
Kutaka watumishi wote serikalini wafanane mishahara ni ujinga,
Mtu lazima alipwe kutokana na unyeti wa taasisi aliyopo,Dereva wa jaji mkuu,awezi kulipwa sawa na dereva wa Tanesco anayepereka mafundi site,
Dereva wa jaji lazima awe na mavazi stahiki,suti,huyu anatunza siri,ukipata hii nafasi lazima ulipwe vzr Ili uendsne na boss na ofisi unsyoihudumia,dereva wa Tanesco,dawasa,muruwasa,Hawa ni kuvaa overlol tu,
 
Ni ushetani tu, hakuna justification. Na huu ushetani uliasisiwa na Mkapa.
Wewe ni mpumbavu elimu yako ya phd kama haina tija nani akulipe pesa ya bure.

Umeambiwa bargaining power na uhitaji wa kazi yako ndio vinaamua hutaki kaombewe pepo mchafu akutoke au awatoke unaoona wanafanya ushetani vinginevyo kulia Lia hakutakusaidia
 
Tuna tatizo la kufukiria kama watanzania.
Mleta mada ameleta hoja inayotakiwa kujadiliwa lakini watu mnahamisha mada na kuanza kumshambulia.

Hii fact mbona iko wazi sana, Electrical engineer wa Halmashauri alipwe laki 9 na electrical engineer wa TBS alipwe 2m ilihali wote wamesoma taaluma moja na wameajiriwa na serikali na sisi kama watanzania bado hatuoni kuna tatizo hapo? Majibu yanatoka kwa jazba tu kama vipi nayeye aende huko TBS akapate mshahara mnono, kwahiyo halmashauri hawahitaji electrical engineer?

Ni kweli hayo majibu ni majibu sahihi kwa wasomi mlioko humu jamvini au kwakuwa mwafrika ni mbinafsi zaidi regardless anafanya nini na wapi?
Na wa Tanesco alipwe 3mln ndo inavyotakiwa uwe umesoma elimu moja nk suala ni mazingira ya kazi ni tofauti na mashirika hayo yanatakiwa kuzalisha na kiasi wanachozalisha na kikupwa kuliko services za salary zao but nyie wa Halmashauri kwanza hata kujiendesha hamuwezi lakini pia unyeti wa kazi.

Ukimlipa Tbs vihela vya huko Halmashauri atahongwa mpate bidhaa feki afu mufe tuu kama mizogo
 
Back
Top Bottom