Utofauti wa mishahara katika Utumishi wa umma, kunavunja moyo na kusababisha watu kubeza kusoma sana

Utofauti wa mishahara katika Utumishi wa umma, kunavunja moyo na kusababisha watu kubeza kusoma sana

Mtu anaona kabisa pale wanalipa vizuri kuliko hapa. Badala ya kuhamia wanakolipa vizuri anataka wamuongezee pesa nyingi akiwa pale pale na uzalishaji ule ule[emoji3][emoji3]

Aisee unatakiwa kuhama ndugu.

Kwamba dereva anayemuendesha raisi alipwe sawa na dereva anayemuendesha afisa wa halmashauri?[emoji3][emoji3]

Au dereva wa Tanapa alipwe sawa na dereva wa halmashauri [emoji2960]

Hebu kaa chini fikiria kidogo reasons behind, kwanini mshahara uko tofauti?
 
mtoa mada anahoja nzuri ila watu humu wanatoa majibu sio mfano mm nina jamaa zangu nilisoma nao chuo fulani wanemalia degree ya elimu hesabu na wote gpa zao ni 4.2 mmoja aliajiriwa kufundisha shule ya secondary mshahsra TGTS D1 ni 716,000 apo hajakatwa makato mwingine aliajiriwa kama tutor udsm mshahara ni 1.6M

kumbuka wote elimu sawa kabisaaa

shida hapa serikali inatakiwa kuwavuta wale wenyemishahara midogo angalau wapande wafanane na wengne
Kupanga ni kuchagua

Kumbuka huyo wa udsm alitulia kimya kazi za ualimu zilipotangazwa Ila huyo mwenzake akapapalikia kupata kazi haraka na kumuacha mwenzie anasubiri vyuo vitoe kazi.
Pia huyo wa chuo unakuta interview wamefanya watu 40 na anatakiwa mtu 1 tu na jamaa akatusua kwenye michakato yote ya usaili, wakati mwalimu wa sekondary aliapply to mtandaoni na kupangiwa kituo.

Kwa hiyo kwenye maisha yako unatakiwa kuwa makini na kazi unayoomba
 
Mshahara unalipwa kutokana na kiwango Cha uzalishaji wa mtumishi husika na sio kiwango Cha elimu,unaweza ukawa na PhD lakini umhimu wako ukazidiwa na mwenye diploma
 
Ila kaka izo taasisi usidhani ni rahisi kuingia hata pale utumishi ni fair ila interview zao ni balaa hamna upendeleo ila izo paper unakuta katika job description wameandika "an attractive salary scale is offered for qualified candidates " hapo ni wewe tu jitihda zako

Kaka hamna shortcut na katika izo taasisi ujue kuna siri kubwa na masharti mengi kwa wafanyakazi tofauti na huko kwingine wacha salary ziwe tofauti kwa kweli

Kikubwa we unayo nafasi pia kuomba ajira kama zikitoka piga mahesabu TRA watu wanafanya ukusanyaji wa mabilion labda finance wapale wanacalculate na kumanage matrillion ufanananisha na hapo Ruvuma almashauri mwaka mzima wanakusanya sijui bil kumi na kitu then mlipwe sasa hamna kitu kama icho

Na hizo taasisi hazina wafanyakazi wengi nyingi hutoa gawio

Nb; kwa awamu hii zitaongezeka mfano mawakala wa malls so msisite kuomba huko kuna maslahi
 
Nilishangaa kuona salary slip ya ndugu yangu mmoja ambae ni police mwenye cheo cha ACP,ni RTO kwenye moja ya mikoa hapa nchini..mshahara wake kabla ya makato ni 2.1m..nikajisemea ndio maana police wanakula rushwa sana asee.yani cheo kikubwa afu mshahara kiduchu.
 
Kwani mnasoma ili muwe na mishahara minono au kuongeza maarifa
Ukiongeza maarifa unaongeza ufanisi wa ufanyaji kazi katika sekta yako mfano,, Kuna daktari amesoma miaka 5 degree lakini Kuna daktari bingwa mwenye super specialization, huyu kaongeza elimu yake Ina maana ana uwezo wa kufanya Mambo mengi kuliko uyo wa degree hapa maarifa yake lazima yambebe ATA kwenye mshahara wake mkuu..ukisema tusome kwa ajili ya maarifa tu afu kiwango Cha mshahara kibaki kilekile bila kuangalia elimu ya mtu sizani Kama leo hao wanaoitwa wabobezi katka sekta flani wangekuepo maana ingekua ni Kama kujichosha tu.
 
Sio lazima mmoja amfuate mwenzie,unawezatafutwa wastani.
Kati ya laki 9 Na 2m. MF wanawezalipwa 1.4m.
Technically unachosema ni kwamba yule wa 2mil ashushwe ili awe anaipata 1.4m.

Kwa ufupi ni kwamba unasema mwenye mshahara wa 2mil ASHUSHWE.

Hiyo ndio roho mbaya ninayozungumzia hapa sasa. Sasa huyo akishushwa inakuwa imekusaidia nini wewe kwa mfano.
 
Kwani mnasoma ili muwe na mishahara minono au kuongeza maarifa
Kama hayo maarifa huyatumii unaenda kuwa bodaboda kulikuwa na haja gani ya kupoteza muda miaka 25 unasoma halafu aliyesoma miaka 11 anakuzidi kipato?
 
Burundi wao wameanza utaratibu mpya kuwa ni amri hata wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye mashirika ya UN, yaliyopo burundi azima mishahara yao ilingane na watumishi wengine wa serikali!!!kwani kazi wanazofanya huko hata wenzao walioko serikalini wanaweza zifanya!!Africa kuna vituko sana!!
UN si serikali. Huwezi sema walingane mishahara wkt UN ni taasisi ambayo si ya serikali
 
Watumishi wa umma wa Tanzania ni kikundi cha watu wasiojitambua. Inafikia mahali wao wanajifanya kama wana Ccm! Ivi unaweza kwenda nchi gani wafanyakazi wasiongezewe mishahara kwa miaka mitano na bado wanaenda kazini bila hata kuhoji??? Na raisi anakwambia kabisa sitaongeza mishahara ambayo ni takwa la kisheria wao wapo tu wameinamisha vichwa kama KONDOO anayekwenda kuchinjwa
Hovyooo
 
Dah! Wewe jamaa mbona unatunanga hivi!!! Tunachukua hatua kwa tahadhari. Huyu jamaa humfahamu kama ni dkteta uchwara? Sasa akitufukuza kazi huoni familia zetu zitateseka!

Tumeshaingia kwenye ujasiriamali na pia kilimo tofauti kabisa na ilivyokua enzi za JK
Kwa sasa wengi tumeamua kufanya kazi kwa mazoea! Tumepoteza morali ya kazi! Tumempuuza na kumdharau, nk.

Hatua zote hizi hazitoshi tu!! Usisahau kwenye vyama vyote vya wafanyakazi wameshawekwa watu wake wanao mlamba miguu kuviongoza kama ilivyo kwenye taasisi nyingine, hivyo usitegemee working class movements za aina yoyote ile kutokea.. Kwa sasa tunaishi kwa akili na tahadhari kubwa! Hivyo mtuchukulie tu.

Kiukweli inaleta maudhi kuona tunaendeshwa kama magari mabovu na mtu mmoja tu na kwa utashi wake. That man is a devil!! Miaka zaidi ya sita, mshahara ni ule ule! No promotion, no annual incriment!!
 
Dah! Wewe jamaa mbona unatunanga hivi!!! Tunachukua hatua kwa tahadhari. Huyu jamaa humfahamu kama ni dkteta uchwara? Sasa akitufukuza kazi huoni familia zetu zitateseka!

Tumeshaingia kwenye ujasiriamali na pia kilimo tofauti kabisa na ilivyokua enzi za JK
Kwa sasa wengi tumeamua kufanya kazi kwa mazoea! Tumepoteza morali ya kazi! Tumempuuza na kumdharau, nk.

Hatua zote hizi hazitoshi tu!! Usisahau kwenye vyama vyote vya wafanyakazi wameshawekwa watu wake wanao mlamba miguu kama ilivyo kwenye taasisi nyingine. Kwa sasa tunaishi kwa akili na tahadhari kubwa! Hivyo mtuchukulie tu.

Kiukweli inaleta maudhi kuona tunaendeshwa kama magari mabovu na mtu mmoja tu na kwa utashi wake. That man is a devil!! Miaka zaidi ya sita, mshahara ni ule ule! No promotion, no annual incriment!!
Hahaha zumbe mkuu.
Kwanza huyu kiongozi ni muoga sana kwa wafanyakazi aliingia tu madarakani aliwahonga mamilioni na kuwapeleka kusoma nje watoto wa viongozi wote wa vyama vya wafanyakazi ngapi ya taifa ili waufyate
 
Kwa sasa tunajipa tu matumaini ya kwamba ipo siku ataondoka na hivyo maisha yatarudi kuwa normal. Huyu mzee anafanya mambo makubwa sana kwenye miundombinu. Kwa hilo hakuna wa kulipinga.

Anapozingua ni pale anapowanyima wafanyakazi haki zao za msingi, kwa kigezo cha kujenga hiyo miundombinu. Na mbaya zaidi katika hilo kundi la wafanyakazi, kuna wengine haki zao wanapewa kwa wakati. Mfano Wanajeshi. Ila wengine ndiyo wanaonewa.

Yaani ni kitu kinacholeta maudhi kuona mtumishi aliye ajiriwa mwaka 2014 yuko daraja sawa na aliye ajiriwa mwaka 2020! Enzi za JK, huu uonevu haukuwepo. Badala ya kuongeza mshahara, yeye anaongeza makato ya Bodi ya Mikopo!! Yule Mzee ni mkatili sana.
 
UN si serikali. Huwezi sema walingane mishahara wkt UN ni taasisi ambayo si ya serikali
Ndio hapo sasa!!!, serikali ya burundi mbona ilishatoa maagizo hayo toka mwaka jana!!kuwa haitaki utofauti huo, kwani serikali za kidikteta, zina shindwa jambo?!!wao wanashindwa kuboresha masilahi ya wafanyakazi wao, wanakimbila kuona kuwa wanaolipa vizuri, wanawagombanisha!!
 
Burundi wao wameanza utaratibu mpya kuwa ni amri hata wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye mashirika ya UN, yaliyopo burundi azima mishahara yao ilingane na watumishi wengine wa serikali!!!kwani kazi wanazofanya huko hata wenzao walioko serikalini wanaweza zifanya!!Africa kuna vituko sana!!
Na bahati mbaya baadhi ya hawa wanaolipwa vizuri wanajisahau na kudharau wengine wakati wote mna elimu sawa na mnatumikia serikali moja.
 
Kutaka watumishi wote serikalini wafanane mishahara ni ujinga,
Mtu lazima alipwe kutokana na unyeti wa taasisi aliyopo,Dereva wa jaji mkuu,awezi kulipwa sawa na dereva wa Tanesco anayepereka mafundi site,
Dereva wa jaji lazima awe na mavazi stahiki,suti,huyu anatunza siri,ukipata hii nafasi lazima ulipwe vzr Ili uendsne na boss na ofisi unsyoihudumia,dereva wa Tanesco,dawasa,muruwasa,Hawa ni kuvaa overlol tu,
Mentality ya kipumbavu na kibaguzi kabisa! Huu ni ukaburu sawa na ule wa kubaguana kwa rangi.
 
mtoa mada anahoja nzuri ila watu humu wanatoa majibu sio mfano mm nina jamaa zangu nilisoma nao chuo fulani wanemalia degree ya elimu hesabu na wote gpa zao ni 4.2 mmoja aliajiriwa kufundisha shule ya secondary mshahsra TGTS D1 ni 716,000 apo hajakatwa makato mwingine aliajiriwa kama tutor udsm mshahara ni 1.6M

kumbuka wote elimu sawa kabisaaa

shida hapa serikali inatakiwa kuwavuta wale wenyemishahara midogo angalau wapande wafanane na wengne
Ulichopendekeza ndio kinatakiwa kufanywa na serikali yenye watu makini na wapenda haki.
 
Back
Top Bottom