Utoto wa Fei Toto utawasumbua wachezaji wa Kizanzibari

Utoto wa Fei Toto utawasumbua wachezaji wa Kizanzibari

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Mpira ni furaha na mpira ni ajira pia. Lakini mpira una sheria, kanuni na taratibu zake. Fei Toto kuiacha Yanga katikati ya mashindano ya African championship, ligi kuu, Azam cup na mapinduzi cup sio Cha mtu muungwana hata kidogo na kinaudhi kila mtu mwenye akili lazini.

Lakini kuondoka kwake kihuni kinahusika sana na uzanzibar wake, Yaani aliyemtorosha ametumia uhusiano wa mchezaji ña aliyemrubuni.

Hii inaweza kusababisha Yanga kwasasa isitafute vipaji Zanzibar,
 
Nyie mtahangaika sana kutafuta hatia ya Feisal lakini kama tatizo basi linaanzia hapo kwenye uongozi.

Maslahi ya mchezaji ni kitu muhimu sana, usiione thamani ya mchezaji punde tu baada ya yeye kuonesha dalili ya kutaka kuondoka

Ni kama saizi mnavyotumia muda mwingi kutafuta makosa ya Feisal wakati huu ulikuwa ni muda mzuri wa kurekebisha na kuboresha maslahi ya wengine ambao wamesalia ili lisije kutokea tena.
 
Mpira ni furaha na mpira ni ajira pia. Lakini mpira una sheria, kanuni na taratibu zake. Fei Toto kuiacha Yanga katikati ya mashindano ya African championship...
Mwacheni kijana wa watu hakuna mtu alimnunulua viatu wakati akianza kucheza , hakuna mtu alimnunulia chakula alipokuwa mtoto, ukiwa mshabiki unaamini mchezaji ni Mali Yako , yaani wewe na club ni dada na kaka mawazo ya hovyo kabisa.
 
Mpira una mengi.
Huwezi kuongeza mishahara ghafla bila kuwa na bajeti na fedha.

Kama mchezaji anaona anapata asichostahili Yanga basi akatafute kwingine atakapo ridhika.
Na ndicho alichofanya kijana
 
Acha fei toto aende nafikiri sisi WANANCHI ni zaidi ya fei toto kama walipita WAKINA edibily Jonas lunyamila ,akida makunda, sekilojo chambua sembuse feitoto nafikiri ameondoka wakati sahihi acha akatafute riziki kwingine ila WANANCHI sio kwamba tuatashindwa kucheza kisa feitoto
 
Mpira ni furaha na mpira ni ajira pia. Lakini mpira una sheria, kanuni na taratibu zake. Fei Toto kuiacha Yanga katikati ya mashindano ya African championship...
Morrison naye ni mzanzibar? Mbona aliwapiga na kitu kizito kichwani na bado mkamrudia kumsajiri ?
 
Nyie mtahangaika sana kutafuta hatia ya Feisal lakini kama tatizo basi linaanzia hapo kwenye uongozi...
Kama aliona maslahi madogo, asingekubali kusaini mkataba mpya. Kwani yeye ni mtoto mdogo asijue kukataa kuwa msiponilipa kiasi fulani sisaini mkataba mpya.

Lakini kukubali kwake kusaini mkataba mpya unaoishia mwaka 2024 inamaana karidhika na kiwango hicho

N B mkataba ni makubaliano ya pande mbili
 
Mpira ni biashara.

Fei toto anauza ujuzi wake kwenye timu.

Iwe yanga ama Azam ama Geita lazima waweke offer mezani
 
Mpira una mengi.
Huwezi kuongeza mishahara ghafla bila kuwa na bajeti na fedha.

Kama mchezaji anaona anapata asichostahili Yanga basi akatafute kwingine atakapo ridhika.
Hilo la bajeti na fedha kweli ni changamoto na kwa mazingira hayo wala sina noma na Club ambayo imeshindwa kuongeza mkataba mzuri kwa mchezaji

Lakini kwanini alipotishia kuondoka Club ilikuwa tayari kuongeza hiyo pesa aliyosemekana kuihitaji?

Ilitoka wapi kama tatizo ni bajeti ya fedha?
 
Mbona mnamsakama sana mtoto wa watu, pesa yenyewe mnamlipa kama mwalim wa primary 3M, nao ni mshahala wa kumlipa kwa level yake kwanza hautoshi hata matumizi tu ya family.

Utopolo tumieni akili wakati mwingine, kambole mmemfungia ndani miezi 4 mnamlipa 10M, feitoto anae toa jasho kila siku 3M.

Qmmke zenu, acheni akatafute pesa kwa wanao mdhamini
 
Kama aliona maslahi madogo, asingekubali kusaini mkataba mpya. Kwani yeye ni mtoto mdogo asijue kukataa kuwa msiponilipa kiasi fulani sisaini mkataba mpya. Lakini kukubali kwake kusaini mkataba mpya unaoishia mwaka 2024 inamaana karidhika na kiwango hicho

N B mkataba ni makubaliano ya pande mbili
Kipindi anasaini mkataba mwaka hakuwa na power ya kuweza kusililizwa kwasababu hakuwa na plan B itayomsaidia endapo wasopofika makubaliano

Vipi kama alijaribu kugusia swala la Yanga wamuongezee mshahara ila walimu ignore kwasababu walijua hana jeuri ya kwenda sehemu yeyote kwakua hakuna timu iliyomuhitaji kwa wakati huo?

Lakini kitu kingine wisely ni kwanini swala la kuongeza mshahara mpaka liombwe na mchezaji?

Kwani uongozi wenyewe hauoni mchango au thamani ya mchezaji kustahili malipo zaidi ya hayo mpaka mchezaji mwenyewe aombe?
 
Acha fei toto aende nafikiri sisi WANANCHI ni zaidi ya fei toto kama walipita WAKINA edibily Jonas lunyamila ,akida makunda ,sekilojo chambua sembuse feitoto nafikiri ameondoka wakati sahihi acha akatafute riziki kwingine ila WANANCHI sio kwamba tuatashindwa kucheza kisa feitoto
Bila kusahau nonda Shaban

Sent from my Redmi Note 8 Pro using JamiiForums mobile app
 
Kipindi anasaini mkataba mwaka hakuwa na power ya kuweza kusililizwa kwasababu hakuwa na plan B itayomsaidia endapo wasopofika makubaliano...
Mkuu haya magazeti unayoyaandika kila unapoletwa Uzi kuhusu saga ya Feitoto hayawezi kupeleka ubingwa pale msimbazi.

Hizi nguvu ungezitumia kuuhoji uongozi wa Simba kutoa majibu kwanini CEO amejiuzulu, ungehoji kwanini makombe yamekauka gafla Simba na kuhamia Yanga, kwanini Simba imekuwa mnyonge Kwa Yanga, Hapo ungekuwa umetumia vizuri maandishi yako kwa manufaa ya timu yako pendwa na labda ingepelekea kurudisha furaha yako..

Huu ni ushauri wa bure
 
Sielewi mnataka feisal acheze yanga hadi uzee wake. Sheikh katimiza matakwa ya mkataba na hataki kua mwajiriwa sehemu anapoona ujuzi wake hauna dhamani.

Tuache akajenge maisha kwingine
 
Mkuu haya magazeti unayoyaandika kila unapoletwa Uzi kuhusu saga ya Feitoto hayawezi kupeleka ubingwa pale msimbazi...
Hili ni jukwaa la michezo, kama hujui upo wapi unaweza ukatoka nje usome vizuri bango ujue upo mahala gani na zinajadiliwa mada za aina gani.

Ingekuwa jukwaa la michezo linahusisha mada za ubingwa pekee nadhani tungekuwa na mada moja kwa mwaka mzima.

Unalazimisha watu waongee mada zinazohusu ubingwa at the same time unanitaka nimjadili former CEO. Hueleweki

Feisal kaondoka huku mashabiki wa Yanga mkiwa mmetuacha njia panda

Mmeridhia Feisal kuondoka na ndio maana baada ya game yenu na Azam mli shout "hatumtaki Feisal"?

Au bado mnamuhitaji na ndio maana mko tayari kususia bidhaa za Azam kama njia moja yapo ya kulipiza maumivu??

Nataka nipate majibu hayo kwa mashabiki wa Yanga wa humu JF
 
Back
Top Bottom