Utoto wa Fei Toto utawasumbua wachezaji wa Kizanzibari

Utoto wa Fei Toto utawasumbua wachezaji wa Kizanzibari

Hata kama ndio mumlipe laki nne
 
Nyie mtahangaika sana kutafuta hatia ya Feisal lakini kama tatizo basi linaanzia hapo kwenye uongozi.

Maslahi ya mchezaji ni kitu muhimu sana, usiione thamani ya mchezaji punde tu baada ya yeye kuonesha dalili ya kutaka kuondoka

Ni kama saizi mnavyotumia muda mwingi kutafuta makosa ya Feisal wakati huu ulikuwa ni muda mzuri wa kurekebisha na kuboresha maslahi ya wengine ambao wamesalia ili lisije kutokea tena.
Thamani ya mchezaji mahiri inaonekana pale anapotaka kuongeza mkataba na anapovunjiwa mkataba na timu nyingine, Feisal ametengenezwa kwa gharama kubwa hadi aonekane mchezaji mkubwa.

Amelishwa, amevalishwa, amenolewa na makocha Bora kabisa wanaolipwa hela ndefu ambao wamemuongezea thamani hii inayoringa nayo, club nilazima imuuze na sio kuchukuliwa kihuni. Timu zitaona ukakasi kutengeneza mpumbavu mwingine wa aina hii.
 
Thamani ya mchezaji mahari inaonekana pale anapotaka kuongeza mkataba na anapovunjiwa mkataba na timu nyingine, Feisal ametengenezwa...
Mkuu kusema Yanga imemtengeneza Feisal nakataa

Yanga ingekuwa ina huo uwezo wa kutengeneza wachezaji leo hii Makambo angekuwa bora zaidi kuliko alivyo

Au wale wachezaji mliokatisha mikataba yao na kuamua kuachana nao baada ya kutoridhishwa na viwango vyao.

Hayo yote yasingewezekana kama mna taaluma ya kumtengeneza mchezaji.

Feisal alikuwa na kipaji cha mpira tangu mdogo, Yanga amepata uzoefu tu.

Kumvalisha na kumlisha mchezaji sio big deal kuitumia kama pay back kwa mchango wake uwanjani.

Wachezaji wangapi wanazidiwa uwezo na Feisal mnawavisha na kuwalisha na bado mshahara wao ni mlima kuliko Feisal??

Wenzenu walioona thamani ya miguu yake ndio hao walioamua kumpa kile ambacho kinamridhisha bila kuangalia vitu vidogo kama kuvaa na kula

Kwasababu wote mmemjua akiwa mkubwa, kipindi yupo mtoto unafikiri alikuwa analala njaa au kutembea uchi?

Tubadilike tuthamini wachezaji
 
Acha fei toto aende nafikiri sisi WANANCHI ni zaidi ya fei toto kama walipita WAKINA edibily Jonas lunyamila ,akida makunda ,sekilojo chambua sembuse feitoto nafikiri ameondoka wakati sahihi acha akatafute riziki kwingine ila WANANCHI sio kwamba tuatashindwa kucheza kisa feitoto
Binafsi sikatai mchezaji kuiacha timu kwenda timu nyingine. Lakini ziko taratibu za kimpira za kujiunga na kuondoka kwenye timu.

Tabia za Akina canavaro silisababisha Yanga iwe kipenzi Cha wachezaji wengi wa Zanzibar, lakini tabia ya Fei Toto nayo itasababisha Yanga iwachukie pia.

Eti mtu anasema Mimi ndiye kocha wake wa timu ya utotoni niliyevumbua kipaji chake, hivyo nimemshauri aende akatafite maslahi zaidi,
 
Morrison naye ni mzanzibar? Mbona aliwapiga na kitu kizito kichwani na bado mkamrudia kumsajiri ?
Issue ya Morrison ni tofauti kabisaa na ya huyu mwehu, Morrison kaja Yanga akiwa mchezaji mkubwa kabisa lakini Fei kaja Yanga akiwa mchezaji mdogo kabisa.

Yanga ilakikuza kipaji chache kwa gharama kubwa ya mabenchi ya ufundi na mazingira Bora ya kucheza mpira. Mbona Msuva aliondoka na watu hawana kinyonyo nae?
 
Kama aliona maslahi madogo, asingekubali kusaini mkataba mpya. Kwani yeye ni mtoto mdogo asijue kukataa kuwa msiponilipa kiasi fulani sisaini mkataba mpya. Lakini kukubali kwake kusaini mkataba mpya unaoishia mwaka 2024 inamaana karidhika na kiwango hicho

N B mkataba ni makubaliano ya pande mbili
Huwa nawashangaa sana wanaosema na kuwa analipwa kidogo wakati aliridhia mwenyewe kulipwa hicho na akasaini
 
Kipindi anasaini mkataba mwaka hakuwa na power ya kuweza kusililizwa kwasababu hakuwa na plan B itayomsaidia endapo wasopofika makubaliano...
Kama hakuwa na jeuru ya kwenda popote maanake hakuwa na ubora/ kiwango cha kumpeleka popote au unataka kusema alikuwa ajitambui?
 
Nyie mtahangaika sana kutafuta hatia ya Feisal lakini kama tatizo basi linaanzia hapo kwenye uongozi...
Mkuu mlitaka apewe sh ngapi nyie viazi? Maslah ya mchezaji hayarekebishwi katkat ya mkataba ... Fei kiwango chake kimepanda akiwa kat kat ya mkataba, katika kurenew mkataba angeomba hayo maslah kama angenyimwa angetimka Zake, ndo wanavyofanya wachezaji wengi tuu worldwide, Sadio Mane ni mfano.

Fei karubuniwa na hajafanya uungwana , kama demand ilikuwa kubwa Sana walau angechora mwisho wa msimu
 
Si eisal Salum peke yake.

Wachezaji Wengi wa Kibongo na viongozi wao wote Wana Akili fupi mno.

Akili zao ni ndogo sana.
Hawajui kujipambania.
Hawajui Thamani Yao.
Hawajui Haki zao.
Wavivu.
Wanaridhika na vitu vidogo mno.

BONGO NI TATIZO
 
Yanga ni Taasisi, Imeanza toka 1930's huko, Walishakuja na kusepa wengi mno! Yanga haiwezi kupoteza kwakua Fei hayupo, lakini pia Yanga haikusema Fei afie jangwani, issue ilikua ni kuondoka kiungwana!! Kauzwa CR 7, Wyne Rooney na wengine wakali wengi sembuse Fei.. So issue ilikua ni kuondoka kwa njia rasmi. Pesa isiondoe Utu na ubinadamu.
 
Mpira una mengi.
Huwezi kuongeza mishahara ghafla bila kuwa na bajeti na fedha.

Kama mchezaji anaona anapata asichostahili Yanga basi akatafute kwingine atakapo ridhika.
Huwezi kuongeza mshahara gafla na hapo hapo wageni wanakuja na kulipwa Mara sita ya kile unachopata mzawa na mzawa unakua ndie injini ya timu yaan unavuja jasho unapambania timu hao wageni wanaolipwa pakubwa wakiwa wachezaji wa kawaida tu.

Msuli tembo mshahara sungura, embu tuwaheshimu watanzania wenzetu ,kutajirisha mtoto wa jiran wkt wa kwako yupo na Ana sifa za kuwa tajir huo ni uchawi
 
Nyie mtahangaika sana kutafuta hatia ya Feisal lakini kama tatizo basi linaanzia hapo kwenye uongozi.

Maslahi ya mchezaji ni kitu muhimu sana, usiione thamani ya mchezaji punde tu baada ya yeye kuonesha dalili ya kutaka kuondoka

Ni kama saizi mnavyotumia muda mwingi kutafuta makosa ya Feisal wakati huu ulikuwa ni muda mzuri wa kurekebisha na kuboresha maslahi ya wengine ambao wamesalia ili lisije kutokea tena.
Suala maslahi ni zuri kwa kila mtu ila hapo inakuja wakati anasaini ule mkataba akuliona hilo?jibu ni hapana aliliona ila kipindi anasaini akua na thamani aliyokua nayo sasa,

so kuna vipengele kwenye ule mkataba wa kumuongezea mshahara na mahitaji mengine,na Yanga wala hawajakataa kukaa nae ila inachoonyesha dogo kuna watu nyuma yake wanaomshawishi na wala sio vibaya basi kistaarabu na hao watu wangeenda kukaa na Yanga na sio kama njia ambazo wanatumia
 
Mpira ni furaha na mpira ni ajira pia. Lakini mpira una sheria, kanuni na taratibu zake. Fei Toto kuiacha Yanga katikati ya mashindano ya African championship, ligi kuu, Azam cup na mapinduzi cup sio Cha mtu muungwana hata kidogo na kinaudhi kila mtu mwenye akili lazini. Lakini kuondoka kwake kihuni kinahusika sana na uzanzibar wake, Yaani aliyemtorosha ametumia uhusiano wa mchezaji ña aliyemrubuni.

Hii inaweza kusababisha Yanga kwasasa isitafute vipaji Zanzibar,
Fei...kaondoka kihalali kabisa hata viongozi wenu wanafahamu hilo ila wanaficha tu.
 
Kama aliona maslahi madogo, asingekubali kusaini mkataba mpya. Kwani yeye ni mtoto mdogo asijue kukataa kuwa msiponilipa kiasi fulani sisaini mkataba mpya. Lakini kukubali kwake kusaini mkataba mpya unaoishia mwaka 2024 inamaana karidhika na kiwango hicho

N B mkataba ni makubaliano ya pande mbili
Na mkataba huo huo ulitoa mwanya wa upande moja kuvunja mkataba na ukaweka na kiasi maalumu endapo mchezaji atahitaji kuvunja mkataba wakati wowote kabla ya 2024.Feisal ametumia hicho kipengele pia ambacho ni sehemu ya huo mkataba.
 
Nyie mtahangaika sana kutafuta hatia ya Feisal lakini kama tatizo basi linaanzia hapo kwenye uongozi.

Maslahi ya mchezaji ni kitu muhimu sana, usiione thamani ya mchezaji punde tu baada ya yeye kuonesha dalili ya kutaka kuondoka

Ni kama saizi mnavyotumia muda mwingi kutafuta makosa ya Feisal wakati huu ulikuwa ni muda mzuri wa kurekebisha na kuboresha maslahi ya wengine ambao wamesalia ili lisije kutokea tena.
Hivi unaongelea ushabiki au? Mchezaji ana mkataba wa miaka 2 mbele,club imegoma kumuuza, kwanini asisubiri mkataba wake uishe ndio aondoke bure kama hajaridhika na maslahi?
 
Na mkataba huo huo ulitoa mwanya wa upande moja kuvunja mkataba na ukaweka na kiasi maalumu endapo mchezaji atahitaji kuvunja mkataba wakati wowote kabla ya 2024.Feisal ametumia hicho kipengele pia ambacho ni sehemu ya huo mkataba.
Mkuu hili umedakia tu kwa mbele. Ila kuna mtu nilikuwa namjibu hoja yake ya kusema kuwa eti tatizo ni kulipwa ela ndogo. Hiyo ela ndogo mchezaji angekuwa anaiona ni ndogo asingesaini mkataba mpya na Yanga. Hilo la kuweka kipengele cha kuvunja mkataba kwa kiasi hiko ni swala lingine ambalo ni makosa ya uongozi wa Yanga kuweka kipengele cha ukichaa kiasi hiko
 
Kama aliona maslahi madogo, asingekubali kusaini mkataba mpya. Kwani yeye ni mtoto mdogo asijue kukataa kuwa msiponilipa kiasi fulani sisaini mkataba mpya.

Lakini kukubali kwake kusaini mkataba mpya unaoishia mwaka 2024 inamaana karidhika na kiwango hicho

N B mkataba ni makubaliano ya pande mbili
Yanga ilipojitela ni pale tu ilipoweka kipengele cha Fieitoto kuilipa Yanga milioni 100 na mishahara ya miezi 3 endapo atataka kuvunja Mkataba,mengine yote haya ni maongezi ya kunogesha kijiwe cha JF tu
 
Back
Top Bottom