Utoto wa Fei Toto utawasumbua wachezaji wa Kizanzibari

Mkuu hawa mashabiki wengi wa simba wameamua kulivalia njuga hili swala, wamesahau mwenendo mzima wa timu yao sasa kila dosari kwa Yanga kwao ni Furaha au ( Kombe) . Nje & Ndani wanajua hata Fei akisepa bado Yanga ni tishio kwao.
Fei hajacheza game ngapi mpaka sasa? Yanga imekosa matokeo jibu ni hakuna...! huko kimataifa Fei alionesha kitu kipi? hakuna Fei ni mchezaji kipenzi wa mashabiki na Viongozi tu ila uwanjani ni wakawaida tu...
 
Kwahiyo kama kiwango chake kingekuwa kibovu baada ya kusaini angeomba apunguziwe mshahara? kaka usajili ni kama kamali (gambling), Fei amekosea sana, kiwango chake alichokionyesha kingemsadia sana wakati wa kuongezewa mkataba au kununuliwa na timu nyingine, hivyo yanga na Fei wangecheza win-win situation kwa furaha kabisa. Tamaa mbaya, maana tamaa na heshima havikai nyumba moja.
Ni kosa kwa timu kuongea na mchezaji wa timu nyingine kuhusu uhamisho. Kama kuna timu nyingine zinamtaka kwa bei kubwa angesubiri wakati Yanga inataka kumuongezea mkataba wake. Angewapa masharti yake kabla ya kukubali kusaini mkataba mpya. La sivyo, kama anatakiwa haraka na hiyo timu timu husika ingetoa offer yake kwa Yanga ili ikubali kumwachia mchezaji wake dirisha dogo. Alichofanya Fei ni sawa na binti aliyechukua pesa kwa mchumba na kwenda kumlipa baba yake gharama za kumlea ili aende kuolewa bure na bwana huyo.
 

Umeandika pumba, sounds like you are from there.kinachoamua mshahara wa mchezaji ni makubaliano waliofikia wakati wanajadili mkataba wake. Kama anaona thamani yake imepanda anasubiri mkataba uishe aanze mazungumzo mapya ya kuuboresha mkataba au kuuvunja.
Achana na hisia za vijiweni
 
Punguza mihemko mbona hta Yanga hua wanawafanyia wengine uhuni au mkuki Kwa nguruwe kwa binadamu unauma
 
Hivi mbona Azam hawajasema chochote kuhusu hili sakata? Ukute wahusika ni wengine kabisa Azam ni chambo tu[emoji23][emoji23]
 
Fei Hana hatia kafuata taratibu zote kuvunja mkataba wake walaumuni viongozi wenu Kwa kuingia naye mkataba wa ovyo
 
Kwanini asubiri mpaka mkataba uishe wakati mkataba huo huo una kipengele kinachoruhusu uvunjwe wakati wowote kwa kulipa 100M na mishahara ya miezi mitatu?
 
Kwanini asubiri mpaka mkataba uishe wakati mkataba huo huo una kipengele kinachoruhusu uvunjwe wakati wowote kwa kulipa 100M na mishahara ya miezi mitatu?
Kwa akili zako unadhani mtu anavunja mkataba akiwa amejifungia chumbani mwake? Rage toa elimu huku!!
 
Naona simba mmekua watetezi wa feisal kama suala ni masilahi hv kipindi miquisone na chama wanaondoka mbona mashabiki mlirusha sana lawama kwa uongozi je hamkujua kama kule wanapoenda masilahi yao yalikua makubwa zaidi? Alichokifanya feisal sio uungwana kwa heshima yake angekaa tu mezani na uongozi wamalizane katika maisha ujui kesho yako uko anapoenda anaweza akaflop akarudi tena yanga kama ilivyokua kwa chama na kisinda
 
Kwani kaondoka kwa njia isiyo rasmi ?.... 🙂
 
Uliisoma announcement ya Yanga kuhusu swala la Feisali?

Uongozi wa Yanga ulisema ulikuwa tayari kuboresha mshahara wake pamoja na ku extend mkataba

Sasa kama haiwezekani mshahara kuongezeka kabla ya mkataba kuisha ina maana Yanga ilikuwa inataka kufanya ulaghai??
 
Kwa akili zako unadhani mtu anavunja mkataba akiwa amejifungia chumbani mwake? Rage toa elimu huku!!
Wewe unahitaji kupumzika kwanza,uko so frustrated na swala la Feisal mpaka kila mtu unamtolea povu.Maisha hayapo hivyo ndugu [emoji3][emoji3]
 

Sawa uneandika Point..
ila wewe ni Yanga Damu![emoji123][emoji12]
 
Labda tuombe mkataba wa Yanga na Fei umeandikwa nini kuhusu kuvunja mkataba. Inawezekana Fei alikitumia kifungu hicho kwenye makataba kama kilivyo. Tunachokisema sisi ambacho kinaudhi wengi ni kukosekana kwa busara na hekima katika kukitumia hicho kifungu. yaani inaonekana kama vile Fei aliwekewa sumu kwenye chakula, hivyo anakimbia kujinusuru. Binafsi mimi siungi mkono Yanga kumuongeza mshahara Fei kwa njia ambazo ni kinyume na mkataaba wake. Hii ingesababisha Yanga isitawalike hata kidogo, kila mchezaji angedai kutendewa the same, ila naunga mkono Fei kuongezewa maslahi wakati wa kuongeza kandarasi yake kutoka na perfonce yake. Kipaji pekee hakitoshi katika kufanikisha mambo, bali utahitaji kuwa mwaminifu, hekima, busara na subra. Hata timu inayotaka kumsajili kwa njia hii itamdharau sana Fei, wataishi nae kwa tahadhari kubwa kwa kuwa haaminiki. Kuna mfanyakazi mwenzetu alikuwa amepata kazi nzuri yenye maslahi makubwa kwenye shirika la kimataifa, lakini aliwaambia kuwa hawezi kuripoti kwao mpaka kwanza akamilishe kazi alizozianza za mwajili wake wa sasa. Lile shirika walikubali amalizie kazi za mwajili na azikabidhi kabla hajaondoka,. Walimheshimu na kumuamini sana yule kijana kwa kitendo kile. Angekuwa mtu kama Fei toto angeacha kazi siku hiyohiyo na kusema shauri zao mimi naenda UN kwenye maslahi makubwa.

Fei ameiambia Yanga shauri yenu mimi naondoka.
 
Huyu Mudathir mliyemsajil ni Muha??
Nikajua ndio mmesusa kuwasajili wanzibar tena maana nyie mpaka leo mnahisi kumsajili mchezaji wa ndani ni kama kumsaidia hivyo maslahi mumpangie yoyote mnayopenda na asihoji
 
Huyu Mudathir mliyemsajil ni Muha??
Nikajua ndio mmesusa kuwasajili wanzibar tena maana nyie mpaka leo mnahisi kumsajili mchezaji wa ndani ni kama kumsaidia hivyo maslahi mumpangie yoyote mnayopenda na asihoji
Hakuna anaemshobokea, au huoni!!! Hata kwa kumuangalia TU usoni na anavyoongea na kujiekeza utagundua TU kuwa Fei ana shida ya akili sio kama mudathir. Mudathir ni mwanaume lakini Fei ni kivulana fulani hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…