Utumishi, Wizara ya Fedha na TAKUKURU kwanini mnaruhusu watumishi wa umma kukopea mishahara yao hadi Senti ya mwisho? Hamuoni kuwa inachangia Rushwa?


huu ni uongo. unaongea kwa assumption tuu. huo mkopo nani anaupitisha??
 
Fedha yako haina kazi, Iko siku utakopa usomeshe watoto, ulipe Kodi, hospital na kutunza wazee nyumbani, hutaandiki utumbo ulioandika.
 
Unashangaa kukatwa mshahara wote hiyo haitoshi watu wanakopa tena kwenye visakosi vya mitaani ambapo wanashikilia kadi ya benki, hivyo kinachobakia baada ya benk kukata nacho kinamezwa na sakosi.

Maisha ni magumu kuliko unavyoelewa.
 
Sheria ipo hivyo,Ila maafisa utumishi huwa wanapigwa sound hasa kwa watu wa ngazi za juu huku ,Kuna watu nawafahamu wanapokea elfu 60 Yani mtu kakopa m .40

Hilo haliwezekani tu kwa wachovu na watu wa halmashauri
 
Sheria ipo hivyo,Ila maafisa utumishi huwa wanapigwa sound hasa kwa watu wa ngazi za juu huku ,Kuna watu nawafahamu wanapokea elfu 60 Yani mtu kakopa m .40

Hilo haliwezekani tu kwa wachovu na watu wa halmashauri
Mimi bodi ya mkopo waliponitia kidole nilibakiwa na 160,000/= hapo Nina mke na mtoto, kodi ya pango, nauli ya kazini na mengine mengi. Maisha yana siri nyingi sana
 
Mimi bodi ya mkopo waliponitia kidole nilibakiwa na 160,000/= hapo Nina mke na mtoto, kodi ya pango, nauli ya kazini na mengine mengi. Maisha yana siri nyingi sana
Kwa mtumishi sishangai ,Ila ukimsimulia raia ataona uongo tu,wanajuaga tunalipwa labda million 2, 3 hahaha
 
Mtumishi yoyote wa Umma, ili afanikiwe walau kujenga kibanda, kununua gari, kubuni biashara mkopo hauepukiki.

Kufikiria eti , akikopa mkopo mkubwa na kupokea pesa ndogo mwisho wa mwezi basi huyo ni mla rushwa ni kuwakosea adabu watumishi.

Kama unaoushahidi kwa hilo peleka unakolalamikia, watumishi wengi magari yao yanatumika kutoa huduma kwa umma huku wakiwa na hiyo mikopo.
 
Kwa mtumishi sishangai ,Ila ukimsimulia raia ataona uongo tu,wanajuaga tunalipwa labda million 2, 3 hahaha
Mh Kikwete nitamkumbuka sana, kila mwaka alikuwa anaongeza kitu kama laki hivi hii ilisaidia kupunguza msoto
 
Kama na ofisi ya umma na wana cheque number, Lawson haiwezi kukubali zaidi ya 2/3 ya mshahara kama makato. La bda utufafanunulie zaidi. Na pia inakuwaje mtu kama wewe una access na mafaili confidential?
 
Watumishi wa umma utawajua tu

Majungu na fitna hadi mitandaoni
 
Swala la 1/3 liko wazi kbs na linafanya kazi vzr, mleta mada ana hulka flani...
 
kweli?!!! sikuwa nafikiria kama mishahara inaguswa hivyo kipindi hiki, binafsi mi ni mtumishi pia na kuna wakati nilikwama kupita maelezo hadi nikakimbilia maboto. cha ajabu ni kuwa walinijibu sikopesheki kwa kiasi hicho nilichotaka sababu 1/3 haiukubali. nilishangaa maana niwajuavyo maboto/bayport kama ingelikuwa inawezekana basi lazima wangenipiga hela.........hawaachi fursa hiyo
 
Sheria za mikopo hautakiwi kukatwa zaidi ya 50% ya mshahara , hao watakuwa wamekopa kwenye vikoba na sio bank.
 
Usitegemee Mshahara kwa mfano mtu amekopa amenunua hiace anaingiza kila cku huo si ni Mshahara mwingine. Unataka watu wabweteke wategemee Mshahara. Inategemea umekopa kufanyia nin
 
Labda huko local government.
Maana mambo yao yanaendeshwa ki local zaidi.
Huku sisi sheria na kanuni zinazingatiwa.
Ila kama alikopa akiwa na akili timamu na anakatwa yeye mwenyewe tulia
 
Hizo salary slip za watu umeziona wapi?, acha kupotosha kama kenge!
 
Huyu itakuwa ana stationary anaprint salary slip za watumishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…