Utumishi, Wizara ya Fedha na TAKUKURU kwanini mnaruhusu watumishi wa umma kukopea mishahara yao hadi Senti ya mwisho? Hamuoni kuwa inachangia Rushwa?

Mkuu! Unae mdai kakudanganya mwambie hakuna mtumishi anayekopea mshahara wake mpaka abaki na sifuri
 
Lakini kuna watu wamekatwa Bodi ya Mikopo mpaka kinachobaki kwenye mshahara wao ni chini ya Tsh.100,000 (LAKI MOJA), wewe unaona ni sahihi. Mbona hawajazingatia hiyo 1/3?
 
Mtumishi wa Umma anamatatizo kibao hapo alipo anatembelea Kucha.Nawewe unaetaka asikopeshwe,unamtaka nini mtu huyu?Mind your own salary
 
Bank gani inaruhusu ukope 1/3 mzee. Je utumishi watapitisha mkopo Huo makato yafanyike. Labda useme kunawatumishi sio waungwana wanaacha kadi za benki na bima ya afya vibanda holela vya mikopo hapo nitaelewa.
 
Kitu nikichojifunza kama mzazi umeweza kumlipia mwanao mamilioni tangu chekechea hiyo mitatu ya chuoni malizia kumlipia ada tu, vinginevyo usizae mtoto tu. Mtu anabakia na mshahara 80,000 anazidiwa hadi na mlinzi anaelinda frem za duka barabarani.
 
Mshahara wangu unakuhusu nini? Acha wivu kopa na wewe
 

Sio kweli, iko hivi 1/3 ya mshahara wa mtumishi haiguswi ktk ku appraise mkopo, isipokuwa inaweza kutokea mkopaji amechukua mkopo kwa taarifa za wakati huo zinazosoma kwenye salary slip kwa maana ya Gross na net salary.
Baada ya muda kama alikuwa ni mnufaika wa bodi ya mikopo na mwajiri wake kusawasilisha taarifa zake na kuanza kukatwa hapo ndo hawataangalia hiyo 1/3 ya Grosd salary.

Pia inaweza kutokea mwanzo alikua anakatwa 8% na bodi ya mikopo lakini baada ya ongezeko na kuwa 15% lazima 1/3 iingile.
Sababu nyingine ni kama vile kushushwa daraja/cheo ambavyo vina impact n mshahara nk.
 
Hivi mwanangu mbona una wivu sana na maisha ya watu!kama mtu anawajibika kibaruani kwa nini uanze kumchawia hivi,kila mtu anamipango yake ya kuishi na kufanikiwa!mbona wanasiasa wanatoa rushwa husemi?kumbuka wivu ni mzizi wa dhambi!
 
1/3 huwa inabaki, sidhani kama inakombwa yote.
 
Chadema tu hao! LOL
 
haiwezekani, labda uko mitaani ndio kuna wakopeshaji wa asilimia 50 kwa mwezi huchukua kadi za watumishi. huku ndio takukuru wanakotakiwa kupita ingawa na wenyewe wanapigwa pia

Sent from my BLL-L21 using JamiiForums mobile app
 
Nadhan kuna kanuni fulani kwenye utumishi wa umma inawazuia majaji/mahakimu kutokukopa sana, kwa sababu hizo kazi zina mihela ya rushwa mingi sana pengine kuliko Nazi nyingine yoyote,ukiondoa tra-forodha
 
usiwapangie jinsi ya kuishi,wengine wana vyanzo vingine tofauti na mshahara
 
Mimi bodi ya mkopo waliponitia kidole nilibakiwa na 160,000/= hapo Nina mke na mtoto, kodi ya pango, nauli ya kazini na mengine mengi. Maisha yana siri nyingi sana
Uliishi vipi mkuu? Uliweza hata kuwa na mood ya kazi?
 
Mmmmmh.....
 
Uliishi vipi mkuu? Uliweza hata kuwa na mood ya kazi?
Kopa huku lipa kule, azima huku rudisha kule, zikitokea kazi za data entry unaomba nikipata kazini naaga ugonjwa na cheti cha daktari wiki 2 kazi imeisha unarudi yaani Fujo tupu sikuwa na mood ya kazi kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…