Basi Nenda
JF-Expert Member
- Jul 29, 2017
- 20,774
- 47,866
Unajua for most of us utumwa ni kama hadithi za kufikirika tu, ni ngumu sana kuamini kwamba eti mwarabu mmoja mwenye bunduki ya kipuuzi anaweza akateka watu 100 wenye akili zao, akawafunga minyororo wote na kuwasafirisha for miles bila shida yoyote ile, iliwezekanaje?
Watumwa ndani ya minyororo, wameridhiiika wenyewe, eti wanapigwa picha!
Mtoto mtumwa huko Zanzibar. Hapa anakula adhabu kali ya kusimama na gogo la kilo 30 kwenye jua kali bila viatu kwa muda usiopungua masaa 8 bila kula, hii ni kwa kosa la kimbwa sana sitalitaja hapa, linahusiana na yale mambo flani yale.
Hapa tunaona mbwa mmoja wa kizungu aliekuwa anaitwa T.H Williams akitoa tangazo linaloahidi donge nono la dollar 100 ya mwaka huo, (August 4, 1853) kwa yeyote atakaemrudisha mtumwa wake mrembo sana. Huyu binti Emily bila shaka alimlewesha kwa yale mambo yetu mpaka ana mtafuta kwa nguvu namna hii.
Hapa mtumwa akiwa kwenye maumivu makali sana. Sina uhakika sana, ila inawezekana alikuwa natengenezewa bangili ya kufungwa mnyororo, pia huyu mbwa wa kizungu inawezekana alikuwa anamtoboa enka, u neva know!
Hii picha ndio imenifanya nianze kupata majibu ya swali langu, yaani hao askari wanaowachunga wenzao kama ng'ombe wa maksai ni waafrika wenzetu kabisa. Hapa ni kwenye shamba la mpira (rubber plantation) lililokuwa likimilikiwa na wabelgiji na hao ni wakongoman. Haya ni mambo ya kimbwa kabisa. hiki ndicho wanyanyasaji wanachotufanya watanzania kwa kutumika na watu wa pua ndefu na ndevu nyingi.
huko congo mfalme Leopold 2 alifanya unyama sana mfano watu walikatwa mikono, wafanyakazi wa msituni waliotumwa kuchukua hiyo rubber walijinyunyuzia mwilini unajua rubber ni itomvu wa miti fulani ipo hapo congo so watumwa hawakupewa vyombo vya kubebea ilibidi wajinyunyuzie mwilini alafu inakauka na kunata muda huo huo huku ikiacha maumivu makubwa mno
kasheshe ipo kwenye kuitoa mwilini sasa
rubber ni kama super glue inavonata mwilini so imagine mwili wako wote tuupake super glue afu badae uitoe, waliteseka sana, pia kuna historia inafichwa juu ya watumwa wa Africa nimeisoma na kuigundua miaka 3 iliyopita, watumwa wa kiume walibakwa na baadhi ya wanaume wa kizungu na pia watumwa wa kike walibakwa na wanaume wa kizungu kuna tukio maarufu sana nitalileta humu kuna mtumwa wa kiafrica huko marekani wa kike alibakwa karibu kila siku siku ya mwisho alichoka akamuua master wake na yeye akajiua
Sent using Jamii Forums mobile app