Utumwa katika picha: Hivi iliwezekana vipi? Mbona Waarabu, Wahindi, Wachina hawakufanywa slaves?

Utumwa katika picha: Hivi iliwezekana vipi? Mbona Waarabu, Wahindi, Wachina hawakufanywa slaves?

Unajua for most of us utumwa ni kama hadithi za kufikirika tu, ni ngumu sana kuamini kwamba eti mwarabu mmoja mwenye bunduki ya kipuuzi anaweza akateka watu 100 wenye akili zao, akawafunga minyororo wote na kuwasafirisha for miles bila shida yoyote ile, iliwezekanaje?

slaves510x492.gif

Watumwa ndani ya minyororo, wameridhiiika wenyewe, eti wanapigwa picha!

Mtoto mtumwa huko Zanzibar. Hapa anakula adhabu kali ya kusimama na gogo la kilo 30 kwenye jua kali bila viatu kwa muda usiopungua masaa 8 bila kula, hii ni kwa kosa la kimbwa sana sitalitaja hapa, linahusiana na yale mambo flani yale.

Hapa tunaona mbwa mmoja wa kizungu aliekuwa anaitwa T.H Williams akitoa tangazo linaloahidi donge nono la dollar 100 ya mwaka huo, (August 4, 1853) kwa yeyote atakaemrudisha mtumwa wake mrembo sana. Huyu binti Emily bila shaka alimlewesha kwa yale mambo yetu mpaka ana mtafuta kwa nguvu namna hii.

SlaveShackle_450x397.jpg

Hapa mtumwa akiwa kwenye maumivu makali sana. Sina uhakika sana, ila inawezekana alikuwa natengenezewa bangili ya kufungwa mnyororo, pia huyu mbwa wa kizungu inawezekana alikuwa anamtoboa enka, u neva know!

Hii picha ndio imenifanya nianze kupata majibu ya swali langu, yaani hao askari wanaowachunga wenzao kama ng'ombe wa maksai ni waafrika wenzetu kabisa. Hapa ni kwenye shamba la mpira (rubber plantation) lililokuwa likimilikiwa na wabelgiji na hao ni wakongoman. Haya ni mambo ya kimbwa kabisa. hiki ndicho wanyanyasaji wanachotufanya watanzania kwa kutumika na watu wa pua ndefu na ndevu nyingi.

huko congo mfalme Leopold 2 alifanya unyama sana mfano watu walikatwa mikono, wafanyakazi wa msituni waliotumwa kuchukua hiyo rubber walijinyunyuzia mwilini unajua rubber ni itomvu wa miti fulani ipo hapo congo so watumwa hawakupewa vyombo vya kubebea ilibidi wajinyunyuzie mwilini alafu inakauka na kunata muda huo huo huku ikiacha maumivu makubwa mno
kasheshe ipo kwenye kuitoa mwilini sasa
rubber ni kama super glue inavonata mwilini so imagine mwili wako wote tuupake super glue afu badae uitoe, waliteseka sana, pia kuna historia inafichwa juu ya watumwa wa Africa nimeisoma na kuigundua miaka 3 iliyopita, watumwa wa kiume walibakwa na baadhi ya wanaume wa kizungu na pia watumwa wa kike walibakwa na wanaume wa kizungu kuna tukio maarufu sana nitalileta humu kuna mtumwa wa kiafrica huko marekani wa kike alibakwa karibu kila siku siku ya mwisho alichoka akamuua master wake na yeye akajiua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utumwa ulikuwepo na upo hadi leo. Huyo house girl wenu hapo ni mtumwa. Usibishe, fikiriaa wee utaona, sio mfanyakazi kama unavyoweza fikiria kwa haraka haraka; ni utumwa uliofanyiwa modification
 
SlaveShackle_450x397.jpg

Hapa mtumwa akiwa kwenye maumivu makali sana. Sina uhakika sana, ila inawezekana alikuwa natengenezewa bangili ya kufungwa mnyororo, pia huyu mbwa wa kizungu inawezekana alikuwa anamtoboa enka, u neva know!
Mpendwa inaonekana hasira imekushika kabla hujamaliza kuangalia picha. Mimi simwoni mtu anayeteswa, mimi namwona mtu anayefunguliwa nyororo zake.
Tafadhali angalia sehemu ifuatayo ya picha:

elementi.jpg

Ninatambua hapa sehemu zifuatazo: bangili ya chuma mguuni, bangili inashikwa katika jiriwa (kibanio) ya kifundi, askari Mzungu anashika msumeno wa chuma (nina uhakika maana ninao mmoja nyumbani). Anafanya nini? Ukiwa na bangili ya chuma na msumeno wa chuma - anakata bangili?
Kwa nini amebana bangili katika jiriwa? Labda isichezecheze asipate kuumiza mguu?
Mzungu huyu ni askari, picha imechukuliwa kwenye meli (nyuma unaona boti ndogo ya kujiokoa) kwa hiyo nahisi ni manowari fulani.
Sasa hujaleta habari kuhusu chanzo cha picha yako. Nikiangalia kofia ya askari, inawezekana ni mwanamaji Mjerumani (si lazima!). Kama ni vile ilipigwa Afrika ya Mashariki ambako manowari za Wajerumani zilitumiwa kwa muda mfupi kuzuia usafirishaji wa watumwa waliopelekwa Unguja. Wafungwa waliopatikana kwenye jahazi waliwekwa huru (hata kwa msumeno).

Lakini inawezeka pia alikuwa Mwingereza maana manowari za Waingereza kwa miaka mingi ya karne ya 19 zilikuwa na kazi ya kuzuia usafirishaji wa watumwa, zaidi kutoka Afrika ya Magharibi, lakini pia kutoka Afrika ya Mashariki. (linganisha West Africa Squadron)
(shughuli hizi zilianza 1807 baada ya wapinzani wa utumwa kule Uingereza kushika viti vingi bungeni na kuunda sheria ya kuzuia kwanza biashara ya kimataifa ya watumwa, baadaye pia utumwa mwenywe. Kabla ya hayo Waingereza walikuwa wafanyabiashara wa watumwa).
 
Utumwa katika picha: Hivi iliwezekana vipi? Mbona Waarabu, Wahindi, Wachina hawakufanywa slaves?
Mkuu, si vile. Utumwa ulipatikana karibu kote duniani.
* Waarabu walikuwa watumwa - maana bila hii Qurani isingekuwa na maelezo kuhusu watumwa
* Katika Ulaya kuna kundi kubwa ya makabila na mataifa, hadi leo wanaitwa "Slavonic" na lugha zao "slavonic languages", ni Warusi, Wabulgaria, Waserbia, Wakroatia, Wapoland, Waslovakia, Wacheki... Jina hili latokana na neno "slavi" iliyokuwa jina la watumwa; kwa sababu miaka 1000 iliyopita walikuwa makabila dhaifu bila maendeleo makubwa hivyo walikamatwa kama watumwa; hasa kabla ya kupokea Ukristo maana walifanya vita na mataifa ya Wakristo wa Ulaya Magharibi na wafungwa wa vita walikuwa chanzo kikuu cha watumwa; wafayabiashara waarabu walivamia Bahari Nyeusi na kuwanunua na kupeleka katika milki ya Waislamu.
* mzanzibari mashuhuri ni yule mama anayejulikana kama Sayyida Salme au "Princess Salme", au tangu kuolewa na Merumani kama "Emily Ruete"; mamake alikuwa binti kutoka nchi ya Georgia ya leo (kati ya Urusi na Uturuki) aliyeuzwa kama mtumwa na kununuliwa na sultani wa Zanzibar. Soma habari zake hapa: Emily Ruete - Wikipedia, kamusi elezo huru
 
Utumwa sio sisi tu wanatumikishwa Spain kwenye mashamba ya mbogamboga na wanaishi maisha ya duni kabisa
Nani kasema utumwa umeisha?

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Attachments

  • Adjustments.jpg
    Adjustments.jpg
    100.2 KB · Views: 2
Biashara ya Utumwa haikua Africa tu, nchi dhaifu au makabila dhaifu dhaifu duniani yalifanywa utumwa,
Tujitahidi kusoma historia,

BTW kukubali kua mtumwa wa mtu ni akili yako ndogo tu, pambana hadi mwisho,

Sema hapana kwenye utumwa.

Corona Virus: Stay Home the only Medicine found.
 
Mkuu, si vile. Utumwa ulipatikana karibu kote duniani.
* Waarabu walikuwa watumwa - maana bila hii Qurani isingekuwa na maelezo kuhusu watumwa
* Katika Ulaya kuna kundi kubwa ya makabila na mataifa, hadi leo wanaitwa "Slavonic" na lugha zao "slavonic languages", ni Warusi, Wabulgaria, Waserbia, Wakroatia, Wapoland, Waslovakia, Wacheki... Jina hili latokana na neno "slavi" iliyokuwa jina la watumwa; kwa sababu miaka 1000 iliyopita walikuwa makabila dhaifu bila maendeleo makubwa hivyo walikamatwa kama watumwa; hasa kabla ya kupokea Ukristo maana walifanya vita na mataifa ya Wakristo wa Ulaya Magharibi na wafungwa wa vita walikuwa chanzo kikuu cha watumwa; wafayabiashara waarabu walivamia Bahari Nyeusi na kuwanunua na kupeleka katika milki ya Waislamu.
* mzanzibari mashuhuri ni yule mama anayejulikana kama Sayyida Salme au "Princess Salme", au tangu kuolewa na Merumani kama "Emily Ruete"; mamake alikuwa binti kutoka nchi ya Georgia ya leo (kati ya Urusi na Uturuki) aliyeuzwa kama mtumwa na kununuliwa na sultani wa Zanzibar. Soma habari zake hapa: Emily Ruete - Wikipedia, kamusi elezo huru
Aisee!
 
A very deep thread, I hope itakua sticky

Tuna issues kwenye ubongo mkuu

I have always been asking myself, how come mwarabu mmoja au wawili wanaswaga watu mia?? lakini angekua mbantu ndio anaswaga wenzake, wangemgeuka na kumla nyama

We ahve demostrated a lot of inferiority kiasi kwamba ni vigumu kuamini kama we are not inferior
Mwarabu Mmoja mwenye utapia mlo anaiswaga mijibaba ya kibantu mia moja hadi bagamoyo huku akiwa na gobore lenye risasi moja

Mbona ndugu zetu Wamasai waliogopewa sana kiasi ambacho Mwarabu akikosea stepu alikuwa akidungwa mikuki mpaka kufanana na nungunungu ndani muda mfupi tu
Mbona ndugu zetu Wazimba walitengeneza mishikaki ya Waarabu 1500 huko Kilwa Kisiwani na kuwafanya kitoweo hadi wakawa wanacheua tasbihi

Wenyeji wa Kindu na maeneo yanaozunguka walikuwa na udhaifu wao tu Wabembe na Wamanyema ndio waliokubali kuswagwa pengine kwa hiari yao
 
Kaka historia yalo ya ajabu kidogo.
Wamaasai waliogopwa na wote, maana katika mwendo wao wa kupanua maeneo walimshambulia yeyote. Waulizie Wagikuyu, Wakamba, Wachagga.......

Kumbe Wazimba ndugu zako? Unajuaje? Hali halisi hakuna habari kuhusu hao isipokuwwa kumbukumbu ya kimaandishi iliyotungwa na mapadre 2 Wareno. Wataalamu wa historia wanavutana kiasi gani labda ni kweli na kiasi gani masimulizi tu. Nikifuatilia majadiliano yao uwezekano mkubwa walikuwa ama sehemu ya "Wamaravi" (mababu wa wasemaji wa Chichewa cha leo), au pia jina tu kwa aina mbalimbali ya makundi ya vijana waliozunguka nchi kwa kupora. Ukitaka kuamini masimulizi ya Wareno, walichinja na kula watu wote njiani - mwishoni pia Waarabu wa Kilwa; ilhali hao walikuwa wachache, walikula pia wakazi Waafrika wote.

Sasa unataka kuwapandisha cheo cha kuwa watetezi wa (nini???, nani???) dhidi ya "Waarabu"?? Hakika wala Wamaasai wala Wazimba walitofautisha kati ya adui na adui - tofauti ilikuwa tu windo jepesi au windo gumu.

Halafu - ukiangalia historia ya utumwa - sio kawaida ilikuwa machifu kukamata watu na kutafuta wateja baadaye? Waarabu kuwinda watumwa haikuwa kawaida (ilitokea kwa muda mfupi katika karne ya 19, kama Tipu Tipp). Karne zote za kabla jahazi za Waswahili, waarabu, Waajemi na kadhalika walifika tu pwani na kutafuta bidhaa zilizopatikana - ni wenyeji walioleta bidhaa. Pamoja na watumwa.
 
Kama tumenunulishwa chanjo dozi milioni 3 kwa lazima, kweli utumwa bado upo
 
Unajua for most of us utumwa ni kama hadithi za kufikirika tu, ni ngumu sana kuamini kwamba eti mwarabu mmoja mwenye bunduki ya kipuuzi anaweza akateka watu 100 wenye akili zao, akawafunga minyororo wote na kuwasafirisha for miles bila shida yoyote ile, iliwezekanaje?

slaves510x492.gif

Watumwa ndani ya minyororo, wameridhiiika wenyewe, eti wanapigwa picha!

Mtoto mtumwa huko Zanzibar. Hapa anakula adhabu kali ya kusimama na gogo la kilo 30 kwenye jua kali bila viatu kwa muda usiopungua masaa 8 bila kula, hii ni kwa kosa la kimbwa sana sitalitaja hapa, linahusiana na yale mambo flani yale.

Hapa tunaona mbwa mmoja wa kizungu aliekuwa anaitwa T.H Williams akitoa tangazo linaloahidi donge nono la dollar 100 ya mwaka huo, (August 4, 1853) kwa yeyote atakaemrudisha mtumwa wake mrembo sana. Huyu binti Emily bila shaka alimlewesha kwa yale mambo yetu mpaka ana mtafuta kwa nguvu namna hii.

SlaveShackle_450x397.jpg

Hapa mtumwa akiwa kwenye maumivu makali sana. Sina uhakika sana, ila inawezekana alikuwa natengenezewa bangili ya kufungwa mnyororo, pia huyu mbwa wa kizungu inawezekana alikuwa anamtoboa enka, u neva know!

Hii picha ndio imenifanya nianze kupata majibu ya swali langu, yaani hao askari wanaowachunga wenzao kama ng'ombe wa maksai ni waafrika wenzetu kabisa. Hapa ni kwenye shamba la mpira (rubber plantation) lililokuwa likimilikiwa na wabelgiji na hao ni wakongoman. Haya ni mambo ya kimbwa kabisa. hiki ndicho wanyanyasaji wanachotufanya watanzania kwa kutumika na watu wa pua ndefu na ndevu nyingi.
Tatizo ni umasikini wa kutupa wa mAfrica. Ilisabasha kusalitana kuanzia family mpaka uongozi uliokuepo na uliopo hadi sasa.

Kama leo tu viongozi wako wanaingia mikataba ya kitumwa utasemaJe hapo !!
 
Tatizo ni umasikini wa kutupa wa mAfrica. Ilisabasha kusalitana kuanzia family mpaka uongozi uliokuepo na uliopo hadi sasa.

Kama leo tu viongozi wako wanaingia mikataba ya kitumwa utasemaJe hapo !!
Ndio mimi nimeshangaa jinsi tulivyonunulishwa chanjo bila kupenda, viongozi kama hawa hata kutuuza utumwani hawashindwi!!
 
Alafu bado kuna watu wanaamini kuwa wazungu na waarabu wanatupenda. Ukitaka kuprove hili katangaze uchumba kutaka kuoa mwarabu uone reactions zao.

Sasa wewe naee lazima uolewe na mwalabu!!! Hoja zingine hazina mashiko. Mtu hataki utamlazimisha umuowe/akuowe!!!! Apo apo mtasema waarabu wabaguzi na makatili wakati siyo kabisaa. Waarabu wengiwao ni wa2 wema na wakalimu sana kuliko jamii yoyote.
 
Nimezungumzia kumuoa mwarabu ambaye mmependana, sijasema kulazimisha kuoa asiyekupenda. Read btn the lines
 
Huwezi kuwa mkweli ikiwa hutataja warabu ambao diyo walikuwa makatili na vinara wa kuchukua watumwa East Aafrica. Kinyume cha hapo, una agenda zako binafsi zisizo na maslahi wala tija kwa taifa.

Ikiwa una ushahidi wa kutosha kuhusu Waarabu na biashara ya utumwa tupia picha humu.
 
Back
Top Bottom