FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Ila jamani mimi niliishi Uarabuni miaka 3. Kiukweli waarabu wengi hawana u binadamu hasa kwa mtu mweusi. Bado wanaona mtu mweusi ni mtumwa tu. Nimeshuhudia mabinti wengi wadogo kutoka Africa hasa kutoka Ethiopia wanapoletwa uarabuni, ukiwakuta Airport kwakweli utaguswa tu maana nilishuhudia walikuwa kama 50 wanaongozwa kama ng, ombe na waliingizwa kwenye chumba kimoja nakufungiwa kumsubiria wakala aliyewaleta ili aje akamilishe taratibu za immigration halafu awagawe kwa watu walioweka order ya House girl. Na kinachofanyika huyo Agent anachukuwa Passport zao ili wasiweze kutoroka. Hivyo hata apate mateso kiasi gani hataweza kuondoka hadi wakala aliyewaleta akubali. Na hata maslahi yake yote yanalipwa kwa huyo wakala ndipo alipwe yeye kiasi atakachopangiwa na huyo wakala. Nilikuta kesi nyingi za nyuma za kuteswa na wengine kufariki kwakutupwa ngorofani na wake za matajiri zao wanapokuwa na hisia kuwa huenda wakafanya mapenzi na waume zao. Na kwavile nimeshaishi na wazungu basi kwa mtazamo wangu naona angalau Mzungu anathamini Utu na ubinadamu hata kama atakunyonya. Pia tukumbuke kuwa japokuwa biashara ya utumwa iliwanufaisha wazungu na waarabu lakini ni wazungu ndio walioanzisha campaign yakukomesha biashara hiyo. Mwarabu hakuwa hata na wazo hilo
Jee, umeiona hii picha? kuna mzungu au Mwaarabu hapo?
